Elections 2010 Matokeo Kijiji Cha Kigarama, Kanyigo, Nkenge (Kagera)

Kishaju

Senior Member
Feb 23, 2008
106
62
Urais
CCM: 382
Chadema: 342

Udiwani: sijapata kamili ila mgombea wa chadema amemzidi wa CCM kwa kura 61

Kijiji cha nshuma naambia slaa kamzidi JK kwa kura 8, na kwenye udiwani wa CCM amemzidi wa chadema kwa kura 12.

Ubunge - wameairisha ila huyu mama anayegombea hakuwa na mpinzani.
 
Tunachoweza kusema hali ya Chadema nchi nzima inatia matumaini sana..........................
 
kagera kwa shemeji tenaaaa... najua kule tunachukua kila kitu.... ndo itakuwa zawadi ya first lady kwa rais
 
Matokeo Kijiji Cha Kigarama, Kanyigo, Nkenge (Kagera)
Urais
CCM: 382
Chadema: 342

Udiwani: sijapata kamili ila mgombea wa chadema amemzidi wa CCM kwa kura 61

Kijiji cha nshuma naambia slaa kamzidi JK kwa kura 8, na kwenye udiwani wa CCM amemzidi wa chadema kwa kura 12.

"Ubunge - wameairisha ila huyu mama anayegombea hakuwa na mpinzani."


Hata wewe mheshimiwa Kishaju umechakachuliwa?

Ukweli ni kwamba huyu mama na chichiem wenzake wamekuwa wakitumia nguvu ya peasa kununua waandishi wa habari na kuandika habari za uongo kwamba huyo mama hana mpinzani lakini sio kweli. Jiulize kwa nini uchaguzi ngazi ya mbunge umeahirishwa?
Hapo Nkenge yupo mgombea wa upinzani kupitia TLP Bwana William Kweyamba na ukweli ni kwamba mpaka sasa amekuwa tishio kwa huyo mama Asumpta Mshama wa chichiem. Wameshatumia mbinu nyingi ikiwemo vitisho, kutaka kumnunua na hata juzi na jana baada ya William Kweyamba kuonyeshwa kwenye karatasi za uchaguzi kuwa ni wa UDP badala ya TLP wakamshawishi sana ili ajitoe uchaguzi uendelee na huyu mama apite bila kupingwa lakini jamaa akakataa. Walikuwa wakimwambia aseme kiasi chochote anachohitaji kama gharama alizotumia mpaka sasa wamrudishie ili ajitoe zoezi la uchaguzi liendelee.
Baada ya jitihada zote za chichiem kushindwa basi uchaguzi umeahirishwa mpaka baada ya siku 90 kwani tume ilichemsha kwenye makatasi ya kura kama nilivyoeleza hapo juu.

Ni kweli kwamba Mgombea wa CHADEMA alijitoa, na yule wa CUF akapata skendo akafungwa wakati wa kampeni hivyo hilo jimbo ni vita kati ya chichiem na TLP. Bahati mbaya habari zake hazikuwa available hapa JF.
Habari ndiyo hiyo tusichakachuliwe na chichiem kuamini kuwa yule mama hana mpinzani WHILE ukweli ni kwamba anapumulia machine kwa upinzani uliopo NKENGE kwa kilaza Kamala.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom