Mateso kwa wanaume toka kwa wake zao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mateso kwa wanaume toka kwa wake zao

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Edo, Dec 30, 2009.

 1. E

  Edo JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kuna siku nilihudhuria harusi moja hapo Mayfair Plaza. Sheikh mfungisha ndoa akapewa nafasi atoe mawaidha japo kwa ufupi kwa wanandoa wale.
  Yule sheikh akatoa mfano mmoja wa jinsi ambavyo ndoa zote zina matatizo na ni muhimu kuvumiliana. Akasema:-
  Kuna siku alikuwa msikitini akisikiliza mawaidha hayohayo ya mambo ya ndoa. Mtoa mawaidha akauliza wanaume. Wangapi humu ndani wamewahi kupigwa na wake zao? Kama wapo waje wasimame juu wasogee mbele. Kwa muda wengi wakasita, lakini baada ya muda mfupi wote wakasimama wakaenda mbele . Akabaki bwana mmoja ameketi. Wale wanaume kumwona jama kaketi, wakamsifu sana kwamba yeye kapata mke mwema na mtoa mawaidha akasema hebu mwenzetu atujulishe nini siri ya mafanikio yake.

  Yule bwana kwanza akasikitika sana akasema jamani mimi sina unafuu wowote kwa huyo mke wangu, ni kwamba kipigo alichonipa ndio kinanifanya hata kusimama siwezi !!!

  Tuliishia kucheka, na hotuba ikaishia hapo
   
 2. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mambo kama haya ni ya kuweka kwenye jukwaa ka la jokes/utani kwani ni uongo wa waziwazi wenye lengo la kufurhisha watu.

  ukweli ni asilimia ndogo sana yawanaume wenye ujasiri wa kusimama hadharani na kukiri kupigwa na wake zao.

  wahusika, hamisheni utani huu hapa
   
Loading...