Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
MATOKEO MAZURI AU MABAYA YANATEGEMEANA NA MSINGI ULIOWEKA
Kama umewahi kuona jengo lolote kubwa, najua ulishaona, ila unapokuta jengo hilo tayari limekamilika, huwezi kujua msingi ni mkubwa kiasi gani. Hii ni kwa sababu msingi umefichwa.Kama umewahi kuona mwanzo wa ujenzi wa majengo makubwa sana, msingi pia huwa unakuwa mkubwa sana, na unazidi kufichwa, yaani unakwenda mbali zaidi.
Wewe utaona jengo la ghorofa nyingi kwenda juu, lakini hujui huko chini kumefichwa nini.
Utakubaliana na mimi ya kwamba kama unaishi kwenye nyumba ya kawaida ambayo sio ghorofa, mtu akikuambia leo anataka aongeze nyumba hiyo kwenye ghorofa tano juu utamshangaa sana. Na kama ni nyumba yako hutakubaliana na hilo, kwa sababu unajua ni hatari, unajua msingi wa nyumba hiyo haukuandaliwa kwa ajili ya ghorofa, bali kwa ajili ya nyumba ya kawaida.
Hivi pia ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kila siku na mafanikio.Chochote unachoona kipo juu, wale wote ambao unaona wamefanikiwa sana, wale wote ambao unatamani kuwa kama wao, hawakufika tu pale siku moja, bali walijenga msingi imara sana uliowawezesha kufika pale.Na vibaya zaidi ni kwamba msingi huo hauonekani, umefichwa.
Na sio kwamba wao ndio wameuficha, bali jamii ndio imeficha, kwa sababu hadithi zao za mwanzo hazifurahishi, bali zinazofurahisha ni hizi za sasa, alitoka kuuza nyanya na sasa anamiliki viwanda. Ila ile hadithi ya kati kati, kutoka kwenye nyanya mpaka viwanda, wengi hawaitafuti, ambayo hii ndio msingi mkuu kabisa.
Chochote unachotaka kwenye maisha yako, unahitaji kukijengea msingi. Na msingi unaojenga sasa, ndio utakaoamua mbele yako inakuwaje, kama unajenga msingi wa nyumba ndogo, ina maana unajiondolea nafasi za kuwa na ghorofa baadaye. Ndio maana ni muhimu sana kuwa na malengo makubwa na ambayo unayafanyia kazi, huu ni msingi mzuri sana kwako.
Unajenga msingi kwa kuweka malengo makubwa sana ambayo yatakusukuma kila siku.
Unajenga msingi kwa kuchukua hatua kubwa zaidi ya ulizozoea kuchukua. Unajenga msingi kwa kujifunza mambo mapya kila siku na kuyatumia kwenye maisha yako. na unajenga msingi kwa kuamua kutokukata tamaa na kuwa king’ang’anizi.
Je unajenga msingi wa nini?