Mateso makubwa wanayopata Wastaafu katika mchakato wa uhakiki Arusha Mjini

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,227
1. Ugawaji wa number kwa ajili ya foleni haupo sytematic kabisa, wapo wanaolekezwa kwenda kuchukua number manispaa na kurudi tena Ofiisi za mkuu wa mkoa, wapo wanaopewa number direct kwa mkuu wa mkoa. Wapo wapatiwa number toka Jumatatu siku ya kwanza ya mchakato hadi leo hawajamaliza na wapo wanaokuja leo leo wanamaliza mchakato. {Waliogaiwa number Jumatatu leo wameambiwa number hizo hazipo wanaanza upya}.

2. Mechanism ya Jengo mahala mchakato unafanyika ni gorophani {Kumbuka hawa ni wazee na wengine ni wagonjwa kabisa}.

3. Mrundikano wa watu ni mkubwa {Magomjwa ni hatari kusambaa}.

4. Wazee hawa wanatoka Mbali kwa ni Willaya nne zote zimeonganishwa sehemu moja na wote wanafanyiwa uhakiki sehemu moja (ofisi za mkuu mkoa mjini).

5. Walitoa maelezo kwamba wale ambao majina ya vitambulisho vyao havifanani basi waende kula kiapo kwa mwanasheria. Wazee hawa wameenda kula kiopo kwa gharama na baadae waafisa wamesema viapo vya wanasheria havitakiwi bali kiapo cha mahakama ndicho kinachotakiwa.

6. Muda wa mchakato ni mchache sana, kutoka Jumatatu hadi leo Ijumaa ndio mwisho.

Wazee hawa wanapata tabu sana hapa.
 
Watu wanateswa utafikiri kustaafu ni suala la Ghafla.

Anyway, hawa wazee ndio huwaambi kitu kuhusu CCM. Na hayo ndio matunda yenyewe.
 
Mimi nipo DSM, naomba kwa anayejua

Uhakiki wa DSM unafanyika lini na ni wapi wapi unafanyika, atusaidie taarifa tafadhali.
 
Back
Top Bottom