Matibabu ya Kienyeji na Matumizi ya Miti Shamba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,337
Matumizi ya miti shamba na tiba za kienyeji yameongezeka sana. Kwa kawaida, watu hutumia tiba hizi kwa magonjwa ya kudumu ambayo dawa za kawaida zimeshindwa kutibu. Watu pia huzitumia kwa ajili ya kuboresha afya yao kwa jumla.
Tiba za kienyeji na miti shamba hutibu mwili mzima badala ya ugonjwa fulani au dalili za ugonjwa fulani. Wakati mwingine, zinatibu kuumwa na maumivu ambayo dawa za kuandikiwa na daktari haziwezi. Kwa mfano, kuumwa na kichwa, maumivu ya viungo na maumivu wakati wa hedhi.

Tahadhari – Kuchanganya dawa za kienyeji na dawa za kuandikiwa na daktari kunaweza leta athari usizotarajia. Kabla hujaanza kutumia tiba yoyote ya kienyeji, ongea na daktari.

Tiba za kienyeji na miti shamba zinazotumika sana ni zipi na zinatumikaje?

 • Mshubiri - Aloe - kuungua, vidonda vy amafua, ngozi iliyokauka, uchungu, kuchomeka na miale ya jua.
 • Arnica – kuchubukwa na kufura. Paka krimu ya Arnica au umeze vidonge vya Arnica ili kuzuia kufura au kuchibukwa.
 • Echinacea - mafua, maambukizi, kutibu vidonda
 • Mbegu za Flax– kuzuia saratani, gesi kwa tumbo, cholestroli ya juu mwilini, kukoma hedhi, ugonjwa wa mdomo na meno, shida za wakati wa hedhi
 • Garlic – kutibu na kuzuia saratani, ugonjwa wa moyo, shida za kutembea kwa damu, cholestroli ya juu, shinikizo la damu, maambukizo ya ngozi
 • Ginkgo Biloba – inasaidia kusafirishwa kwa damu, zuia kupoteza fahamu, kuumwa na kichwa, mfadhaiko
 • Ginseng – shinikizo la damu, ugonjwa wa sukari, mfadhaiko
 • Lavender – kuumwa na kichwa, mfadhaiko, kukatwa,kuchomeka, kuumwa na kudingwa na mdudu na kukosa usingizi. (si salama kwa mama wajawazito)
 • Melatonin - Alzheimer's, kutibu saratani, mfadhaiko, UKIMWI, kukosa usingizi
 • Rescue Remedy - mshtuko, wasiwasi or kukosa usingizi
 • St. John's Wort - mfadhaiko, uchovu, kukosa usingizi, uchungu, PMS, ponya vidonda
 • Mafuta au dawa ya kuchua yaTea-Tree – kuzuia kuvu na kuponya vodonda vya kuchomeka au kukatwa, chunusi, jipu na kuumwa na wadudu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom