MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

Sijawahi kusikia, haitatokea na wala haipendezi kusikia kitu kama Abdalah's law of motion au Khalfan's principle of ....... It sounds good unaposikia kitu kama Newton's Law of Motion, Charles's and Boyles's Law, Ohm's Law, Albert Einstain, n.k. Kwa hiyo, kinachotokea sasa hapa nchini, ni mwendelezo wa mambo yaliyoanza tangu enzi na enzi.

Hapo pekundu umeniacha hoi bi taaban
 
Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),
3. Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson,
4. Diana Matabwa (St Francis)
5. Neema Kafwimi (St Francis)
6. Beatrice Issara (Mary Goreti)
7. Johnston Dedani (Ilboru)
8. Samwel Emmanuel (Moshi Technical)
9. Bertha Sanga (Marian)
10.Bernadetha Kalluvya (St Francis).

Halafu miaka 15 ijayo hao wakishika nafasi za juu serikalini waislamu tunaanza ooooh tumebaguliwa, tunanyanyaswa, udini etc. Waislamu wenzangu tunaona hapo namba 1 hadi 10 hatupo, sababu nini? Kuina mchawiiiii. Mimi nilikataa kabisa kusoma madrasa nikang,ang,ana na elimu dunia na sasa naona matunda yake sina inferiority kama wengi wa waislamu tulivyo. UKWELI NI KUWA WAISLAMU TUWEKEZE KWENYE ELIMU DUNIA PIA hata mtume SAWS AMEAGIZA HIVYO....
 
Nina uhakika hizo shule kumi za mwisho nyingi zitakuwa za ndugu zangu wa nusu kwa nusu aka pasu kwa pasu kutokana na maeneo yake! Mniwie radhi ndg zangu siwatukani ila ndo ukweli wenyewe...mbaya zaidi nyingi ya shule hizo hapo juu zilizofanya vizuri ni za Wakatoliki!? :embarrassed:

Watasema wasahihishaji ni wakatoliki....yule mama si anaitwa Dr Joyce Ndalichako?
 
1.Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),

Halafu zis two ni wa kabila letu lileeee la kina lalu le shimboni mangiiii. Tukubali tukatae anaepanda kingi anavuna kingi wachaga ni mfano bora Tanzania.
 
1.Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),

Halafu zis two ni wa kabila letu lileeee la kina lalu le shimboni mangiiii. Tukubali tukatae anaepanda kingi anavuna kingi wachaga ni mfano bora Tanzania.

Na dawa ni kuwa TUWAOE na WATUOE kwa wingi ili TANZANIA yote tuwe kama wachagga na kuacha kulalama
 
Wadada wametia fora.

Wanafunzi kumi bora kitaifa

1. Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),
3. Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson,
4. Diana Matabwa (St Francis)
5. Neema Kafwimi (St Francis)
6. Beatrice Issara (Mary Goreti)
7. Johnston Dedani (Ilboru)
8. Samwel Emmanuel (Moshi Technical)
9. Bertha Sanga (Marian)
10.Bernadetha Kalluvya (St Francis).
 
Jamani mi nadhani we need to be serious. Aliye karibu hapo nashauri a-take hili swala aende pale baraza la mitihani aombe kumuona mkurugenzi..amuhoji haya maswali yote. Jamani mambo megine tuache kulalamika...as concerned citizens we need to do something. Mimi niko mkoani..I would have gladly done this!

Hii ni kazi ya TCRA! Hapa clearly anti-competitive practices are being practiced out in the open!! Tusiangalie dowans kila siku kuna vitu viingi sana vya kipuuzi vinaendelea kwenye maamuzi yanayo fanywa na watu walio serikalini!
 
..mbona mie jana nimepata hayo matokeo ya Form Four kwenye website yao? ni kweli hayakuwepo ila jana mchana waliweka.
 

Matokeo Kidato IV: Wasichana nafasi 8 za kwanza

MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne, uliofanyika Oktoba mwaka jana yametoka huku katika watahiniwa bora wa kitaifa, wasichana wakiongoza kwa asilimia 80 na wavulana kuambulia asilimia 20.

Matokeo hayo yanaonesha kati ya watahiniwa 10 bora kitaifa, wavulana ni wawili huku shule za seminari hasa za wasichana zikiendelea kuongoza kama ilivyo ada.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, amesema pamoja na mafanikio hayo kwa wasichana, kiwango cha ufaulu cha jumla kimeshuka.

Mwanafunzi wa kwanza bora Tanzania ni Lucylight Mallya wa sekondari ya wasichana ya Marian mkoani Pwani akifuatiwa na wasichana wenzake Maria-Dorin Shayo (Marian) na Sherryen Mutoka (Barbro-Johansson, Dar es Salaam).

Aliyeshika nafasi ya nne kitaifa ni Diana Matabwa akifuatiwa na Neema Kafwimi wote wa St. Francis na Beatrice Issara (St Mary Goreti, Kilimanjaro).

Nafasi ya saba ndiyo iliyoshikwa na mvulana Johnston Dedani (Ilboru, Arusha) na ya nane Samwel Emmanuel (Ufundi Moshi, Kilimanjaro). Lakini nafasi za tisa na kumi zilichukuliwa na wasichana, Bertha Sanga (Marian) na Bernadeta Kalluvya (St. Francis).

Moja ya vituko vilivyofanywa na baadhi ya watahiniwa ni pamoja na kuandika matusi kwenye karatasi za kujibia mitihani.

Dk. Ndalichako alisema wanafunzi hao walitukana kwenye karatasi za Biolojia, Historia, Kemia na Jiografia na kwa kosa hilo, wanafunzi hao wamefutiwa matokeo.

Licha ya mafanikio hayo kwa wasichana yanayodhihirisha kaulimbiu kwamba mwanamke akiwezeshwa anaweza, ubora wa kufaulu kwa madaraja unaonesha watahiniwa 40,388 sawa na asilimia 11.50 wamefaulu katika madaraja ya kwanza hadi la tatu.

Kati yao, wasichana waliofaulu ni 12,583 sawa na asilimia 7.81 na wavulana ni 27,805 sawa na asilimia 14.62.

Hata hivyo, wavulana ndio waliokuwa watahiniwa wengi katika mtihani huo, kwa kuwa wasichana waliosajiliwa walikuwa asilimia 45.88 na wavulana asilimia 54.12.

Mafanikio hayo kwa wasichana ni makubwa ikizingatiwa kuwa mfumo dume umekuwa ukiwaathiri katika masomo yao, ikiwamo kupangiwa kazi nyingi za nyumbani, kuliko wavulana na pia wengi waliacha shule kutokana na mimba.

Pia katika mlinganisho wa ufaulu wa mwaka jana na mwaka huu, matokeo hayo yameonesha kiwango kushuka. Wakati mwaka jana waliofaulu walikuwa asilimia 72.51 mwaka huu ni asilimia 50.40 tu.

Hali hiyo inaonesha tatizo si shule za kata kwa kuwa matokeo hayo, kwa shule hizo ni ya pili, lakini wadau wanahusisha matokeo mabaya na uamuzi wa Serikali wa mwaka 2008 wa kuruhusu waliofeli mtihani wa kidato cha pili, kuendelea na masomo bila kurudia mtihani.

Wanafunzi wengi waliofeli mtihani wa kidato cha pili, ndio waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana na matokeo yao kuwa mabaya kuliko mwaka uliopita.

Dk. Ndalichako alisema waliofanya mtihani walikuwa 352,840 sawa na asilimia 97.04 ambapo watahiniwa 10,749 sawa na asilimia 2.96 hawakufanya mtihani huo.

Shule 10 bora kwa kigezo cha ‘Grade Point Average A=1 na F=5 zenye watahiniwa zaidi ya 40 ni Uru Seminari ya Kilimanjaro, Marian na St.Francis.

Nyingine ni Cannosa, Feza Boys na Barbro Johanson za Dar es Salaam, Msolwa ya Morogoro, St Mary Goreti ya Kilimanjaro, Abbey ya Mtwara na St Joseph Sem Iterambogo ya Kigoma.

Shule 10 bora kwa kigezo hicho pia zenye watahiniwa chini ya 40 ni seminari ya Don Bosco, sekondari ya wasichana ya Bethelsabs ikifuatiwa na Seminari ya St. Joseph- Kilocha na seminari ya Mafinga zote za Iringa.

Nyingine ni Feza Girls ya Dar es Salaam, seminari ya Maua ya Kilimanjaro, Queen of Apostles Ushirombo ya Shinyanga, seminari ya Sengerema ya Mwanza na seminari ya Dungunyi Singida.

Alisema shule 10 za mwisho zenye watahiniwa zaidi ya 40 ni sekondari za Changaa, Thawi, Hurui, Kikore, Kolo zote za Dodoma, sekondari ya Pande Darajani ya Tanga, Igawa ya Morogoro, Makata ya Lindi, Mbuyuni na Naputa za Mtwara.

“Shule 10 za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40 ni Sanje ya Morogoro, Daluni ya Tanga, Kinangali ya Singida; Mtanga, Mipingo na Pande za Lindi; Imalampaka ya Tabora, Chongoleani ya Tanga, Mwamanenge ya Shinyanga na Kaoze ya Rukwa,” alisema Ndalichako.

Akizungumzia watahiniwa wa kujitegemea, alisema waliosajiliwa walikuwa 94,525 wakiwamo wasichana 49,252 sawa na asilimia 52.10 na wavulana 45,273 sawa na asilimia 47.90 na mwaka jana walikuwa 96,892 hivyo watahiniwa kupungua kwa 2,367 sawa na asilimia 2.44.

Alisema watahiniwa 88,586 wakiwamo wasichana 46,358 na wavulana 42,228 walifanya mitihani huku watahiniwa hao 5,939 sawa na asilimia 6.28 wakiwa hawakufanya mtihani.

Katika ufaulu ni watahiniwa 8,295 sawa na asilimia 35.17 ya waliofanya mtihani ndio waliofaulu ikilinganishwa na asilimia 28.82 ya waliofaulu mwaka jana, hivyo kiwango cha ufaulu kuongezeka kwa asilimia 6.35.

Matokeo ya watahiniwa 1,448 waliofanya mtihani bila kulipa, yamesitishwa hadi watakapolipa ada wanayodaiwa na faini katika kipindi cha miaka miwili na baada ya muda huo kumalizika, matokeo yatafutwa kwa mujibu wa kanuni za mitihani.

Ndalichako alisema wamesitisha matokeo ya wanafunzi wawili waliotumia sifa zinazofanana hadi wakuu wa shule watakapowasilisha nyaraka zinazothibitisha uhalali na mmoja mwenye namba S 3484/0014 kutokana na kutumia sifa za mtu mwingine hadi uchunguzi utakapokamilika.

Alisema pia Baraza limefuta na kuwaondoa katika usajili wa mitihani watahiniwa wanne wa sekondari za Kisaka na Nguvu Mpya kwa kutumia sifa za watahiniwa wengine.

Aidha, watahiniwa wengine 35 wa sekondari ya Bara wamefutiwa matokeo kwa kuwa walisajiliwa katika shule hiyo kwa kutumia majina ya watahiniwa waliochaguliwa kujiunga na shule hiyo lakini hawakuripoti.

Dk. Ndalichako alisema pia wamemfutia mwanafunzi wa sekondari ya Ludewa aliyefanya mitihani bila usajili.

Wengine waliofutiwa ni wanne wa sekondari ya Ibanda waliokuwa si wanafunzi halali wa shule hiyo na 42 walioondolewa baada ya kubainika sifa za kidato cha pili walizowasilisha hazikuwa sahihi.

“Watahiniwa wengine 56 wa kujitegemea tumewafutia matokeo baada ya kuondolewa kwenye usajili kwa kutokuwa na sifa za kufanya mtihani, lakini wakafanya mitihani katika vituo vya Mwigo Sekondari 29 na Twitange Sekondari walifanya 27,” alisema Dk. Ndalichako.

Aliongeza kuwa watahiniwa 311 wa shule na wawili wa kujitegemea, wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kufanya udanganyifu.

Alisema Baraza pia limefuta usajili wa kituo cha watahiniwa wa kujitegemea na mba P1189 cha Biafra, Dar es Salaam, kwa kukiuka taratibu za uendeshaji mitihani.

Kituo hicho kwa mujibu wa Dk. Ndalichako kilikuwa na watahiniwa wengi kuliko uwezo wake na kusababisha usumbufu uliofanya Kamati ya Mitihani ya Mkoa kuhamishia watahiniwa katika vituo vingine bila ushirikiano wa uongozi wa kituo.



Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 26th January 2011 @ 19:03
 
Aliyeongoza kidato cha nne ni yatima Wednesday, 26 January 2011 20:22

lucymallya.jpg
Lucylight Mallya

Mussa Juma, Arusha

MWANAFUNZI aliyeongoza mtihani wa kidato cha mne kitaifa mwaka 2010, Lucylight Mallya (18), amebainika kuwa ni yatima ambaye wazazi wake wote walifariki dunia miaka minne iliyopita.

Akizungumza katika mahojiano maalum, akiwa nyumbani kwa baba yake mkubwa kijiji cha Nguruma wilayani Arumeru, binti huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ya Marian, iliyoko Bagamoyo, mkoani Pwani alisema anamshukuru Mungu, walimu na walezi wake kwa kumwezesha kufaulu.

"Sikutegemea kuwa wa kwanza namshukuru sana Mungu, walimu, walezi wangu hasa baba mkubwa na mama na wote walionifikisha hapa ikiwa ni pamoja na wanafunzi wenzangu....," alisema Lucylight.

Lucylighty ambaye ni kwanza kati ya watoto, wanne walioachwa na marehemu wazazi walofariki dunia mwaka 2006 na (2007), alisema malengo yake ni kuwa daktari.

Binti huyo alisema wakati anafanya mtihani huo, somo aliloona gumu lilikuwa ni fizikia, lakini anamshukuru Mungu kuwa amefaulu vizuri na kuwa wa kwanza hapa nchini.

"Mimi nilikuwa napenda sana Kemia, Bailojia na Fizikia na nilikuwa nimejiandaa sana hivyo namshukuru Mungu kunisaidia kutimiza ndoto zangu," alisema Lucylighty.

Baba Mkubwa wa Lucy ambaye ndiye anamlea, Dominick Mallya alisema anashukuru Mungu kwa binti yake huyo kuongoza kitaifa.

Hata hivyo, Mallya alisema binti huyo amesoma katika mazingira magumu kwasababu hakuwa na fedha za kutosha hivyo alimwomba mmiliki wa shule hiyo, Father Valentine Bayo kumtafutia mfadhili.

"Mamshukuru Father Bayo kwani tangu mtoto huyu akiwa kidato cha pili hadi kumaliza kidato cha nne alikuwa analipiwa na wafadhili,"alisema Mallya.

Hata hivyo, aliomba wafadhili wa kumsaidia, ili aweze kuendelea ya masomo ya kidato cha tano hadi sita na chuo kikuu kwasababu yeye (Mallya) hanafedha za kutosha kuwasomesha watoto wote alionao.

"Baba yake Lucy ambaye ni mdogo wangu alifariki dunia mwaka 2006 na mkewe alifariki mwaka 2007, waliacha watoto wanne na mimi nina watoto watano hivyo tunashindwa kumudu gharama za kuwasomesha," alifahmisha Mallya na kuongeza:

"Tungependa kupata tena ufadhili wa Lucylight ili aweze kuendelea na masomo ya juu katika shule ambayo alikuwa akisoma".

Lucylight alizaliwa Jijini Dar es Salaam, miaka 18 iliyopita alisoma Shule ya Msingi St Mary's Tabata na baada ya alihitimu la saba mwaka 2006 alichaguliwa kwenda Shulea ya Sekondari ta Wasichana Tabora lakini aliamua kwenda Marian Girls alikohitimu kidato cha nne mwaka jana.

Taarifa za maendeleo yake zinaonyesha kuwa akiwa kidato cha kwanza alishika nafasi ya tatu, lakini kuanzia kidato cha pili hadi cha nne alikuwa akishika nafasi ya kwanza.

 
MATOKEO KIDATO CHA NNE: Wasichana wang'ara
• Shule za serikali zagaragazwa tena, seminari juu

na Betty Kangonga


amka2.gif
JUMLA ya watahiniwa 177,021 waliofanya mtihani wa taifa wa Kidato cha Nne Oktoba mwaka jana wamefaulu huku wasichana wanane wakishika nafasi kumi bora kitaifa.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, kiwango cha ufaulu kimeporomoka kwa asilimia 22.11 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka juzi.
Shule za binafsi hususan seminari zimeendelea kung'ara wakati zile za umma zikifanya vibaya na kushika nafasi za mwisho.
Katika matokeo hayo, wanafunzi wanne wamefutiwa matokeo kutokana na kuandika lugha ya matusi katika mitihani ya masomo ya Biolojia, Historia, Kemia na Jiografia.
Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Joyce Ndalichako, alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo ni zile zilizokuwa na watahiniwa kuanzia 40 na zaidi, ambazo ni Uru Seminari (Kilimanjaro), Marian Wasichana (Pwani), St Francis (Mbeya) na Canossa (Dar es Salaam).
Nyingine ni Msolwa (Morogoro), Feza Wavulana (Dar es Salaam), St Mary Goreti (Kilimanjaro), Abbey (Mtwara), St Joseph's Iterambogo (Kigoma) na Barbro - Johnson (Dar es Salaam).
Aliwataja wanafunzi walioshika nafasi kumi bora kitaifa kuwa ni Lucylight Mallya, Maria –Dorin Shayo wa Shule ya Wasichana ya Marian, Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson, Diana Matabwa na Neema Kafwimi wa Shule ya Wasichana ya St Francis.
Wengine ni Beatrice Issara wa St Mary Goreti, Johnston Dedani wa Ilboru, Samwel Emmanuel wa Moshi Technical, Bertha Sanga wa Marian na Bernadetha Kalluvya wa St Francis.
Hata hivyo, pamoja na wasichana kung'ara katika nafasi kumi za kwanza kitaifa, bado wavulana wameendelea kufaulu kwa wingi.
"Wasichana waliofaulu ni 69,996 sawa na asilimia 43.47 na wavulana ni 107,025 sawa na asilimia 56.28," alibainisha Ndalichako.
Alizitaja shule kumi za mwisho kitaifa zilizokuwa na watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni Changaa, Kolo, Kikore, Hurui, Thawi, (Dodoma), Pande Darajani (Tanga), Igawa (Morogoro), Makata (Lindi), Mbuyuni na Naputa (Mtwara).
Ndalichako alisema shule kumi bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo zipo katika kundi la watahiniwa chini ya 40 ni pamoja na Don Bosco (Iringa), Feza wasichana (Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro) na Queen of Apostle Ushirombo (Shinyanga).
Nyingine ni Sengerema Seminari (Mwanza), Sanu Seminari (Manyara), Bethelsabs Wasichana (Iringa), St Joseph –Kilocha Seminari (Iringa), Dungunyi Seminari (Singida) na Mafinga Seminari (Iringa).
"Pia zipo shule za mwisho ambazo zimefanya vibaya zilizokuwa na watahiniwa chini ya 40 kati ya hizo ni Sanje ya mkoani (Morogoro), Daluni (Tanga), Kinangali (Singida), Mtanga (Lindi), Pande (Lindi), Imalampaka (Tabora), Chongoleani (Tanga), Mwamanenge (Shinyanga), Mipingo (Lindi) na Kaoze (Rukwa)", alisema.
Jumla ya watahiniwa 311 na watahiniwa wawili wa kujitegemea wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.
"Baraza pia limefuta usajili wa kituo cha watahiniwa wa kujitegemea P1189 cha Biafra kutokana na kukiuka taratibu za uendeshaji mitihani…maana kituo hicho kilikuwa na watahiniwa wengi kuliko uwezo wake, jambo lililosababisha usumbufu," alisema.
Pia baraza hilo limetangaza kusitisha matokeo ya wanafunzi 1,448 ambao walifanya mitihani bila ya kulipa ada ya mtihani, ambapo watatakiwa kulipa na faini katika kipindi cha miaka miwili ili waweze kupewa matokeo hayo.
"Wanafunzi wawili wamefanya mtihani kwa sifa zinazofanana, hivyo tumesitisha matokeo yao hadi wakuu wa shule hizo watakapowasilisha nyaraka kuthibitisha uhalali," alieleza.
Ndalichako alisema watahiniwa 35 wa Shule ya Sekondari Bara wamefutiwa matokeo na kuondolewa katika usajili baada ya kutumia majina ya watahiniwa ambao walichaguliwa kujiunga na shule hiyo lakini hawakwenda kuripoti.
Alisema watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo kwa mwaka 2010 walikuwa 458,114 wakiwamo wasichana 216,084 sawa na asilimia 47.17 na wavulana 242,030 sawa na asilimia 52.83, ikilinganishwa na mwaka 2009 ambao walikuwa 351,152, hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa watahiniwa 106,962.
"Watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 441,426 sawa na asilimia 96.36 na watahiniwa 16,688 hawakufanya mtihani sawa na asilimia 3.64 ya waliosajiliwa," alifafanua.
 
Jamani tusiogope kuwaambia hao wenzetu ukweli ili kesho na keshokutwa wasije sema tena kuwa wameonewa.Ok utawala walioutaka umekaa madarakani miaka 5 tulitegemea na hizo Al...................zingekuwa zinatamba lakini wapi,Huko shuleni kwao wanasoma nini?Inabidi ufanyike mtihani wa kujiunga na vyuo vikuu ili wajue uwezo baina ya St. na Al. isije ikawa vyuo vya wenzetu wanatoka wahitimu wasokuwa na weledi.Poleniiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Joyce Ndalichako, alisema shule kumi bora zilizokuwa na watahiniwa kuanzia 40 na zaidi,ni

1. Uru Seminari (Kilimanjaro),
2. Marian Wasichana (Pwani),
3. St Francis (Mbeya)
4. Canossa (Dar es Salaam).
5. Msolwa (Morogoro),
6. Feza Wavulana (Dar es Salaam),
7. St Mary Goreti (Kilimanjaro),
8. Abbey (Mtwara),
9. St Joseph's Iterambogo (Kigoma)
10.Barbro - Johnson (Dar es Salaam).

Wanafunzi kumi bora kitaifa

1. Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),
3. Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson,
4. Diana Matabwa (St Francis)
5. Neema Kafwimi (St Francis)
6. Beatrice Issara (Mary Goreti)
7. Johnston Dedani (Ilboru)
8. Samwel Emmanuel (Moshi Technical)
9. Bertha Sanga (Marian)
10.Bernadetha Kalluvya (St Francis).

Shule kumi za mwisho zilizokuwa na watahiniwa 40 na zaidi ni

1. Changaa, 2. Kolo, 3. Kikore, 4. Hurui, 5. Thawi, zote kutoka Dodoma
6. Pande Darajani (Tanga),
7. Igawa (Morogoro),
8. Makata (Lindi),
9. Mbuyuni na 10. Naputa kutoka Mtwara.


My take: .

Kwa nadharia ya maksi, watoto walioongoza ndiyo hao, lakini ukiunganisha na mazingira ya shule, idadi ya walimu, vifaa vya kufundishia, muda wa kusoma nk, kama kuna mtoto ameweza kupata DIV1 tena kafaulu masomo ya sayansi toka shule ya kata yenye walimu watatu tu, nadhani nae angefikiriwa kuwa katika wale bora. Kwa maana nyingine pamoja na ku-rank wanafunzi kwa maksi tu, waangalie pia mazingira wanayosomea. Kama wanaweza kusema wafanyakazi katika mazingira magumu waongezewe posho maalum, then wanafunzi katika mazingira hayohayo watathminiwe tofauti. Kwa mfano angalia mwanafunzi huyu, shule ina waalimu watatu na iko kijijini sana, hakuna umeme, hajawahi kuona computer, radio anaweza kusikiliza za uganda au Rwanda tu. Inaitwa Nyabishenge S3064/0031 M EDSON MNYAMBO FORTUNATUS 17 I CIV-B HIST-B GEO-C KISW-C ENGL-B PHY-C CHEM-C BIO-D B/MATH-B
 
Thamani ya elimu imeteremshwa sana na ufisadi na hivi sasa ni dhuluma inaamua ajira za wasomi wetu serikalini na hili linachangia sana vijana wengi kutojituma darasani..................

Hoja ya kujiajiri inayosambazwa na warasimu serikalini haina mashiko kwa vijana wengi kwa sababu vijana hujiuliza ............mbona hao warasimu mbona hawaachi ngazi na kwenda kujiajiri?

Vile vile hakuna mazingira mazuri ya kuwawezesha vijana wetu waweze kujiajiri........na kujiajiri vijana wengi waona ni debe tupu ambalo haliachi kutika.............................

Kwa hiyo kufanya vizuri au la hasha hakuna uhusiano na utashi wa mtu bali inatagemea sana mtazamo wake wa mwanafunzi juu ya faida ya elimu.....................
 
Vijana hawa wengi watapiga kura 2015 na wengi hawataichagua CCM...... wengi ni waitachagua chadema....
 
Lucylight Mallya,(Marian),
2. Maria –Dorin Shayo (Marian),
3. Sherryen Mutoka wa Barbro - Johansson,
4. Diana Matabwa (St Francis)
5. Neema Kafwimi (St Francis)
6. Beatrice Issara (Mary Goreti)
7. Johnston Dedani (Ilboru)
8. Samwel Emmanuel (Moshi Technical)
9. Bertha Sanga (Marian)
10.Bernadetha Kalluvya (St Francis).

Halafu miaka 15 ijayo hao wakishika nafasi za juu serikalini waislamu tunaanza ooooh tumebaguliwa, tunanyanyaswa, udini etc. Waislamu wenzangu tunaona hapo namba 1 hadi 10 hatupo, sababu nini? Kuina mchawiiiii. Mimi nilikataa kabisa kusoma madrasa nikang,ang,ana na elimu dunia na sasa naona matunda yake sina inferiority kama wengi wa waislamu tulivyo. UKWELI NI KUWA WAISLAMU TUWEKEZE KWENYE ELIMU DUNIA PIA hata mtume SAWS AMEAGIZA HIVYO....

Mkuu nakubaliana na wewe kwa asilimia 200 kuhusu umuhimu wa elimu. Madrassa ni muhimu pia na ina umuhimu wake katika jamii, lakini ilmu dunia, kwa mazingira ya hapa duniani ni namba moja.
 
Wana JF kutokana na trend ya perfomance ya shule za sekondari za serikali mi nafikiri tuzigeuze shule zote seminary kwa kuzikabidhi makanisa mi naona serikali imeshindwa kuziendesha( MA SHEKHEH TUUNGENI MKONO KWA HILI)
 
Back
Top Bottom