Matokeo ya darasa 7 kitaifa yachukua sura ya mtihani wa mock mkoa

Rose Mutwe

Member
Nov 9, 2011
16
0
Ndugu wa JF
Haijawahi kutokea serikali kutumia matokea ya mock mkoa darasa la saba kufanya selection, mwaka huu hilo limefanyika. Je huko ni kutatua tatizo au kuendeleza udhaifu? Je wanaweza kutatua tatizo kwa kuficha ukweli?

Nawasilisha
 

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
1,195
Ndugu wa JF
Haijawahi kutokea serikali kutumia matokea ya mock mkoa darasa la saba kufanya selection, mwaka huu hilo limefanyika. Je huko ni kutatua tatizo au kuendeleza udhaifu? Je wanaweza kutatua tatizo kwa kuficha ukweli?

Nawasilisha

Chanzo cha habari ni kipi?
 

big f

Member
Nov 26, 2012
60
0
Ndugu wa JF
Haijawahi kutokea serikali kutumia matokea ya mock mkoa darasa la saba kufanya selection, mwaka huu hilo limefanyika. Je huko ni kutatua tatizo au kuendeleza udhaifu? Je wanaweza kutatua tatizo kwa kuficha ukweli?

Nawasilisha

Athari za PASSIVE RESISTANCE ya walimu zaanza kuonekana, serikali yashusha viwango vya ufaulu huku ikijinasibu eti kiwango cha ufaulu kimepanda. Wadanganyeni hao hao wasiojua kuchanganua mambo. Kauli hii ya waziri kwamba ufaulu umepanda ni sawa na ile isemayo uchumi wa nchi umekua wakati hali ya mwananchi wa kawaida inazidi kudidimia. Matokeo ya Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ni matokeo ya ubabe wa serikali. Matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu ni vituko na aibu kubwaaa! Baada ya serikali kukomaaa kutowasikiliza walimu na kukimbilia mahakamani kukwepa na kusitisha mgomo wa walimu leo wameamua kushusha kiwango cha ufaulu. Kwa mara ya kwanza Eti mwaka huu wanafunzi waliopata alama D yaani alama chini ya 100 wamefaulu na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari. Ni ajabu kusikia kuwa kuna wanafunzi wenye alama 70 mpaka 50 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari. Bado tuna bomu kubwa tunalisubiri la idadi ya wanafunzi walioingia kidato cha kwanza wasiojua kusoma na kuandika, maana yake mtihani wenyewe ulikuwa wa kuchagua hadi somo la Hesabu, aibu kubwa kwa nchi hii. "Shame of this Government".
 

no9

Senior Member
Nov 11, 2010
190
0
sasa hivi kama mwalimu tunaye muandaa ni wa daraja la nne tena d4 tena kwa masomo tofauti kuna kitu hapo
 

mzeelapa

JF-Expert Member
Jul 14, 2010
1,100
1,500
Kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu kwa kupunguza alama za ufaulu ni kosa kubwa. Kwa kuwa tumeruhusu wanafunzi wasio na uwezo kwenda sekondari, ndio hao hao watakaosababisha zoezi kama hili kuendelea kidato cha pili, baadae kidato cha nne. Si ajabu kidato cha sita na vyuo vikuu. Ili elimu ipande inatakIwa kuwe na ushindani kufaulu kuanzia darasa la saba.
Miaka ya nyuma wakati shule za sekondari zilipokuwa chache kulikuwa na ushindani mkubwa kwa wanafunzi na walimu katika kuingia sekondari, ndio maana waliotutangulia wana uwezo mkubwa kulinganisha na wanafunzi wa sasa, na bado tunajidai elimu inakua, kwa kupeleka wastani wa alama 20 sekondari? SHAME.. Enzi hizo huna wastani wa alama 70 sekondari utaisikia redioni labda unde shule za binafsi, na ilikuwa inaeleweka kabisa waliosomea shule za binafsi ni wale waliofeli darasa la saba (Ukiacha shule za Agakhan-Wahindi na seminary) sasa hivi kinyume. Inasikitisha na sijui tunaipeleka wapi nchi hii. Tusubiri mikataba mibovu, uchumi mbovu, uongozi mbovu yaani kila kitu kitakuwa kibovu.

Maoni yangu ni kwamba ufanyike utafiti kujua nini kifanyike katika kuboresha elimu, bila kuwahusisha watumishi wa wizara ya elimu. Tuache siasa za eti elimu imekua kwa kupeleka watoto wengi sekondari zisizo na ubora. Afadhali kuwa na shule chache zilizo bora kuliko kuwa na shule kila kata zisizo na elimu bora.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom