Mateso ya wanyama wa Vingunguti

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
7,718
7,434
Juzi kwenye tv wakati sakata la machinjio ya Vingunguti linaelezwa niliona ng'ombe mmoja ameshindwa kusimama kwa njaa kwani ulikuwa unamwona amekonda kabisa. Nina imani na wanyama wengine huwa wanatendewa vile vile.

Kwa kweli huu ni ukatili usiopimika kuwacha wanyama na njaa kwa vile watachinjwa. Mimi nilijisikia vibaya sana sana kumwona ng'ombe yule ameshindwa hata kusimama kwa njaa.

Jee nyinyi munaotetea haki za wanyama munaona hii ni sawa? Tufanyeje ili kuzuia ukatili huu dhidi ya wanyama wasio na hatia? Ninaogopa na sisi tutapigwa laana kwa mateso haya tunayowapa wanyama.
 
Ni vibaya kuwaaumiza wanyama kwa njia yeyoye...
...but who said they feel what we feel?

Hi..si kusema tuumize wanyama!!
 
Juzi kwenye tv wakati sakata la machinjio ya Vingunguti linaelezwa niliona ng'ombe mmoja ameshindwa kusimama kwa njaa kwani ulikuwa unamwona amekonda kabisa. Nina imani na wanyama wengine huwa wanatendewa vile vile.

Kwa kweli huu ni ukatili usiopimika kuwacha wanyama na njaa kwa vile watachinjwa. Mimi nilijisikia vibaya sana sana kumwona ng'ombe yule ameshindwa hata kusimama kwa njaa.

Jee nyinyi munaotetea haki za wanyama munaona hii ni sawa? Tufanyeje ili kuzuia ukatili huu dhidi ya wanyama wasio na hatia? Ninaogopa na sisi tutapigwa laana kwa mateso haya tunayowapa wanyama.

mnada wa pugu ufungwe kwa kuwa hauna maji kwa ajiri ya wanyama wanaoletwa kuuzwa.
 
Its true na wengi wakifika pale nasikia wanakuwa wameshakufa ila wanapitishwa mlango wa nyuma. Really bad! Inaumiza sana kuona wanyama wakiteseka.Na Wakati wa kushushwa kwenye gari mmoja akikosea akaruka vibaya akashindwa kunyanyuka, basi wengine wote wanaofuata wanakuja juu yake na kinachofuata anashindwa kabisa kunyanyuka! It pains kwa kweli sipendi kuona wanyama wakiteseka especially domestic animals.
 
Back
Top Bottom