Mateso Yanayotokana Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB)

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
276
1,000
*FAHAMU KIDOGO KUHUSU LOAN BOARD NDUGU!*

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao. Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA, yaani watoto wa maskini.

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi (Watanzania wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano:

Daktari ambaye amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30. Basic salary yake ni 1.5 Mil.

Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo:

HESLB 225,000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension 80,000

Total deduction 642,510 TSH
Take home yake ni 857,590 TSH — ana watoto na anasomesha!

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil (225,000x12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil, atakuwa amepunguza deni lake hadi 27,300,000 TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27,300,000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000 + 1.8 Mil sawa na 29,100,000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambayo ni 1.8

Hivyo 26,400,000 + 1.8 Mil.
Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, ikiwa una pension ya 15 Mil, na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi, maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out, ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni, ni deni la maisha hasa waliosoma kozi za sayansi kama udaktari, Nesi, famasi, na injinia na wale waliosoma nje ya nchi. Hawa wote madeni yao si chini ya 25 Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

MAPENDEKEZO:

1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika wa hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu redioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato. Watanzania wengi hawajui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu iondolewe kwa sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli? Doh, tutapata laana katika nchi.

USHAURI:

1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho. Hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake. You need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akueleweshe, ni hatari sana. Fuatilieni haya mambo.

Pongezi kwa Mchambuzi!

Twitter *@fadhilikangusi*
 
Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,215
2,000

Duuh! Kumbe ni hatari kiasi hiki..?
 
impelle

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
806
1,000
Nilitumia mil13, nimeanza kulipa tangu 2015, mwezi wa nane nilienda bodi kuulizia deni lililobaki, nimejikuta nadaiwa mil 13.
Ni ujinga uliopindukia kwa hawa viongozi wetu kutofikiria hali zetu. Ni muda wa kufanya maamuzi muhimu, kama hali itaendelea hivi, nitaacha kazi (tanzania) na nitahama nchi kikazi.
 
Ludau

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
361
500
Magufuli katika ubora wake. Sio mikopo tu nenda kikokotoo, nenda nhif na mengine mengi. Bahati nzuri tunateseka wote ccm na wapinzani. Mrudisheni tenaaaa
 
RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
2,622
2,000
Yeah,
Kwakua CHADEMA ndio iliyoyaleta hayo.
Ndio mkuu, siunajua wabongo hawasikia wapo kama Kenge, wakivuja damu ndio wanaelewa wameumia. Sasa hawataki kuelewa ccm ndio inaleta haya, dawa nikuwambia waendelee kuichagua maana kwenye makato hawaangalii kadi ya chama.
 
Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
1,693
2,000
Magufuli katika ubora wake. Sio mikopo tu nenda kikokotoo, nenda nhif na mengine mengi. Bahati nzuri tunateseka wote ccm na wapinzani. Mrudisheni tenaaaa
Hatuteseki wote boss, fikiria wao pengine wamekaa mjengoni awamu tano mfululizo, kila awamu anapewa kiinua mgongo ya si chini ya milioni 282. Mwanaye asomee mkopo ili iweje? Na ashindwe vipi kulipa hilo deni kwa mkupuo mmoja kuepuka hiyo 6% interest aliyoipitisha bungeni ikiwa huyo mtoto amesoma kwa mkopo.

Wanajua wanachofanya na wamelenga hasa kukusanya kutoka kwetu ili walipane viinua mgongo visivyofanana na uhalisia. Na kw hili, hakuna uvyama, woooote mjengoni mule ni wamoja, sio hao wanaojiita wapinzani au watawala.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,225
2,000
*FAHAMU KIDOGO KUHUSU LOAN BOARD NDUGU!*

Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao. Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA, yaani watoto wa maskini.

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi (Watanzania wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano:

Daktari ambaye amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30. Basic salary yake ni 1.5 Mil.

Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo:

HESLB 225,000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension 80,000

Total deduction 642,510 TSH
Take home yake ni 857,590 TSH — ana watoto na anasomesha!

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil (225,000x12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil, atakuwa amepunguza deni lake hadi 27,300,000 TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27,300,000 TSH.

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000 + 1.8 Mil sawa na 29,100,000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambayo ni 1.8

Hivyo 26,400,000 + 1.8 Mil.
Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on.

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa.

Yaani, ikiwa una pension ya 15 Mil, na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria.

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi, maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out, ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu.

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni, ni deni la maisha hasa waliosoma kozi za sayansi kama udaktari, Nesi, famasi, na injinia na wale waliosoma nje ya nchi. Hawa wote madeni yao si chini ya 25 Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair.

MAPENDEKEZO:

1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno.

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika wa hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu redioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato. Watanzania wengi hawajui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu iondolewe kwa sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli? Doh, tutapata laana katika nchi.

USHAURI:

1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho. Hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil.

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake. You need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akueleweshe, ni hatari sana. Fuatilieni haya mambo.

Pongezi kwa Mchambuzi!

Twitter *@fadhilikangusi*
Kuna vitu viwili sijavielewa kwako, pengine nilikua naelewa tofauti na wewe.

1) Kadiri mlipaji anavyozidi kulipa rejesho, hiyo 6% itakatwa kwenye ile ile 30mil aliokopa awali (wizi) au itakatwa kwenye Salio lililobaki baada ya kutoa rejesho la mwaka husika?

2) Ukianza tu kulipa nafahamu kua 6% retention fees (wizi) inakufa hapo hapo, mbona kwako ni kama tu iko kila mwaka hata kwa yule anaerudisha mkopo?
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,225
2,000
Ndio mkuu, siunajua wabongo hawasikia wapo kama Kenge, wakivuja damu ndio wanaelewa wameumia. Sasa hawataki kuelewa ccm ndio inaleta haya, dawa nikuwambia waendelee kuichagua maana kwenye makato hawaangalii kadi ya chama.
Hawa ndio waliowaimbia Wapinzani kua Wataisoma Number. Wakidhani kua sheria kandamizi kama hizi huwaathiri Wapinzani tu. Au ugumu wa life ya kitaa utawapata tu Wapinzani.
 
RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
2,622
2,000
Hawa ndio waliowaimbia Wapinzani kua Wataisoma Number. Wakidhani kua sheria kandamizi kama hizi huwaathiri Wapinzani tu. Au ugumu wa life ya kitaa utawapata tu Wapinzani.
Unakuta mtu analalamika makato ya HESLB nimakubwa lakini huyohuyo anamshangilia Magufuli na anataka apigie kura ccm. Bora hali iwe ngumu mpaka wajitambue.
 
Ludau

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
361
500
Ila magufuli ajitathmini sana. Hata kama atarudi ikulu October hii, 2025 atatoka kwa aibu sana. Mema aliyofanya ni kidogo kuliko ubaya. Tuombe uzima.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,225
2,000
Unakuta mtu analalamika makato ya HESLB nimakubwa lakini huyohuyo anamshangilia Magufuli na anataka apigie kura ccm. Bora hali iwe ngumu mpaka wajitambue.
Ha ha ha,
Hii inatokana na kuwaachia wengine wafikirie kwa niaba yetu, hatutumii akili zetu tulizozaliwa nazo.

Ndo maana anaweza akaja Mgombea akatuambia kua Bei ya Umeme ni kubwa Sana kuliko hata USA, akichaguliwa atahakikisha inashuka. Wakati mgombea huyo ndio anaeshikilia hicho anachogombea kwa miaka mitano Sasa.
 
Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,381
2,000
Madaktari wana nafuu kwa kuwa ada walilipiwa na serikali.. Walichokopeshwa ni meals n accommodation.. Wengine na sie kama ma engineer nk hali ni tete!
 
Emmathias

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
432
500
Naamini asilimia kubwa ya graduates hatuijui hii sheria kandamizi, kumbe inaumiza kias hiki?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom