Matendo ya huruma: Ulishawahi kwenda kumuona mgonjwa halafu akakuuliza amekwambia nani naumwa?

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
3,438
2,000
"Amewaambia nani naumwa?" nimekumbuka haya maneno tuliambiwa na jirani yetu mgonjwa baada ya kusikia anaumwa tukasema ngoja tukamuone ila kilichotukuta mpaka huwa nawaza Mara mbili mbili namna ya kwenda kumuona mgonjwa.

Jamii yetu bado haielewi kama suala LA kuumwa linabaki kuwa la familia au public?

Ndio maana wengine yanatukuta kama hayo.

Au unaenda kumuona mgonjwa unaambiwa amelala ni Mara tu baada ya kutusikia

Mwingine baada kuondoka tukaja kusikia eti tulienda kumuona kama amekonda au la!

Ukienda kumuona unaambiwa "mbea" usipoenda lawama

Mpaka Leo huwa najifikiria Mara mbili mbili suala LA kuangalia mgonjwa.
 
chef detat

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
16,851
2,000
Dah! Nimewahi kuumwa sana alafu nilipopona nikakutana na manzi fulani akaniuliza "nasikia ulikuwa unaumwa ?" nikaharibu nikauliza nani alimwambia, alijisikia viby sana
 
Saint Anno II

JF-Expert Member
Sep 12, 2021
350
1,000
Kwa dunia ya sasa kama ukisikia mwenzako ni mgonjwa mjali kwa kumpigia simu na kumfariji kadiri maradhi yake yanavyokuwa marefu au mafupi,kisha tafuta siku ktk mazungumzo yenu mpe ahadi ya kwenda kumuona so kwa hatua hii kama atakuona snitch atakukataa kwa sababu yoyote atakayoona yeye inafaa akikubali sawa.

Ikiwa alikupa yeye taarifa unaweza wakati wowote kwenda kumtizama,kwa watu wazima huwa hawana shida ni vizuri ukisikia wapo ktk hali ya maradhi ukawaone bila hata taarifa maana wao hawana tena cha kupoteza.
 
Chakwale

JF-Expert Member
May 17, 2015
1,031
2,000
Ni upuuzi kuona anaekuja kukuona wakati unaumwa anakuja kukuchunguza or mbea. Ugonjwa ni suala mtambuka hakuna anaependa kuumwa.

Anaekuja kukuona ni vile anakujali na kukuthamini ndio mana anakuja kukuona. Ukiumwa na ukatembelewa na MTU inakupa faraja mgonjwa na pia kukupa hata unafuu fulani mana kinga za mwili zinaimarika.

Binafsi huwa nawaona washamba na watu katili sana wenye tabia hizo za kutoa Maneno ya hovyo linapokuja suala na maradhi.

Sisi ni binadamu tumeumbwa tofauti na wanyama kujuliana hali ndipo tofauti yetu na wanyama ilipo.
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
3,298

Ulikuwa unajitambua miaka ya ngoma imeshika hatamu.Asikwambie mtu wengine walikuwa wanaenda kumshuhudia mgonjwa jinsi alivyo konda kisha kwenda kusambaza umbea.

Wagonjwa wa ukimwi walikuwa wakali kweli halafu hata kuinua mkono hawawezi ila sauti ya ukali kubwa
 
njumu za kosovo

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
569
1,000
Ulikuwa unajitambua miaka ya ngoma imeshika hatamu.Asikwambie mtu wengine walikuwa wanaenda kumshuhudia mgonjwa jinsi alivyo konda kisha kwenda kusambaza umbea.
Wagonjwa wa ukimwi walikuwa wakali kweli halafu hata kuinua mkono hawawezi ila sauti ya ukali kubwa !!
Umenikumbusha mbali sana bwana bwana kipindi hiko huo ugonjwa ndo watu wanabaki kichwa tu na mbavu walikua wakali hatari hatariii hata kama mtu alikua mstaarabu lakini akishaanza kuumwa tu anakua na mikwara dunia hakuna
 
MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
1,178
2,000
Kuna watu wa ajabu sana duniani. mtu anaumwa, kumuona hawaendi na taarifa zako wanasambaza. shukuru Mungu unaruhusiwa hawajui wanaendelea kusambaza uko mahututi. ghafla wanakutana na wewe, mnasalimiana wakupa pole, wanasema tulipata taarifa kwa fulani uko mahututi (aliyewapa taarifa hakuja kukuona wala hakuwasiliana kwa simu) ndio utajua kuna wasemaji wa familia wakujitolea na wengine wanatoa huduma hiyo online tena bure.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
15,389

Mimi nadhani tatizo sio kwenda kumwona mgonjwa, tatizo ni mahusiano ya yule anayeenda kumuona kabla hajawa mgonjwa.

Kama palikua na umbali kimahusiano ya kujuliana hali ni wazi kabisa kusema unamjali mtu sababu ni mgonjwa lazima izue maswali kwake! Upendo huo umeanza lini!? Ni sawa pale mtu akifa ndio watu wanamchangia pesa hata kumuandalia mazishi lakini alipolipokuwa hai huo upendo hukuwepo kabisaaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom