Matendo ya Sabaya: Ukweli ni kwamba tulipaswa kupata Serikali Mpya ila tatizo Katiba haisemi hivyo

mimi nilikuwa mwanachadema mara tu chama kilipo anzishwa mwaka 1992 na marehemu Bobu makani, ofisi zake kipindi hiko zikiwa mitaa ya kisutu.
Mbowe kakiharibu sana chama.
Kama kweli chadema tunataka kuimarika na kusonga mbele tunahitaji mabadiliko ya uongozi.
 
Maneno ya Sabaya kuwa alikuwa anatekeleza maagizo toka Juu ni mazito sana. Kwa kifupi ni kwamba Serikali ndiyo inayowatuma watendaji wake kuwaumiza/ kuwapora mali na fedha raia wake badala ya kuwatetea/kuwalinda dhidi ya maovu.

Sabaya katoa ushahidi mzuri sana kwa wananchi dhidi ya Serikali yao pamoja na Viongozi wakuu wa Serikali. Aibu kubwa Sana. Je maagizo hayo yaliishia Kwa Sabaya na Bosi wake wa wakati huo tu au hadi hivi sasa bado yanatolewa???
 
Ni kama kawatolewa kafara tu ila ukweli ni wengi tu walipaswa kuwajibika.
 
Je, Mama,Waziri Mkuu, IGP na Mkuu wa TISSS pamoja na waliowahi kuwa mawaziri wa mambo ya ndani bila kusahau RPC wa Kilimanjaro,OCD na wengineo hawakujua yaliyokuwa yanafanywa na Sabaya?
ulikosea hapo ☝️ nkajiuliza unajuaje kama baadhi hawakutimiza wajibu wao

ila hapa👇 ukaweka mambo sawa AHSANTE

Labda Mkuu wa TISS na wasaidizi wake wanaweza kuwa na la kujitetea iwapo walitimiza wajibu wao ila hawa watendaji wengine ama walipaswa kujiuzulu kupinga matendo ya Sabaya au kuchukua hatua.
 
ulikosea hapo ☝️ nkajiuliza unajuaje kama baadhi hawakutimiza wajibu wao

ila hapa👇 ukaweka mambo sawa AHSANTE
Inawezekana wewe ni member wa TISS na kuna unayoyajua kuhusiana na hii issue.
 
Mandela alipokaa jela miaka 27 aliharibiwa nini?
Akili zako hazina akili.
Mandela hajawahi kukata watu masikio, Wala Mandela hajawahi kupigilia watu misumari. Mandela akutumia namba feki za UN kuvamia wafanya biashara na kufanya unyang’anyi.
Mandela hakuwahi kubaka watoto wa kike kama Sabaya..
Muwe na adabu mnapoingia jukwaa hili , sio FB hapa.
 
Ukifikiri kwa makini, wote waliokuwa mabosi wa Sabaya chini ya Magufuli na wakuu wote wa vgombo vya ulinzi na usalama hawakupaswa kuendelea kuwa madarakani leo hii ila katiba ndio tatizo kwani haitoa hata fursa ya kufanya uchaguzi tupate viongozi wengine ambao bila shaka wangekuja na watendaji tofauti na hawa tulionayo leo hii.

Je, Mama,Waziri Mkuu, IGP na Mkuu wa TISSS pamoja na waliowahi kuwa mawaziri wa mambo ya ndani bila kusahau RPC wa Kilimanjaro,OCD na wengineo hawakujua yaliyokuwa yanafanywa na Sabaya?

Kama walijua na wakaendelea kubaki serikalini, leo hii wanastahili kuwa madarakani au baadhi yao wanastahili wawajibike kwa makosa ya Sabaya aliokuwa chini yao?

Labda Mkuu wa TISS na wasaidizi wake wanaweza kuwa na la kujitetea iwapo walitimiza wajibu wao ila hawa watendaji wengine ama walipaswa kujiuzulu kupinga matendo ya Sabaya au kuchukua hatua.

Kama watu wakitaka tu kuandamana serikali kupitia Jeshi la Polisi wanachukua hatua. Vipi kwa Sabaya kutenda yote haya na serikali ilikuwepo? Intelijensia ya Polisi inayotambua hatari ya maandamano ya wapinzani ilikuwa wapi kubaini matendo haya ya Sabaya?

Nawaza tu tutasikia mambo gani ikitokea kesi ya waliotaka kumua Lissu kwa risasi inatinga mahakamani kama tumesikia haya kwa Sabaya aliedai kutekeleza maagizo kutoka juu?
Inasikitisha sana..
Bado yanaguswa matawi.
Shina na mizizi bado kabisa..

Back
Top Bottom