Yaliyojiri matokeo ya Mbunge jimbo la Buyungu na uchaguzi wa madiwani kata 36 Tanzania bara

hugochavez

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,907
1,009
Habari wakuu, leo ni uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma na uchaguzi wa madiwani kata 79 Tanzania Bara. Katika uchaguzi wa mbunge jimbo la Buyungu kuna upinzani mkubwa sana kati ya mgombea kutoka CCM na CHADEMA.

=====

Fuatili kinachojiri hapa;
3cb9b31d-5dfb-42c4-8784-e22e650cd098.jpeg

39036923_2091957467732206_7081217395297091584_n.jpg

Mgombea wa CCM Christopher Kajoro Chiza, Kashinda Ubunge Jimbo la Buyungu (Kakonko),

BUYUNGU, KIGOMA: Zoezi la kuhesabu na kujumlisha kura kutoka vituo mbalimbali lamalizika saa 11:12 alfajiri ya leo

> Chiza C Kajoro wa CCM ameibuka mshindi kwa kupata kura 24,578 huku Elia F. Michael wa CHADEMA akipata kura 16,910. CCM 58% CHADEMA 40% others 2%

Update kutoka Arusha
Chadema wajitoa katika uchaguzi kata ya Songoro, Arusha baada ya mgombea wao na mawakala kupigwa. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amethibitisha

MATOKEO
> Omari Mzee(CCM) ametangazwa mshindi udiwani kata ya Makorora, Jijini Tanga

> Juma Ramadhani(CCM) ametangazwa mshindi kata ya Mabokweni, jijini Tanga

> Alex Mwinuka(CCM) ametangazwa mshindi udiwani Kata ya Mwanganyanga, wilayani Kyela, Mbeya,baada ya kupata kura 867

> Emilian Siwingwa(CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa Udiwani katika Kata ya Mpona, Wilayani Songwe

> Apaikunda Naburi(CCM) ametangazwa kuwa mshindi katika Kata ya Mawenzi, Wilayani Moshi baada ya kupata kura 400 kati ya 569

> MATOKEO YA UDIWANI TARIME: Mgombea wa CCM Chacha Ghati ametangazwa mshindi wa udiwani kata ya Turwa Wilaya ya Tarime mkoani Mara baada ya kuibuka kidedea kwa kupata kura 1401 dhidi ya mgombea wa CHADEMA Charles Mnanka aliyepata kura 1121.
turwa.jpg

Pichani ni Agai, Gerald Mwita Martine na Emily Solo, wakiwa wameshikilia hati ya ushindi ya udiwani kata ya Turwa

Bu1.jpg

Zoezi la upigaji kura likiwa linaendelea jimbo la Buyungu


Kaloleni.jpg

Mgombea wa udiwani Kata ya Kaloleni(Arusha) kupitia CHADEMA akiwa amelazwa baada ya kupigwa vibaya
DkZMe8aWsAEqzst.jpg
 
Hata kwa amani hii utasikia chadema wanalia wamepigwa na kuzuiwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.
 
Back
Top Bottom