Matokeo kutangazwa vituoni si CCM wala UKAWA wanahitaji kushangilia

kajekudya

kajekudya

JF-Expert Member
1,050
2,000
Ukiangalia siasa za mwaka ni dhahiri kuna wanaume wawili wanumiza nyasi, yaani JPM wa CCM na ENL wa CDM/UKAWA. Wanaume hawa wamekuja na staili mpya, staili ya kutengeneza mafuriko lengo likiwa ni kuuaminisha umma wa Tanzania na dunia kwa ujumla kwamba wanakubalika, pamoja na njia zingine nyingi zinazotumika mojawapo ni kuwaleta watu wa maeneo au mikoa jirani kwenda kutengeneza mafuriko eneo mkutano unapofanyika, kweli wanafanikiwa maana watu wanajaa mpaka wengine wanakufaa au kuzimia kwa kukosa hewa au kukanyagana. Lkn kuna kitu hapa hawakiangalii, tareh 25 watu hataweza kutoka eneo moja kwenda lingine kupiga kura, yaani kama una wafuasi 50 katelelo halaf siku ya mkutano wako pale ulileta watu 300 ili utengeneze mafuriko kumbuka tareh 25 ni watu 50 tu watakupigia kura pale katelelo. ninachosema ni kuwa mwaka huu yanaweza yakatokea maajabu kwa either kati ya hawa wawili mmoja kushindwa vibaya, na hakutakuwa na visingizio maana kura zimehesabiwa kila kituo, ingekuwa tofauti kama mfumo wa zamani ungetumika maana amabaye atashindwa angesingizia wizi wa kura wkt wa kusafirisha masanduku na watu wangemuamini maana wakt wa kampeni alipata watu wengi bila kujali wametoka wap, lkn kwa mtindo huu, itakuwa ngumu maana mafuriko hayatakuwa na nafasi ck ya uchaguz ndo maana nasema si CCM wala UKAWA WANASTAHILI KUFURAHIA maana maana wote wanatumia mtindo mmoja, lakin tare 25 itaweka wazi kama kweli haya mafuriko ni ya kweli au feki.
 
J

jebibay

JF-Expert Member
1,413
1,225
Utaratibu upi wa zamani unaouzungumzia ? Kwenye uchaguzi wa 2010 kura zilihesabiwa vituoni na kubandikwa vituoni. Hakuna jambo jipya hapo.
 
makedonia

makedonia

JF-Expert Member
2,168
2,000
CCM nzima hamumwezi lowasa hakyanani.....
 
mr.London

mr.London

JF-Expert Member
2,733
2,000
CCM ndio hubeba watu kutoka sehemu mbali mbali kuja kwenye mikutano kwamfano Diamond analipwa fedha nyingi kuvuta watu kwenye mikutano ya ccm sasa hili ungelitolea mfano kwa ccm. Litawadhuru CCM kwa asilimia kubwa mana mpaka watoto huenda kuongeza idadi hukaa mbele kumchek diamond ilhali wao hawapigi ata kura
 
Lateni

Lateni

JF-Expert Member
677
225
Ukiona ccm wamekubaliana na huu utaratibu wa kura kuhesabiwa vituoni basi ujue tayari wamesha andaa mpango mpya wa goli la mkono.

Ninakuwa na mashaka na vitambulisho feki vya kupigia kura na mawakala wa upinzani kununuliwa dakika za mwisho kwenye chumba cha kuhesabia kura. Hapa ndipo pana goli la mkono.
 
mgt software

mgt software

JF-Expert Member
12,102
2,000
Hata mje na wajukuu lowasa anapita kama mvua
 
Y

Yodoki II

JF-Expert Member
4,880
2,000
Kwa hali ilivyo,yeyote anaweza kushnda.Mashabiki mjiandae kisaikolojia kwa matokeo chanya na hasi vingnevyo kuna watu watajitia vitanzi.
 
1

1954

JF-Expert Member
7,457
2,000
CCM peke yake ndio hubeba watu kwenda mkutanoni? Nilibahatika kuhudhuria mkutano mmoja waUKAWA kusini mwa Tanzania. UKAWA ilisafirisha watu kwa malori na mabasi kwenda kwenye mkutano/ Watu hao walilipiwa nauli ya kwenda tu na baada ya mkutano wakakwama ikabidi mgombea mmoja wa ubunge wa CCM kuwalipia kwa '' huruma ikiwa ni namna ya kukejeli UKAWA
 
M

Mba Ta Sanja

JF-Expert Member
384
0
1954 we' mwongo, siku hiyohiyo tungeiona humu.Kina Faizafoxy walikuwa wapi wasiilete humu?
 
mpasuajipu99

mpasuajipu99

JF-Expert Member
679
195
CCM peke yake ndio hubeba watu kwenda mkutanoni? Nilibahatika kuhudhuria mkutano mmoja waUKAWA kusini mwa Tanzania. UKAWA ilisafirisha watu kwa malori na mabasi kwenda kwenye mkutano/ Watu hao walilipiwa nauli ya kwenda tu na baada ya mkutano wakakwama ikabidi mgombea mmoja wa ubunge wa CCM kuwalipia kwa '' huruma ikiwa ni namna ya kukejeli UKAWA
Longolongo phuuuuu
 
hk.com

hk.com

JF-Expert Member
818
0
but ulinzi wa kura ni muhimu tunaogopa mawakala wasijefika bei.
 
DE FULE

DE FULE

JF-Expert Member
1,153
2,000
CCM peke yake ndio hubeba watu kwenda mkutanoni? Nilibahatika kuhudhuria mkutano mmoja waUKAWA kusini mwa Tanzania. UKAWA ilisafirisha watu kwa malori na mabasi kwenda kwenye mkutano/ Watu hao walilipiwa nauli ya kwenda tu na baada ya mkutano wakakwama ikabidi mgombea mmoja wa ubunge wa CCM kuwalipia kwa '' huruma ikiwa ni namna ya kukejeli UKAWA
Mkuu hawawezi kukubali kamwe, juzi wametoa Watu Zenji kupitia Nungwi kuwajaza tangamano lkn wamekalia kusema ni CCM pekee, hapo ndo kuna tatizo....
 
T

tufe

JF-Expert Member
750
195
Hakuna kilichobadika baba,mfumo ni ule ule. Kura zote zinahesabiwa kituoni na matokeo yanabandikwa vituoni. Lubuva atafute jengine la kusema sio hili, kwani hili lipo tangia zama za jaji MAKAME.
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
13,138
2,000
CCM ndio hubeba watu kutoka sehemu mbali mbali kuja kwenye mikutano kwamfano Diamond analipwa fedha nyingi kuvuta watu kwenye mikutano ya ccm sasa hili ungelitolea mfano kwa ccm. Litawadhuru CCM kwa asilimia kubwa mana mpaka watoto huenda kuongeza idadi hukaa mbele kumchek diamond ilhali wao hawapigi ata kura
It is very true.

Hilo la kura zote za udiwani, ubunge na Urais kuhesabiwa na kubandikwa vituoni ni big blow kwa CCM na Magufuli wao na it is very very big advantage kwa Lowassa na Ukawa.

Kwa kuwa siyo siri kuwa lile goli la mkono ambalo Nape alikuwa akitamba nalo ndiyo hilo la kutotangaza matokeo ya Urais vituoni na kusafirisha maboksi ili njiani waingize maboksi yao ili yakawaongezee 'hesabu' wakati wa kuhesabu upya kura hizo wilayani.

Kwa bahati nzuri sana goli hilo la mkono la maccm 'Refa' Lubuva ameliona na amelipigia filimbi ya kuligomea.
 
Kunta Kinte

Kunta Kinte

JF-Expert Member
3,687
1,500
Utaratibu upi wa zamani unaouzungumzia ? Kwenye uchaguzi wa 2010 kura zilihesabiwa vituoni na kubandikwa vituoni. Hakuna jambo jipya hapo.
Unachosema wewe sicho alichosema mwenyekiti wa tume, tukuamini wewe au yeye?
 
Forum statistics

Threads
1,425,226

Messages
35,085,100

Members
538,249
Top Bottom