Matokeo ya CAG yakipuuzwa, ukaguzi wa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya CAG yakipuuzwa, ukaguzi wa nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by salisalum, May 24, 2011.

 1. s

  salisalum JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mwaka 2006/7 kulikuwa na halmashauri 100 ambazo zilipata hati safi za ukaguzi, idadi hii imeanguka hadi halmashauri 65 tu zilizopata hati safi mwaka 2009/2010, ikionesha kushuka kwa ubora wa kusimamia fedha za umma. Pia idadi ya halmashauri zenye kasoro imeongezeka mara mbili, na ukaguzi wa ndani umekuwa dhaifu mno kulinda rasilimali za umma. Kwa mfano, report ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikari (CAG) inaonesha kwamba asilimia 91 ya halmashauri zote, kitengo cha ukaguzi wa ndani ni butu; asilimia 64 ya halmashauri mazingira yake ya uthibiti wa ndani ni dhaifu na asilimia 86 ya halmashauri zote mfumo wake wa mahesabu hautoshelezi.


  Matokeo haya ni utafiti na ufuatiliaji makini ulivyofanyika hivi punde na hawa jamaa wa Uwazi. Raisi alipotoa hotuba alisema hali ya utunzaji na utumiaji wa fedha za serikali ime-improve. Akasema sema kiswahili chake siku ile lakini kama nilikuwa simwelewi. Viongozi wetu mgonjwa yuko mahututi watakwambia aah huyu, mbona atakuwa discharged leo asubuhi!  Kama kuna kutokujali basi nchi yetu inaelekea hatarini. Nimefurahia huu uchanganuzi wa hawa jamaa.  full report hii hapa: http://uwazi.org/uploads/files/If%20findings%20are%20ignored%20why%20audit%20Swahili%20Final.pdf
   
Loading...