Mateso makubwa waliyoyapata watuhumiwa wa Ugaidi walioshitakiwa pamoja na Mbowe yanatisha, Inashangaza wamewezaje kuwa hai hadi sasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,644
218,096
Baadhi ya Picha za makovu ya watuhumiwa wa Ugaidi wanaoshitakiwa pamoja na Mbowe zimeanza kuonekana hadharani, hawa watu waliteswa kinyama! Hii nchi haikuwahi kufikia unyama kama huu , tena kwa tuhuma za uzushi zilizojaa uongo mtupu! kisa ni Kumkomoa Mbowe, Inasikitisha sana!

Tunaomba radhi kwamba hatutaweza kuwaonyesha picha za majeraha yote, kutokana na Maadili ya Kitanzania kwa vile majeraha mengine yako maeneo yasiyoruhusiwa kuwekwa hadharani, bali itoshe tu kusema kwamba KILA ALIYEHUSIKA NA UNYAMA HUU AWE HAI AU AMEKUFA ATALIPA .

Wakili_Peter_Kibatala_Je__inaruhusiwa_Kumchoma_choma_Mtuhumiwa_na_Bisibisi_na_Kumwambia_tutaku...jpg
 
Picha za makovu ya watuhumiwa au picha ya makovu ya mtuhumiwa? Afu picha hii umeileta leo baada ya mawakili wenu kuulizwa sababu ya kumpa Mbowe maji peke yake kila siku, huku mkiwatelekeza wenzake aliokamatwa nao. Unafiki ni kitu kibaya sana hapa dunia na ndio maana Mungu anaamua kushusha viboko vyake kwa njia hii tunayoiona mahakamani.
 
Mkuu una akili timamu? Ni bora nijiridhishe kuhusu akili yako kwanza kabla sijakushushia nyundo
 
Picha za makovu ya watuhumiwa au picha ya makovu ya mtuhumiwa? Afu picha hii umeileta leo baada ya mawakili wenu kuulizwa sababu ya kumpa Mbowe maji peke yake kila siku, huku mkiwatelekeza wenzake aliokamatwa nao. Unafiki ni kitu kibaya sana hapa dunia na ndio maana Mungu anaamua kushusha viboko vyake kwa njia hii tunayoiona mahakamani.
Hahahaaa wacha wanyooooshwe tu Mbowe lazima ale miaka
 
Hivi sheria zingefuatwa unadhani tungeandika haya ? hivi mateso ya kinyama namna hii ili kutengeneza uongo maana yake nini ?
Hakuna kitu kama hicho, weka mezani ushahidi wa hayo mateso, unataka kutueleza hapa wote wenye makovu wameteswa na polisi? kwa nature ya ilokuwa kazi yao wanakisa vipi makovu?
 
Back
Top Bottom