Mateso ya wafanyakazi wapya wa t m a | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mateso ya wafanyakazi wapya wa t m a

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by eddymyinga, Feb 23, 2012.

 1. e

  eddymyinga Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa sisi ni wazalendo wa kweli na nchi yetu lakini sasa tunavunjwa nguvu na baadhi ya watendaji wa hidala husika , kweli tuna uchungu sana pesa za serikari zilizotumika kuwasomesha wasomi huko kigoma na tunawapa hajila pasipo kuwaekea mazingira bora tulio waajiri , sasa mtu anaajiriwa na kupangiwa kituo cha kazi bukoba au maswa , ametoka dar es salaam , hadi sasa hamjawapa ela ya kuanzia maisha , hii lakini ni uonevu maana mtu huyu atafikia kwanani na aishi vipi ?

  Mm napenda kumshukuru sana mama kijazi ila anaharibiwa na watendaji wake, mm naomba muwasaidie vijana wenu maana madada (wasichana) msipo wapa ela mnatarajia nini kama hawana ela , mtasababisha tabia mbovu , ili kusukuma maisha, vijana wameajiriwa tar 1/2/2012 hadi leo wanaombaomba mtaani misaada maana hawana ela kabisa.

  Wengine wamefukuzwa kwenye nyumba walizofikia , inauma sana , jamani serikari iliangalie sana hili wengine wamekosa hata nauli ya kwenda kazini , wakiacha kazi na kutafuta kwingine hasa kwenye kampuni binafsi serikari itakua imeingia hasara kubwa kuwasomesha na kupoteza nguvu kazi yake yakulitumikia taifa katika secta za serikari na kuzinufaisha secta binafsi ambazo hazina mcahango wa mojakwamoja kwenye jamii au serikari yetu.

  Ndugu watanzania kila mtu asimame kwenye nafasi yake kama mnyanyua uchumi wa nchi yetu kwa kutenda kile kilicho muweka sehemu husika na si kwa maslahi binafsi na kunyanyasa na kutesa wengine wasio na hatia ni mimi mwana jamii wa kitanzania god bless tanzania - amen
   
 2. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  You mean, Tanzania Meteorological Agency?

  Nchi inakwenda kama gari lisilo na dereva, mambo yako shaghalabaghala, kila mtu ndani ya serikali ni kama vile Rais, hakuna wa kumkosoa mwingine, kwaujumla ile Chain of Command imekatika mahali fulani!!!

  Fedha ya kujikimu kuwalipa watumishi wa Umma hakuna, mishahara inakopwa NSSF, ila fedha ya kwenda kuwahonga wapiga kura kwenye chaguzi ndogo ipo. Hapa kosa ni letu sisi watz wenyewe viongozi na watawala hawahusiki!!!

  Subiri uone fedha zetu walipakodi zitakavyotumika ARUMERU.
   
Loading...