Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,493
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi. Margaret Sitta ametangaza matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambapo matokeo ya mwaka huu yameshuka toka asilimia 70.48 mwaka jana hadi asilimia 54.18. (sawa na asilimia 16) Kati ya wanafunzi 792,102 waliojiandikisha kufanya mtihani huo wanafunzi 20,000 hawakuweza kufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali. Na wale waliofanya mtihani ni wanafunzi 419,198 ndio waliofaulu kuendelea na elimu ya sekondari. Kimasomo kati ya wale waliofaulu asilimia 82 walifanya vizuri katika Kiswahili, 66% Sayansi, 56.39% Maarifa,31.21% Kiingereza, na 17.42 Hisabati. Kati ya wasichana waliofanya mtihani ni asilimia 45.39 ambao walifaulu na kati ya wavulana wote waliofanya mtihani ni asilimia 62.52 waliofaulu. Asilimia 90 ya wasichana waliofaulu wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza kwenye shule za serikali mwakani na upande wa wavulana ni asilimia 88 waliopata nafasi kwenye shule za serikali.
Kwa mujibu wa mama Sitta, Serikali inafanya tathmini na kufanya utafiti wa "haraka na wa kina" ili ielewe ni kwanini kumekuwa na kushuka huko kwa kiwango cha kufaulu.
Kwa mujibu wa mama Sitta, Serikali inafanya tathmini na kufanya utafiti wa "haraka na wa kina" ili ielewe ni kwanini kumekuwa na kushuka huko kwa kiwango cha kufaulu.