Mateso ya Absalom Kibanda yasitutishe, yatutie nguvu za kupambana kwa umakini zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mateso ya Absalom Kibanda yasitutishe, yatutie nguvu za kupambana kwa umakini zaidi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by akilimtindi, Mar 8, 2013.

 1. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu zanguni Wana-JF, nawapeni pole sana kwa majanga yanayowaandama wapenda haki wa nchi hii na wale wote wanaofanya bidii kuuweka uovu wa nchi hii wazi mbele ya wale wasiojua kinachoendelea.

  Binafsi napenda kutoa pole kwa familia ya Kibanda pamoja na familia za wengine wote waliowahi kuumizwa kwa namna moja au nyingine kwenye mfululizo huu wa matukio yenye utata, nalazimika kutoa pole kwa ujumla maana hiki ni kidonda kipya kabla vidonda vingi vya siku kadhaa zilizopita havijapona hata kidogo.

  Niombe radhi kwa wanajukwaa maana nimepotea kwa muda hapa jukwaani, lengo langu la kwanza kuandika haya ya leo ni kujaribu kueleza na kusisitiza tena kwamba ukombozi sio lelemama na ni ukweli usiopingika kwamba hii keki ya Taifa hili iko mikononi mwa watu fulani, ambao tulishawaachia nafasi walikaujua utamu wake kwa muda mrefu.

  Sio kazi rahisi hata kidogo kwa kuona keki hiyo inawaponyoka na kwenda kusikojulikana ama kwa maneno mengine kwenda wasikoweza kuifikia na kuitafuna kwa jinsi wanavyoweza wao na kwa wakati wanaotaka wao.

  Hata hivyo ikiwa sio kazi rahisi wao kuona keki hiyo inawaponyoka, kwa uelewa wangu ni kazi rahisi sana sisi kuichukua keki hiyo na kuirudisha mikononi mwetu kama tutafanya uamuzi...naamini sio wakati sahihi sana kuliongelea hili kwa sasa maana naona kama vile kuna namna Wadanganyika wamechanganyikiwa.

  Cha msingi hatutakiwi kulegea, tunapaswa kuangalia mbele na kuendeleza vita hii hadi tutakapofanikiwa kuirudisha keki hii mikononi mwetu sisi wanyonge.

  Lengo langu la pili ambalo nadhani ndilo la muhimu zaidi kwa leo ni kuwapa tahadhari wale walio mstari wa mbele kwenye uwanja wetu wa mapambano kukaa mkao makini zaidi, namaanisha wazi kwamba hii ni vita isiyo rasmi lakini yenye kutafuna taratibu.

  Tusichukulie matukio kama haya ni mzaha na kuendelea kukaa ki-milegezo, ni muhimu sana tena sana wapambanaji kujifunza mbinu muhimu za mapambano maana hawatafundishwa na yeyote wala haitatokea siku wakaambiwa rasmi wajifunze hayo.

  Hakuna jambo la kushangaza, Mungu yu-pamoja nanyi lakini alisisitiza pia kwenye kutumia akili zenu. Simaanishi waliomvamia Kibanda walifanikiwa kwasababu Kibanda kalegea, hapana...namaanisha kuna umuhimu sasa wa kukaa mkao wa kujilinda zaidi ya Kibanda alivyojaribu kujilinda.

  Mimi ni Mkristo kwahiyo naomba ninukuu Bibilia, tafakarini mstari usemao "...Jifunzeni kukaa na wana wa giza, iweni na akili kama wana wa giza".

  Kama nimekosea wenye kuijua kuliko mimi wanisahihishe, naomba kwa leo niishie hapa na walioko mstari wa mbele wanaoelewa watayafanyia kazi vinginevyo kuna hatari ya kuukimbia uwanja wa mapambano.

  Ukihitaji kuendelea na mapambano, moja ya mambo muhimu ni kuangalia kwa upya mbinu zako za mapambano ukilinganisha na mbinu za adui yako pia.
   
 2. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Mpaka mje mgundue kuwa Serikali haihusiki mtakuwa mmeumia sana. Maadui zenu sasa wanachekelea tu wanapoona akili zenu zimeegemea kuishambulia serikali ambayo haihusiki.
   
 3. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa mchango wako, naomba nitenganishie yapi serikali inahusika na yapi serikali haihusiki kati ya matukio kadhaa yenye utata siku za karibuni. Naomba nitangulize jibu kwamba ukiniambia serikali haihusiki popote sitakuwa na haja ya kuendelea kujadiliana na wewe.
   
 4. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hivi wewe jamaa ni lazima kila uzi uujibu?haya tuweke wazi hayo matukio yanayotuhumiwa kwa serikali yako kuifanya.
   
 5. A

  Atongwele JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 2,471
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  mh huo ndio ubaya wa waandishi kutumuwa kisiasa. mpaka watakapokuja jua kuwa viongozi wa CHADEMA ndio wanawateketeza watakuwa wameumizwa sana. cha muhimu waandishi wazingatie maadili ya kazi yao. wajifunze kule somalia jinsi waandishi wanavyouawa na non state actors hususan waandishi wanaoandika taarifa zinazowaudhi wapinzani
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2013
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,203
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  mmekuwa wepesi sana kunyooshea kidole serikali , kisa neno afande lilisikika ...:nono:
   
 7. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mmekamia sana kwamba CHADEMA wanahusika na sio Serikali, nimeuliza swali rahisi na nashangaa niliyemwuliza kakimbia moja kwa moja ama karudi kwa ID nyingine. Inawezekana kweli Serikali haihusiki kwenye hili, je ni wapi katika haya matukio tata Serikali inahusika? Hata sisi tungependa tuilaumu Serikali kwa lile ililolifanya kuliko kutupa lawama hovyo, naomba majibu kama una hoja.
   
 8. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi Mkuu ukisikia mlio wa Mbuzi nje ya nyumba yako kisha ukatoka na kukuta mahindi yako yameliwa utamkimbiza Mbuzi au utamwacha na kuanza kumsaka aliyekula mahindi? Naomba jibu...
   
 9. m

  mwakibete JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2013
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,626
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280


  inaelekea unamjua anayehusika?? Weka mambo hadharan kulisaidia jesh la polis mkuu
   
 10. m

  mwakibete JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2013
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,626
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280


  CHADEMA??? Kuna haja ya kutumia majina halisi humu ndan ili watu kama wewe muitwe kuisaidia polisi.
   
 11. m

  mwakibete JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2013
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,626
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280


  tumnyoshee nani na yeye ndo muhusika mkuu wa kulinda usalama wa raia wake?? Ni lipi kati ya yote iliyonyooshewa ilinawa mikono kwa kumuonyesha muhusika wa tukio? Yu wapi Ighondu?

  Acha unazi kwenye ishu zinazohitaji majibu mazito. Huna cha kuchangia kaa kimya.
   
 12. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2013
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,203
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280

  nikikwambia ni wafuasi wa chadema je ndio walofanya huo unyama ili kuchafua serikali , maana CDM wanaitana MAKAMANDA
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2013
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,203
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280

  wewe kweli akili mtindi ,, cdm pia wanajiita makamanda
   
 14. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2013
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lazima upindishe mambo majibu yanapokosekana, huna hoja na siwezi kubishana na wewe.
   
 15. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2013
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Chadema ni Makamanda hata kama hamtopenda waitwe hivyo itabaki kuwa hivyo, matokeo mnayaona wenyewe..!
   
Loading...