Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,991
- 144,327
Ukifikiri kwa makini, wote waliokuwa mabosi wa Sabaya chini ya Magufuli na wakuu wote wa vgombo vya ulinzi na usalama hawakupaswa kuendelea kuwa madarakani leo hii ila katiba ndio tatizo kwani haitoa hata fursa ya kufanya uchaguzi tupate viongozi wengine ambao bila shaka wangekuja na watendaji tofauti na hawa tulionao leo hii.
Je, Mama, Waziri Mkuu, IGP na Mkuu wa TISSS pamoja na waliowahi kuwa mawaziri wa mambo ya ndani bila kusahau RPC wa Kilimanjaro,OCD na wengineo hawakujua yaliyokuwa yanafanywa na Sabaya?
Kama walijua na wakaendelea kubaki Serikalini, leo hii wanastahili kuwa madarakani au baadhi yao wanastahili wawajibike kwa makosa ya Sabaya aliokuwa chini yao?
Labda Mkuu wa TISS na wasaidizi wake wanaweza kuwa na la kujitetea iwapo walitimiza wajibu wao ila hawa watendaji wengine ama walipaswa kujiuzulu kupinga matendo ya Sabaya au kuchukua hatua.
Kama watu wakitaka tu kuandamana serikali kupitia Jeshi la Polisi wanachukua hatua. Vipi kwa Sabaya kutenda yote haya na serikali ilikuwepo? Intelijensia ya Polisi inayotambua hatari ya maandamano ya wapinzani ilikuwa wapi kubaini matendo haya ya Sabaya?
Nawaza tu tutasikia mambo gani ikitokea kesi ya waliotaka kumua Lissu kwa risasi inatinga mahakamani kama tumesikia haya kwa Sabaya aliedai kutekeleza maagizo kutoka juu?