Matokeo ya Darasa la VII 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya Darasa la VII 2009

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kaitaba, Dec 10, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Leo hii waziri wa elimu anatarajiwa kutoa matokeo ya darasa la saba, watakaopata data waturushie
   
 2. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Invissible tusaidie kupata Annalysis ya shule zilizofanya vizuri na wilaya zinazotoka top ten na shule kumi za mwisho,then tusaidie rank kimkoa,wilaya
   
 3. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Pia hata kwa wale wanaosikia vyombo vya habari k.m redio na t.v wakiona anaanza kuyataja watueleze ili tuanze kufuatilia.
   
 4. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimepata habari kupitia TBC taifa sasa hivi kuwa kufahulu kumeshuka kwa 3.3% na wengi wamefeli engilish na hisabati.

  wenye habari za mtandaoni watujulishe.
   
 5. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mwananchi

  Nusu wafeli mtihani darasa la saba,445,954 waenda kidato cha kwanza


  Na Leon Bahati  WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba yanayoonyesha kuwa zaidi ya nusu ya wanafunzi watahiniwa wa mwaka huu, wamefeli huku 445,954 wakichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.

  Matokeo hayo yaliyotolewa jana yanaonyesha kuwa kati ya wanafunzi 999,070 waliofanya mtihani huo, wanafunzi 505,737 ambao ni sawa na asilimia 50.6 wamefeli na wanafunzi 493,333 ambao ni sawa na asilimia 49.4 wamefaulu.

  Kwa mujibu wa matokeo hayo, wasichana 285,374 na wavulana 220,363 wameshindwa mtihani huo kwa kupata chini ya alama 100 za jumla ya masomo yote. Kwa mujibu wa wizara, jumla ya alama za masomo yote ni 250 na kiwango cha juu cha ufaulu ilikuwa ni alama 235.

  Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Magembe alisema kati ya waliofaulu, wasichana ni 217,250 sawa na asilimia 43.3 na wavulana ni 276,083 sawa na asilimia 55.7.

  Waziri alisema miongoni mwa waliofaulu tayari 445,954 wamechaguliwa kwenye awamu ya kwanza ya watakaojiunga kidato cha kwanza katika sekondari za serikali mwaka ujao.

  "Wanafunzi 445,954, sawa na asilimia 89.5 ya waliofaulu, wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika sekondari za serikali," alisema Profesa Magembe.

  Alibainisha kuwa awamu ya pili ya kuchagua watakaojiunga na sekondari hususan zile mpya za kata, unaendelea na matokeo yake yanatarajiwa kutangazwa wakati wowote.

  Profesa Magembe alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafunzi waliofaulu wanapata nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza.

  Kwa mwaka huu, waziri alisema alama ya juu ya ufaulu kitaifa kwa wavulana ni 235, wasichana 233 wakati ya chini kwa wote ni 100.

  Akizungumzia kuhusu kiwango cha ufaulu, Profesa Magembe alisema mwaka huu umeshuka kwa asilimia 3.3 ikilinganishwa na mwaka jana.

  Pamoja na hali hiyo, alisema mkoa wa Dar es Salaam ndio unaoongoza kwa kufaulu huku Shinyanga ikishika mkia wakati watahiniwa 579 wamefutiwa matokeo kutokana na tuhuma za kufanya udanganyifu.

  Kwa mujibu wa takwimu za matokeo hayo zilizotolewa jana, Dar es Salaam inaongoza katika mikoa iliyofanya vizuri, ikifuatiwa na Arusha, Iringa, Manyara, Ruvuma, Kagera, Tanga, Pwani, Morogoro, Mwanza na Kilimanjaro.

  Mikoa iliyoshika mkia, inaongozwa na Shinyanga, Singida, Tabora, Kigoma, Dodoma, Lindi, Mara, Mtwara, Mbeya na Rukwa.

  Profesa Magembe alisema wanafunzi 1,024,488 walitarajiwa kufanya mtihani huo uliofanyika Septemba 9 na 10, lakini wanafunzi 25,418 walishindwa kufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali.

  Ingawa sababu hizo hazikuwekwa wazi, waziri alisema kwamba tofauti na miaka mingine kigezo cha mwanafunzi kuzuiwa kwa sababu ya mimba hakikuwepo.

  "Tangu mwaka jana, tuliagiza kwamba hata kama mwanafunzi atakuwa mjamzito, aruhusiwe kufanya mitihani," alisema Profesa Magembe.

  Katika hali nyingine, Profesa Magembe alisema kwamba tatizo sugu la wanafunzi nchini kufanya vibaya katika masomo ya Kiingereza na hisabati, limeendelea kujirudia.

  Katika somo la Kiingereza walifaulu kwa asilimia 35.4 na hisabati asilimia 21 hali ambayo Profesa Magembe alisema imepanda kidogo ikilinganishwa na mwaka jana.

  "Ukilinganisha na mwaka jana utaona ufaulu wa masomo ya hisabati na Kiingereza, umepanda kutoka asilimia 31 hadi 35 na hisabati kutoka asilimia 18 hadi 20," alisema Magembe.

  Pamoja na hali hiyo, Profesa Magembe alisema tatizo sugu la wanafunzi wa shule za msingi kutofaulu masomo hayo linatokana na msingi mbovu walio nao walimu wanaofundisha masomo hayo.

  Alisema wizara imekusudia kuweka mkakati wa kuwapiga msasa walimu waliopo na nguvu kubwa zaidi itapelekwa kwenye vyuo vya walimu.

  Ufaulu wa mwaka huu kwa kila somo alisema, Kiswahili ni asilimia 69.1, sayansi 53.4 na maarifa 59.5.

  http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=16581
   
 6. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  sasa kama nusu ya wanafunzi wamefeli tunajivunia kweli kwamba tumeongeza idadi ya wanafunzi au tuliwapeleka kukua? Maafa zaidi tuyategemee form four. labda watunge mtihani wa kuuliza what is your name. kwa kweli serikali yetu ni wababaishaji sana la kwenye majukwaa wanajisifu kinoma.
   
 7. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  baraza la mitihani mnayabania matokeo hadi lini? yamwageni basi!
   
 8. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbeya jamani vipi. Mbona haikuwakilisha vizuri? Hata Moa wa Mara pia ni kama umepunguza sana makali kulikoni? Mara mkoa uliotupa Mwisenge na Musoma Alliance?!

  Hii inatisha wake up Mbeya.
   
 9. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wilaya gani ni ya mwisho ili mkuu wa wilaya aji-Mnari.
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  nasikia mbeya wamepelekwa walimu wa upe tu na ni kampeni ya kupunguza akina mwakyembe wengine...sijui km hii ni kweli
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  nusu ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wamefeli..........................
  ''''ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA''''
   
 12. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Walimu wa voda vasta hawawezi kuchangia hali hii, let us increase our seriousness on our education system otherwise we will cry forever for being labour marked to our neighbour (EA community)
   
 13. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2009
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Suala si waalimu peke yao. Waalimu wanatoa tu mwongozo darasani. Wazazi na vijana wenyewe wanatakiwa wawe na juhudi ya kujihimiza kufuatilia kilichofundishwa. Wazazi wanatakiwa wawawajibishe waalimu na hata watoe mikakati mbali mbali ya elimu. Sitaki kuendekeza ukabila, lakini angalieni wenzetu wa mikoa mingine ambavyo huwa wanatoa pesa zao binafsi ( michango NK) kujenga shule na kuwahimiza vijana wao. Mbeya inaweza kufanya vizuri tu kama wala ndizi wenzetu wengine wanavyofanya.
   
 14. Tuntu

  Tuntu JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mkoa wa mbeya,Afisa Elimu wa mkoa amekuwa ni bomu kupita kiasi,yeye hana kabisa na uamasishaji wa walimu katika kutoa elimu bora,yeye kakalia tu kunyanyasa walimu na kutumia cheo chake kuwapata walimu wa kike,tena ofisini kwake wanapokwenda kwa masuala ya kiofisi,Mkoani wanataarifa zake,sijui kwanini bado wanamwachia tu huku mkoa unazidi kushuka kielimu.
   
 15. M

  Mwaihojo Member

  #15
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ifike mahala Maafisa elimu wa wilaya na mikoa iliyofanya vibaya kuliko ilivyokuwa kabla wao hawajakabidhiwa madaraka hayo wawajibishwe,lazima tuwe serious kwenye suala la elimu!!
   
 16. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  naomba msaada wa kukumbushwa tarehe ya kuanza mtihan wa form 4 wa mwaka 1999 na kumaliza pia na ya form 6 ya mwaka 2002.
   
Loading...