Naomba kuelimishwa kuhusu matumizi ya matofali ya ukubwa tofauti kwenye ujenzi

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,881
872
Habari ya asbuhi wana jukwaa na wadau wote.

Naomba tuelimishane kuhusu tofali za ujenzi za cement manake hua naona kuna tofali za urefu, upana na unene tofauti tunapokua tunajenga nyumba zetu ziwe ni za makazi, biashara au makazi na biashara:-

1. Kuna tofali za nchi sita hizi wajenzi wengi huzitimia kwenye kujengea msingi.

SWALI langu, je hizi tofali ni kwa ajili ya kujengea msingi tu pale unapokua unajenga nyumba?

2. Kuna tofali za nchi tano hizi tofali hutumika sana kwenye ujenzi wa kuta za nje na ndani

SWALI langu, hizi tofali ni kwa ajili ya matumizi hayo na ni matumizi sahihi?

3. Inawezekana kujengea nyumba tofali za nchi tano peke yake?(kwa maana ya msingi, kuta za nje na ndani)
athari za kutumia hizo (tofali 5")ni zipi kigharama na kiubora katika ujenzi?

Karibuni wataalam mtupe hiyo elimu.
 
Haya maswali yatakuwa magumu toka asubuhi hakuna aliyejitokeza ! Lakini tuvumilie tutakula mbivu.
 
Hakuna Tofali malum Kwa ajili ya msingi Tofali za inchi 5 waweza jengea msingi.
 
Kwanza nianze kuelezea utofauti wa tofali la inch 5 na 6. Utofauti ni upana/width tu ila vipimo vingine vinalingana (length = 18' na height = 9'). Hivyo yanatofautiana kwenye unene tu.

Ubora wa matofali ya block yanaanzia kwenye aina ya mchanga, kiasi cha cement, uchanganyaji (Kiasi cha maji na muda way kukoroga), ushindiliaji (vibration) na umwagiliaji (maji ya kutosha kwa siku 7: unaweza kuloweka pia). Hivi vikizingatiwa vyema utapata tofali gumu sana.

Tofali la inch 6 n Nene na linashawishi kulazwa kwa ajili ya msingi kwa kuwa utafika juu mapema. Hii inafanya mafundi wengi wanapenda kuyatumia kuwekea msongi ili pia kuepusha layers (kushikilia layer ni ngumu na garama).

Pia inch 6 zinafaa kujengea, tatizo n garama na n nzito kama nyumba n ndefu. Zinaongeza unene wa ukuta na uimara wa ukuta. Huwa yanatumiwa zaidi serikalini.
 
kantalambaz pia zipo tofali za inchi 4; mara nyingi kwa ajili ya kuta za vyoo vya ndani na makabati. Pia tofali za inchi 6 sio kwa ajli ya msingi tu; zinatumika pia kujengea kuta na wengine kwa ajili ya uimara zaidi hujenga kwa kuzilaza badala ya kuzisimamisha hasa kama paa linategemewa kuwa zito sana. Pia msingi ni lazima uwe umejengwa imara.
 
Habari ya asbuhi wana jukwaa na wadau wote.

Naomba tuelimishane kuhusu tofali za ujenzi za cement manake hua naona kuna tofali za urefu, upana na unene tofauti tunapokua tunajenga nyumba zetu ziwe ni za makazi, biashara au makazi na biashara:-

1.Kuna tofali za nchi sita hizi wajenzi wengi huzitimia kwenye kujengea msingi.
SWALI langu, je hizi tofali ni kwa ajili ya kujengea msingi tu pale unapokua unajenga nyumba?

2.kuna tofali za nchi tano hizi tofali hutumika sana kwenye ujenzi wa kuta za nje na ndani
SWALI langu,hizi tofali ni kwa ajili ya matumizi hayo na ni matumizi sahihi?

3.Inawezekana kujengea nyumba tofali za nchi tano peke yake?(kwa maana ya msingi, kuta za nje na ndani)
athari za kutumia hizo (tofali 5")ni zipi kigharama na kiubora katika ujenzi?

Karibuni wataalam mtupe hiyo elimu.
Ukitumia tofali za nchi 5 kujengea msingi, utatumia tofali nyingi kuliganisha na tofali za nchi 6. Mfano kama utaamua kutumia tofali za nchi 6 kujengea msingi wenye kina cha sentimita 75, utajenga course 5 wakati ukitumia tofali za nchi 5 itakubidi ujenge course 6.

Ukitumia tofali za nchi 6 kujengea msingi utaokoa kiasi fulani cha pesa, na hii ndiyo sababu ya watu wengi kupendelea kutumia tofali za nchi 6 kujengea msingi
 
Ukijengea msingi tofali za nchi 5 unatumia mota nyingi zaidi tofauti na kutumia tofali za nchi 6.

Sababu nyingine ni kuwa 6' inauwezo wa kubeba mzigo mzito zaidi ya 5' ndio maana huwa preffered kujengea foundation.

Kujengea boma 5' huwa preffered zaidi cz ni nyepesi zaidi ya 6'. Kujengea 6' kwa nyumba ya kawaida ni kuupa msingi mzigo usiokuwa na umuhimu. Unless unajenga ghorofa ambapo utaweka nguvu kubwa mno kwenye foundation.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom