Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 3,929
- 3,023
Aliyefungwa miaka 11 aeleza adha za gerezani
2008-06-04 09:17:22
Na Restuta James
Kijana yatima aliyekaa gerezani kwa miaka 11, Gregory Adrian, ameibuka na kusimulia mateso ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayotokea jela yakiwemo ya ulawiti na utumiaji wa mihadarati.
Amesema mengine hayafai kusimuliwa hadharani na kuwaomba viongozi wa serikali na wabunge, kwenda huko wakashuhudie.
Gregory ambaye alikuwa karani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, alidai kuwa, alifungwa kwa kubambikiwa kesi ya kuomba rushwa na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu baada ya kutokea mtafaruku baina yake na wafanyabiashara wa ng`ombe.
Anaeleza kuwa, mbali ya ulawiti na ukiukwaji wa haki za binadamu, wafungwa wamekuwa wakipewa adhabu nzito na zisizostahili kwa mtu yeyote duniani.
Bw. Gregory ambaye alikuwa akihamishiwa katika magereza mbalimbali, alifungwa mwaka 1996 katika gereza la Kahama akiwa na namba 116/1996, Kilimo Malya namba 193/1996, Butimba namba 497/1997, Ukerewe 215/1998, Isanga 958/1999 na kumaliza kifungo mwaka jana katika gereza la Ukonga, jijini Dar es Salaam akiwa na namba 948/2002.
Alisema mara nyingi Mawaziri na Kamati za Bunge wanapofanya ziara magerezani, wamekuwa wakipewa taarifa `zilizopikwa` na hivyo kushindwa kubaini mateso yanayowakabili wafungwa.
Aidha, alisema viongozi hao wameshindwa pia kubaini ukweli kutokana na muda mdogo wanaoutumia katika ziara ambazo zinakuwa za kupangwa.
``Wangepaswa kufanya ziara kwa kushtukiza ili wafungwa wengi waweze kuzungumza badala ya kutoa taarifa ya siku wanayokuja jambo linalowafanya maofisa kuwapangia wafungwa cha kuzungumza,`` alisema.
``Unyanyasaji wa kijinsia ni mkubwa sana gerezani mfano, unaenda kufanyakazi kwa kamishna wa gereza unaporudi maofisa wanakulazimisha kujisaidia haja kubwa mbele ya wenzako ili ukaguliwe usije ukawa umemeza kitu,`` alisema.
Alifafanua kuwa vitendo vya ulawiti na matumizi ya mihadarati ni mkubwa na kwamba maofisa wa magereza wameshindwa kudhibiti hali hiyo.
``Hadi namaliza kifungo nilihamishwa katika magereza nane na hali zinafanana. Vitendo vya mauaji, chakula kidogo na adhabu zilizokinyume na haki za binadamu zinazotolewa na maofisa magereza ni hali ya kawaida kabisa kana kwamba magereza ni mamlaka ya watu binafsi,`` alisema.
Aliongeza kuwa wafungwa wamekuwa wakiuawa kwa sumu na maofisa wa magereza wanapojaribu kulalamikia mateso wanayopewa.
``Nilidhani gerezani ni sehemu ya kumrekebisha mkosefu lakini nimekuta kwamba ni sehemu ya kudhalilishwa na kuteswa pasipomfano,`` alisema.
``Nimefungua mashtaka dhidi ya askari magereza yenye kumbukumbu namba HBUB/S/277/07/08/Magereza/2.iv ambayo imekuwa ikipigwa \'danadana\' kwa miezi saba sasa, naomba serikali na Bunge zichunguze tuhuma hizi ili wafungwa watendewe haki maana wengine wameingia gerezani kwa hila,`` alisema.
SOURCE: Nipashe
http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/06/04/115760.html
Waziri unayehusika usitake kuletewa repoti toka maofisa wa Magereza, umesikia hapo? Acheni kukaa maofisini fumanieni mambo haya kwanini watu wateseke nanyi mkipiga bla bla maofisini?