Elections 2010 Matokeo haya yasiwavunje moyo wanamapinduzi, bado liko tumaini, aluta continua...

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
170
Kila mpenda mabadiliko amehuzunishwa na matokeo ya uchaguzi hasa kwa sababu haki haikutendeka. Lakini ni muhimu kufahamu kuwa kuhuzunika tu hakutoshi. Ni muhimu kukumbuka kuwa kazi ya kuleta mabadiliko ya kifikra ni kazi kubwa inayohitaji uvumilivu, subira na utayari wa kulipa gharama za kila namna.

Nawasihi wapenda mabadiliko msikate tamaa, tuutazame uchaguzi huu positively. Pamoja na kutofikia azma yetu, tujue kuwa hata hivyo tumepiga hatua. Tuna idadi ya viti bungeni ambayo hatukuwa nayo, tumefanikiwa kuwasha moto wa shauku ya mabadiliko kwa umma wa watz. hasa vijana, ambayo haitazimika kirahisi. Tuna mtandao wa kichama karibu kila mkoa sasa kwa viti vya wabunge na madiwani. Hapa nataka kusema kuwa, tumepata vituo ambavyo ni mahali pa kuanzia kujieneza mpaka vijijini. Hii ni strength kubwa. Tutumie mambo haya kuendeleza mapambano ya mabadiliko.

Kampeni kwetu sisi hazijaisha, ndo kwanza zimeanza. Bado ni asubuhi sana, kazi bado kubwa. Tusiweke silaha chini, twende mbele. ALUTA CONTINUA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom