matibabu bure

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
Hospitali Dar es Salaam
kuchunguza saratani
bila malipo Imeandikwa na Mwandishi
Wetu; Tarehe: 4th
December 2010 @ 22:45
Imesomwa na watu: 18;
Jumla ya maoni: 0 HOSPITALI ya Regency
kwa kushirikiana na
wataalamu wa saratani
kutoka India, kesho
(Jumatatu) wanaendesha
kambi ya bure ya uchunguzi wa maradhi ya
saratani. Kambi hiyo ya siku mbili
itaendeshwa katika
hospitali ya Regency jijini
Dar es Salaam na bingwa
wa maradhi ya saratani
kutoka India Dk Sridhar P S kutoka HCG group mji
wa Bangarole, India. Mwenyekiti wa hospitali
hiyo, Dk. Rajni Kanabar,
alisema jana kuwa
uchunguzi huo utafanywa
kwa kushirikiana na
wataalamu kutoka taasisi ya Health Care Global
Group
ya Bangalore. Dk. Kanabar alisema
taasisi hiyo ni kubwa
katika kutibu maradhi ya
saratani kusini na
mashariki mwa bara la
Asia. Alisema wagonjwa
watakaokutwa na
matatizo watapewa
ushauri wa kitaalamu kwa
saratani za mapafu,
mifupa, saratani ya tezi na ile ya damu. “Watakaokuwa na matatizo makubwa
watapelekwa taasisi ya
saratani ya Ocean Road,
lakini wenye matatizo
madogo madogo
watatibiwa hapa hapa Regency, uchunguzi huu
utakuwa na manufaa
makubwa kwa wagonjwa
wa saratani kwa kupata
ushauri wa kitaalamu kwa
mtaalamu bingwa kutoka India,” alisema Dk. Kanabar. “Wale watakaokuwa na matatizo makubwa sana
ambao hawataweza
kutibiwa hapa Tanzania
watapelekwa hospitali ya
HCG Group ya mji wa
Bangalore kwa gharama ndogo sana kama
tulivyokubaliana kati ya
Regency na wao, ” alisema. Alisema ushirikiano baina
ya hospitali hizo
unatarajia kufanikisha
kujengwa kwa kituo cha
aina yake cha utafiti wa
saratani jijini Dar es Salaam. Alisema chini ya
ushirikiano huo,
wataalamu wa saratani
kutoka Marekani, India na
Afrika Kusini watakuwa
wakija nchini kwa makubaliano maalum na
kutibu wagonjwa hapa
nchini kwa gharama
nafuu. Alisema utaratibu huo
utaiwezesha Tanzania
kuwa na uwezo wa kutibia
wagonjwa wa nchini hapa
ambao wana matatizo
makubwa ya saratani na kusaidia kuokoa fedha
nyingi za kigeni kwenda
kutibu wagonjwa nje ya
nchi.


Source:Habari Leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom