Matokea kura za Uspika yanatia shaka kimahesabu!!

shostsm

New Member
Nov 13, 2010
3
0
Kwa kuzingatia idadi ya wabunge wa CCM ndani ya bunge letu, ni dhahiri kila mtu alitegemea Mh Ana Makinda angeshinda kirahisi kabisa katika kinyang’anyiro cha Uspika. Pamoja na matarajio hayo, lakini inatia shaka kidogo jinsi takwimu zinavyotangazwa.
Matokea jinsi yalivyotangazwa:
Watu waliopiga kura: 327
Kura zilizoharibika: 9 (2.7%)
Ana Makinda: Kura 265 (74.2%)
Mabere Marando: Kura 53 (16.2%)
Analysis:
9+265+53=327 OK
2.7% + 74.2% +16.2% =93.1%; hapa ndipo mashaka yangu yanapoanzia; je 6.9% sawa na kura 22 zimeenda kwa nani.
Kama asilimia zilizoandikwa ni sahihi basi:
Kura zilizoharibika 2.7% ni sawa na kura 9
Ana Makinda 74.2% ni sawa na Kura 243 (sio 265)
Mabere Marando 16.2% ni sawa na watu 53
Jumla kura 305
Pamoja na kwamba ninaamini kwamba Ana Makinda ameshinda, lakini nina mashaka, na kuna kila dalili kwamba matokeo halisi ya kura siyo haya. 74.2% ya Ana Makinda ilipangwa tangu kabla ya uchaguzi ukizingatia kuwa wabunge wa CCM wapo 251 ambayo ni sawa na 74.3% ya wabunge wote. Tatizo ni kwamba waliopewa kazi hii ya kuhalalisha kura hizi hesabu zinawapiga chenga wameshindwa kupika vizuri mahesabu yao.
Nionavyo mimi Ana Makinda kashinda lakini chini ya 74.2%; Mabere Marando kapata at least 23.1% yaani zaidi ya kura 76. Hii inapunguza kidogo zile hasira kwamba vyama vingine vya upinzani hawakumpigia kura Marando. Imani yangu ni kwamba Marando kazoa kura zote za upinzani na chache za CCM, siyo hizo zilizotangazwa.
Pamoja na kwamba Halima Mdee alikuwepo kama wakala, lakini lolote linaweza kutokea, CCM are capable of doing anything – atakuwa kapigwa chaga la macho.

Hata matokeo ya kura za Uraisi hesabu zake hazieleweki. Ukijumlisha kura walizopata wagombea pamoja na zilizoharibika unapata waliopiga kura ni 8,626,303 lakini tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa waliopiga kura ni 8,626,283. Hapo kuna tofauti ya kura 20, kuthibitisha kuwa matokeo hayo ni ya kupikwa au KUCHAKACHULIWA. NEC watupe majibu sahihi.
 
Back
Top Bottom