Matokeo ya CHADEMA uraisi 2015 kushuka ukilinganisha na Matokeo ya 2010.

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Kwa mwenendo wa kutangaza matokeo unavyokwenda, zipo dalili kubwa kwamba mgombea uraisi kupitia CHADEMA kwa mwavuli wa vyama vinne vinavyounda umoja wa UKAWA, zipo dalili kwamba mgombea huyo ambaye ni Edward Lowasa akapata matokeo hafifu zaidi mwaka huu ukilinganisha na matokeo ya Dr. W. Slaa ya mwaka 2010 katika nafasi ya uraisi.

Mwaka 2010 waliopiga kura walikuwa milioni 8 na Dr. W. Slaa kupitia Chadema bila kuwepo muungano wa vyama alipata takribani kura milion 2 kati ya 8. Sawa na 25%.

Mwaka huu 2015 waliopiga kura wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 15 na mgombea wa huyo wa uraisi kupitia Chadema, kwa matokeo ya awali inaonyesha atapata chini ya 30% ambapo kura atakazopata jumla hazitafika milioni 5 na ni za vyama vinne kwa wastani wa kura milioni 1 za chama chake.

Katika kampeni za uchaguzi huu tumeshuhudia vituko vingi lakini hali halisi ndiyo hiyo. Tanzania ya leo usipopinga ufisadi na rushwa hawatakuelewa.
 
Huo ni mtizamo wako. siwezi kuupinga manake sijui upeo wako wa kufikiri. hoja. zako nyepesi sana hat kukujibu nahisi nakupa chart.
 
Okoa ccm inayoparaganyika kwa kasi ya ajabu!
Haya chadema yaache tu
 
Back
Top Bottom