Matokeo Darasa la Saba: Shinyanga, Singida na Tabora Kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo Darasa la Saba: Shinyanga, Singida na Tabora Kulikoni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rev. Kishoka, Dec 13, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Shinyanga, Singida na Tabora, je kuna nini mpaka theluthi mbili ya watoto wa shule za msingi wameshindwa kufaulu mtihani wa darasa la saba?

  Je Wabunge kutoka mikoa hii, mnatuambia nini sisi Wananchi tunaposoma matokeo haya?

  Je mtasingizia uhaba wa fedha, waalimu na vitendea kazi au ujaa uzito wa Wasichana au watoto kutumika kama wafanyakazi?

  Mikoa yenu ina hazina kubwa ya mazao ya chakula na biashara na ongezea madini.

  Sasa ni tathmini gani kwenu kimkoa na kitaifa mtatupa?

   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  swali la kujiuliza hapa ni je tunafaulisha zaidi au tunafelisha zaidi!?
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,

  Kama tunafaulisha, basi isingekuwa mambo mabaya namna hi hasa Shinyanga kushika mkia kwa mara ya pili mfululizo.

  Kama ni kufelisha, iweje mikoa mingine inapeta kwa namna? Je mfumo wetu wa elimu una ubaguzi kuwa sehemu fulani zinaneemeka na nyingine zinadumaa?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Reverend.. lakini tumeambiwa shule za msingi na sekondari zimejengwa nyingi sana karibu kila kata, idadi ya walimu imeongezwa n.k so.. nadhani tunafeulisha!
   
 5. m

  madule Senior Member

  #5
  Dec 13, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mh! inasikitisha sana..
  Jamani wekeni mkakati juu ya hilo
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Swali ni hivi, je ubora wa mfumo wa elimu ukoje? Je ubora na viwango vya uelewa na ufundishaji wa walimu wetu ukoje?

  Je tukuangalia sababu nyingine kama lishe, maji, umeme, ajira za watoto, afya na miundombinu tunaweza kusema Shinyanga, Singida na Tabora vina uduni wa kila kiotu mpaka watoto washindwe mtihani wa darasa la saba kwa kiwango kikubwa namna hii?
   
 7. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hizo ndo faida ya fodafasta. wananchi wanaambiwa wajengemajengo then wapeleke wanafunzi, ingekuwa rahisi hivi basi uarabuni wote wangekuwa juu kielimu. Haya ndo matokeo ya siasa kuingilia elimu.
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Je tufanyeje ili tuongeze idadi ya wanaoelimika? Je kufeli Darasa la Saba ni kukosa elimu?
   
 9. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hapa manyema aibu tupu ndugu....kufeli darasa la saba ndio foundation stage elimu ndio inaporomoka kwa serikali kuendekeza hanasa badala kuwaongezea walimu posho hakuna equality kwenye kula cake ya taifa nahisi kama kuna sabotage kwa walimu ila niwe mkweli sina uhakika kwa hili
   
 10. GY

  GY JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hivi kufeli darasa la saba ni kufanyeje? ni kukosa nafasi ya kwenda sekondari ya umma ama? Maana sikumbuki kama nilishawai kupewa cheti kinachoonyesha matokea yangu ya darasa la saba
   
 11. A

  Amanikwenu Senior Member

  #11
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna uwezekano mkubwa kuwa wengi wa vijana wetu waliofeli mtihani wa darasa la saba wana tatizo la kujua kusoma na kuandika vizuri. Hivi hawa vijana zaidi ya laki tano kila mwaka tutawapeleka wapi? Kwangu mimi tatizo letu kubwa ni USANII yani utendaji mbovu.
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Je wanafelishwa ili tuendelee kuwa na kundi la wasio elimika na kutumika kama vibarua?
   
 13. GY

  GY JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ndio maana niliuliza kufeli maana yake ni kukosa nafasi shule ya umma ama? ikiwa ndio maana yake, na kwakua shule nyingi za umma siku izi ni hizi za kata ambazo ni za kutwa, basi kuna uwezekano mkubwa perfomance ya mkoa kwenye elimu ya darasa la saba inategemea idadi ya shule za umma ilizonazo. Probably mikoa uliyoitaja ina shule chache sana za sekondari za umma, na ndio sababu ziko chini kimatokea?

  Am just thinking!
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Dec 16, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka,

  ..kuna tukio mkoani Mara ambapo viongozi walishangaa kukuta wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika ktk moja ya sekondari za kata.

  ..binafsi nadhani huu mpango wa sekondari za kata unawaswaga kwenda sekondari wanafunzi ambao hawako-qualified. sasa sijui utaratibu huu utaendelea mpaka lini.

  ..halafu kinachoogopesha zaidi ni kwamba kuna maeneo wamejizatiti kujenga mpaka form 5 na 6 za kata. lakini ukiangalia hizo O-level walizonazo hazina viwango vya kupasisha wanafunzi kwenda A-level.

  ..kwangu mimi ni bora tukazingatia zaidi VIWANGO/UBORA badala ya IDADI ya shule/wasomi.

  ..ningependa pia kuona tunajielekeza ktk kuwatafutia remedial opportunities wale ambao hawakupasi kwenda form 1 na form 5. kwenye nchi za wenzetu kuna opportunities kama Community colleges etc. hapa kwetu labda VETA ingeweza kusaidia kuwapiga msasa hawa wanafunzi na baadaye kuwapa elimu ya ufundi.

  ..pia ningependa kuona wanafunzi waliopitia mfumo wa VETA wanapatiwa nafasi ya masomi ya ELIMU YA JUU. kama mwanafunzi wa Community College kwa nchi za wenzetu anaweza kufika chuo kikuu, basi hapa kwetu mwanafunzi aliyepitia VETA awe na uwezo wa kuungana na wenzake waliopitia sekondari kufika chuo kikuu.
   
 15. E

  ESU New Member

  #15
  Dec 15, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MENGI NI MAPITO,MATOKEO MAZURI YATAPATIKANAJE?TABORA IMENG'ANG'ANIA WABUNGE BWANYENYE!!!!!!!!!!!!!!ACHA TUCHEMSHE,BUT ONE DAY,WATAFUNGUKA MACHO WAONE,DR,ELIAS.
  :embarrassed:
   
 16. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Ni mkakati maalumu wa mafisadi wa Si Si Em kuiacha mikoa hii isiamke ili wasidai chao.
  si unajua tena almas,dhahabu ndo zimejaa kwao
   
 17. u

  utiyansanga JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2010
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  InasikitisA SANA! HUKU NDIPO NGOME YA CCM(ANGALAU SHINYANGA WAMEANZA KUONA NYOTA) HAYA NDIO MAJIBU YA KWANINI TUPO HIVI NA SIO ILE !MPAKA WATAKAPO AMKA NDIPO WATAKAPO PATA UKOMBOZI ILI KUHAKIKISHA UJINGA ZAIDI NENDA KWENYE MATOKEO YA FORM FOUR UTACHOKA! SHEKULU WAKULIGWE!:hungry: SPESHO KWA SINGIDA.....hii ni aibu kwenu wa KInampanda,longero,Iguguno,KIsiriri,NDAGO ,VIPI MNAKUNYWA BIA MJINI NCHI YENU INAANGAMIA! KUMBUKENI KIKWETE ALIPATA%86!
   
 18. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Hapo umesahau Kilimatinde an Ikungi.
  Dawa ni kuiondoa Si Si Em
   
 19. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #19
  Dec 17, 2010
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,802
  Likes Received: 1,045
  Trophy Points: 280
  ni kukosa wastani wa alama 20 kwa 50 kwa masomo matano yaliyotahiniwa
   
 20. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Nakuunga mkono kwa asilimia mia moja mkuu. Moja ya matatizo makubwa ya mfumo wetu wa elimu na ambao tumerithi toka kwa Muingereza ni kuweka kipaumbele katika masomo ya darasani na kuipa kisogo elimu ya ufundi. Siku hizi kila mtu anashabikia shahada na vyeti vya kalamu na sio ujuzi wa mhitimu. Elimu ya ufundi inapaswa kurudishwa toka shule ya msingi ukianza na somo la Sanaa, Sayanzi Kimu, Kilimo na hata mpaka useremala. Ni vizuri elimu ya sekondari ikawa ya namna mbili ila zote zenye uzito sawa, ufundi na mainstream academia. Ukweli ni kwamba si kila mtoto aendaye shule ana uwezo wa kufaulu masomo yale ya kukariri na ni vyema tukalitambua hilo na kuanza kuwasaidia toka waliwa wadogo kwa kuwapa ujuzi wa kuwasaidia katika maisha.

  Matatizo mengine ya sekta ya elimu yapo mengi tu kama vile matumizi mabaya na ufinyu wa bajeti, idadi na viwango visivyoridhisha vya walimu pamoja na vitendea kazi.

  It's high time tukaangalia namna gani wenzetu wa nchi za Scandinavia, Ujerumani n.k wanavyothamini elimu ya ufundi na mfumo mzima wa Apprenticeship katika kuendeleza taaluma za vizazi vyao vichanga
   
Loading...