Matibabu ya viongozi nje ya nchi - Aibu kwa Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matibabu ya viongozi nje ya nchi - Aibu kwa Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by cancerian, Mar 8, 2011.

 1. c

  cancerian Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu watanzania;

  Ni jambo linalonisikitisha sana kuona viongozi wa serikali wakienda kupata matibabu nje ya nchi. Naamini kiongozi yeyote anabidi aongoze kwa mfano sasa kama waziri wa afya Mh Mwandosya nae yupo India akipata matibabu, hivi kweli atakuwa ana dhamiria au hata kuziamini hospitali zetu na madaktari wetu wa hapa nyumbani?

  Mh Mwakyembe nae yupo safarini kwenda India kutibiwa ugonjwa wa ngozi, miezi kadhaa iliyopita Maalim Seif nae alikuwa India kupata matibabu.

  Jambo la ninalojiuliza ni je? wanaenda kwa gharama zao binafsi au za serikali? na kwanini hawaoni hata aibu kwa mtanzania ambaye anapata huduma za matibabu katika hospitali zisizo na hata panadol hapa nyumbani?

  Na kama kisingizio tunakosa wataalamu hapa nchini, kwanini wasiwaombe hao wenye hospital huko India kuwekeza kwenye mahospitali na kuleta vifaa na wataalamu wao hapa hapa nchini na kuepuka gharama za makazi na usafiri wanazoliingizia taifa?

  Ni aibu kubwa na sijawahi kusikia wananchi wakililalamikia suala hili na pia vyama vya upinzani kulipeleka bungeni.
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  TZ siasa imeharinu kila sekta. Afya, elimu, .................. Viongozi hawana utashi wa kisiasa na wala hawawapendi wananchi kwa sababu hawapati shida na hawaoni tatizo wananchi kuteseka.

  Piga hesabu shule za serikali, sijui za kata zina hali gani. Mtoto wa kiongozi gani anasoma huko?
  Hospitali zetu hazina wafanyakazi, elimu ya wanafanya kazi haiboreshwi, vitendea kazi na dawa hakuna. Haoni shida kwa sababu wamepitisha sheria/kanuni ya wao mabosi kutibiwa nje.

  Nafikiri siku watu wakiamka na kujua haki zao ndio suluhisho maana hata katiba mpya bila watu kiidai haiji na hawaiwezi kufuatwa.
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  tzjamani,

  Inasikitisha sana lakini utafanyaje hasa unapoona watu kule Mbeya wanampokea Bilali kwa furaha na kofia za CCM?

  Unafikiri somo la Maisha Magumu linafika kwao?

  Ona sasa wanavyohaha kwenda kwa Babu wa Monduli.

  Hata huko, bado viongozi wanakuja na kupitishwa kwa njia za mkato.

  Wenye nazo wengine wanakuja kwa Helcopiter.

  Kaazi kwelikweli.
   
 4. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  au wangejenga miundo mbinu mizuri ili kwa babu kufikike kirahisi na watu wengine pamoja na hao wakubwa wangepata dawa ya jero kwenye kikombe kimoja na kurudi home wakiwa freshi,kuliko kwenda mara india mara s.africa halafu wanalazwa kwa masiku mengi na hatimae wanakufa...
   
 5. m

  mob JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 511
  Trophy Points: 280
  fedha zipo ila tatizo ni utashi wa kisiasa na azma ya kutekeleza hakuna
   
 6. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  Pia na Mzee Malecela alienda UK. Naukumbuke pia ile kasumba ya kuwapeleka watoto wao nje japo tungejenga uwezo naamini kungelikuwa na baadhi ya shule nzuri hapa maana hata huko nje hakuna 'kikubwa sana' ukichukulia mantiki halisi ya elimu.

  Tunaweza kujifunza kwa wenzetu Kenya, Waziri Mkuu Odinga alifanyiwa operation (mwaka huu au jana) pale Nairobi Hospital na tukio la karibu kabisa ni la aliyekuwa mshindi wa tuzo ya Nobel Prof. wangari Mathai alikuwa na imani kubwa na madaktari wa nyumbani na ndio maana mauti yamemkuta Nairobi Hospital pia.

  List inaweza kuwa ndefu lakini kama ulivyosema, viongozi wakiwa mfano wanawapa moyo hata local doctors kuimprove kiwango chao.
   
 7. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hizo ndiyo faida za uongozi. Haiwezekani waziri akapata huduma sawa na mwananchi wa kawaida. Hivi vitu vipo hata kwa viongozi wa nchi nyingine.
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Nilimsikia JK kipindi cha kampeni akihojiwa kwenye mdahalo akisema tayari kuna ujenzi wa hospital kubwa na ya kisasa ambayo itakuwa inafaa kwa watu wote hivyo kuondoa tatizo la kwenda kutibiwa nje

  walio na taharifa za kina watujuze hospital hii ya kisasa imefikia wapi ama tuambiwe kama labda ilijengwa India badala ya hapa Tanzania
   
 9. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaheshimu mawazo yako, ila ninachopenda kukutaarifu ni kwamba, siku Mwigulu Nchemba atakapokushughulikia na wewe utapelekwa kutibiwa India, pesa si anazo.
   
 10. K

  Kiguu na njia Member

  #10
  Oct 10, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kidumu CCM!!
   
 11. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna siku waziri mkuu wa India atakuja kutibiwa huku kwetu? Waambie magamba waboreshe hospital zetu ziwe na hadhi kama wanazozifuata huko.
   
 12. peri

  peri JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hata nyerere alitibiwa nje mpaka mauti yange mkuta.
  Angeboresha hosipitali zetu wakati wa uongozi wake angeacha utamaduni wa viongozi kutokwenda nje.
  Haya ni matokeo ya madudu yaliyofanywa kwa miaka 50 tangu tupate uhuru.
   
 13. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  It is shame for our leaders! They know only few have access to travel to abroad suffering from the same disease but many Tanzanians die because they dont have money or their positions dont have those benefits. We have to change this trend for betterment of all Tanzanians.
   
 14. i

  issenye JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Pesa ambazo Serikali inazipoteza kwenye matamasha ya miaka 50 ya uhuru wa nchi ambayo haipo (Tanganyika) zingetosha kabisa kujenga hospitali kubwa na ya kisasa Africa ambayo ingekuwa ni kumbukumbu kwa vizazi vingi vijavyo tofauti na sasa ambapo baada ya tamasha kwisha wananchi wa eneo husika wanaakwa bila kitu isipokuwa uchafuzi wa mazingira na tabia
   
 15. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  India India India kuna nini India?

  Kila mwaka naona watu wanaoitwa Rotary Club au Dr Kanabha wakiwapeleka wagonjwa wa moyo India. Najiuliza hawa watu hawawezi kuwashawishi au kushirikiana nao kujenga hospitali za upasuaji wa moyo hapahapa tukapunguza gharama kubwa za kuwapeleka watu India.

  Zikishajengwa hospitali za kisasa hapa tukapata vifaa vinavyokidhi viwango inabaki kazi ya kuwafundisha vijana wetu wakati wanaendelea kujifunza tuwatumie madakitari bingwa toka nje nadhani tutakuwa tumeokoa fedha nyingi nakupata mapato toka kwa viongozi wa nchi zinazotuzunguka endapo kweli kama huduma zetu zitakuwa kwenye viwango.

  Nina mashaka na pelekapeleka za wagonjwa India inaweza ikawa deal ya watu fulani fulani.
   
 16. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,422
  Likes Received: 2,451
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha kuona viongozi wetu kwenda kutibiwa nje ya nchi, hakuna hata mmoja aliekomaa na kusema, atatibiwa hapa kwetu, na dawa zetu na madaktari wetu na hospitali zetu!
  Aibu mno kwetu, naona hata India na South Africa watakuwa wanaangua vicheko na jinsi serikali isvyoithamini Wizara ya Afya kwa kuisaidia kwa pesa na mali kuboresha huduma za afya.
  Aibu mno kwetu!
   
 17. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  Aliyekuwa awe mrithi wa kiti cha ufalme Saudi Arabia alifia hospitalini New York.
   
 18. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wako hili ndo linatupa uhalali wa kufanya hivyo..??
   
 19. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  wewe una mtazamo gani?
   
 20. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani swala siyo 'kiongozi' aseme atibiwe hapa hapa nchini hata kama kwa ulinganifu wenzetu kimatibabu wako juu sana.

  Swala la msingi nionavyo mimi ni mkakati wa dhati kabisa wa kuboresha huduma zitolewazyo kwenye taasisi zetu za tiba.

  Hilo nalo lina mchakato wa muda mfupi na mrefu. All in all we need a political will and readiness to face the situation
   
Loading...