SoC01 Matembezi Makaburini

Stories of Change - 2021 Competition

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,506
Nilifiliwa na tukaenda kuzika Makaburini.

Baada ya Maziko nilijikuta nikipata hamu na kiu ya ajabu sana ya kutaka kutalii Makaburini.Basi nilianza mzunguko wangu taratibu huku nikisoma mawe ya makaburi yaliyoandikwa JINA,mwaka wa kuzaliwa na mwaka wa kufa.Makaburi mengine yalitiwa nakshi sana kwa nje na mengine yalikuwa ya kawaida.Katika matembezi haya nilitafakri mengi sana kwani niliona watu waliozaliwa miaka michache iliyopita na waliozaliwa miaka mingi iliyopita.Nilijaribu kutafakari kwa kina kwamba chini ya mawe haya ililala mifupa,tu na kwa wale ambao bado walikuwa fresh basi ilikuwa na muozo tu.

Kaburi moja lilinivutia sana lilikuwa na jina la mtu ambaye nilimfahamu lakini si yeye.yeye bado hajafariki.Nilizunguka katika makaburi yote na nikajikuta naanza kutafuta kama kuna kaburi ambamo amezikwa mwenye JINA kama la kwangu.Nilitembea Makaburi yote kwa umakini mkubwa na sikufanikiwa kukuta hata ambaye tulishe ubini tu.Naelewa sababu,huenda ni pamoja na desturi yetu ya kupenda kuzikwa kwenye makaburi ya familia.Na hapo nikajiuliza hivi nikifa nitazikwa wapi?Nilipomaliza matembezi niliketi kwenye kaburi moja wapo nikaswali kwa ajili marehemu wote pale huku nikitafakri fumbo la kifo.

Niliwakumbuka ndugu zangu waliotangulia kufa,rafiki zangu ambao wametangulia kufa,wengine kwa maradhi,ajali n.k.Nilijiuliza hivi kati ya ambao wameshakufa na ambao wako hai ni wapi wengi?Nilicheka moyoni nilipotambua kwamba waliohai ni wachache kuliko waliokufa.Nikawaza kwamba kama wafu wakifufuka wote basi dunia itafurika,nikacheka.

Nikayatafakari maisha yangu,Nikamkumbuka Rafiki wangu wa hisia STEVE JOBS mwanzilishi wa APPLE ambaye naye ni Marehemu.Nikawakumbuka na magwiji wengi ambao tayari wamekufa.Nikayatazama maisha yangu mpaka wakati huu.Nikajiuliza JE ninaishi maisha gani?Hakuna atakeyebakia so ninaishi maisha gani?Nilijaribu kukumbuka matukio mbalimbali katika maisha yangu,watu niliowaumiza,Niliowatendea wema,makosa niliyofanya,maamuzi niliyofanya na matokeo.

Niliyatafakari matarajio na matamanio yangu.Niliyatazama maisha yangu mwezi mmoja ujao,miaka mingi ijayo.Nikasema mbona kama ni ubatili?Nilikumbuka kwamba nimeisha aina nyingi za maisha,maisha ya ukuu na ya kujidhili maisha ya kutenda wema na kutenda uovu,maisha ya uchafu na ya usafi.Niliyakumbuka yote nikajiuliza tena JE maisha ni ubatili?

Nilijawa na huzuni nilipowakumbuka rafiki zangu wengi ambao walifariki wakati wakiwa wanaelekea katika hatua muhimu ya maisha yao.Rafiki yangu mmoja alikuwa ameanzisha kiwanda na kampuni akiwa na umri mdogo na akawa na mafanikio akafariki katika umri mchanga wa miaka 34 wakati akiwa katika hatua ya mafanikio katika maisha yake.Rafiki yangu mwingine alipata scholarship ya PHD na wakati anaanza masomo akafariki.Nikiwakumbuka wengine wengi ambao walifariki katika hatua muhimu za maisha.Huzuni ikanishika na maumivu moyoni.

Nikakumbuka rafiki zangu wengine ambao walifariki wakaacha watoto wao wakiwa wadogo sana,wengine walifiliwa na familia nzima wakajikuta wamebaki wenyewe tu.Nikawakumbuka mayatima,wajane na wagane ambae waliwapoteza wawapendao.Nikajawa na huzuni kuu moyoni.Nikajiuliza je HUU ni Ubatili?

Niliketi pale kwa muda mrefu sana nikijiuliza ni nini cha kufanya na maisha haya ambayo mwishowe yataisha,nitazikwa na kuoza?Nilipatwa na hofu kubwa sana nilipojua kwamba hakuna cha kuogopa wala kuhofu zaidi ya hofu yenyewe.Niliinuka nikawaaga wale wa makaburini nikawaambia,"HAPA nitakuja wakati wangu ukifika ila kwa SASA wacha niende nikaishi maisha yangu"

Nikasema safari hii naenda kuishi maisha yangu,Nitayafanya maisha yangu yawe bora lakini zaidi nitaifanya dunia kuwa sehemu BORA.Kwa kadiri ya KARAMA na uwezo wangu nitajitahidi niifanye DUNIA kuwa sehemu BORA KWA watakaobakia kwani hio ndio maana pekee ya maisha.

Siku zetu hapa duniani zinahesabika,dakika,saa na sekunde zinahesabika kwa nini usifanye Jambo kuifanya dunia kuwa BORA?Kwa nini usiamue tu kuotesha miti katika sehemu ambazo zinahitaji miti?Kwa nini usitunze mazingira,kwa nini usiwe mkarimu?Kwa nini usitoe maarifa kwa watu?Kwa nini usijifunze vitu vipya ili uweze kuwa na mchango bora kwa jamii yako?Kwa nini usitoe ushauri mzuri kwa watu?Kwa nini usitumie muda wako kuifanya hii dunia kuwa bora kwa wanaobakia?

Kwa nini usiondoe chuki moyoni mwako na kusamehe wanaokukosea?Kwa nini usitende wema?Wanadamu wote ni mavumbi kwa nini tuchukizane?Ifanye dunia iwe sehemu bora,wapende wanadamu wenzako,wasaidie na onyesha shukrani kwa wanaokusaidia.UTAKUFA tu.Kuwa mkweli na muwazi kwani maisha ni haya haya tunayoishi changamoto ni hizi hizi.

Wewe unapomwaga chakula kwa ulafi tambua kwamba kuna wanaolala na njaa na katika kutoa hakunaga kidogo.Hizo nguo zako unazoona hazifai kuna ambae zinaweza kumsitiri na kumfanya ajisikia mwenye staha.Kwa nini usitende wema kidogo tu hata kwa jirani yako?Kwanini wewe uwe mwepesi wa kujadili mabya ya watu lakini kuwaambia na kuwashauri unaona vibaya?Kwa nini ufurahie mateso ya mwenzako?Kwa nini ufurahie kufedheheka kwa wengine?Kwa nini uchukie kufanikiwa kwa wengine?Fanya kitu kidogo tu uifanye dunia iwe sehemu bora ya kuishi.Mpe mtu sababu ya kucheka,mpe mtu sababu ya kuona thamani ya maisha,muoneshe mtu heshima na utu.Muonesha staha.Kwa nini wewe unakula na kusaza lakini huwezi kufanya ukarimu kwa wengine?

Ndio wanadamu wamekuwa waovu na wengine wanatumia kama kisingizio lakini sidhani kama ni kweli kwamba hakuna nafasi za kutenda wema.Kweli nawaambieni kuna wanaotamani kupata fursa ya kutendea watu mema hawapati.Kuna wanaotamani kupata watu wa kuwaomba ushauri wanakosa,kuna wanaotamani kupata wa kuketi na kula nao wanakosa.Kwa nini wewe upate fursa ya kutenda mema halafu usitende?Kwa nini?

Kwani utapungikiwa nini ukiotesha mwembe nyumbani kwako?Utapungukiwa nini kama ukimsaidia mtu mwenye shida ya ajira,elimu,mtaji au hata ushauri?Utapungukiwa nini kama ukijitolea damu?Ukiwasaidia Yatima katika vituo vya yatima?Utapungukiwa nini ukinunua BOX la kalamu ukaenda shule ya hapo jirani ukawagawia wanafunzi?Utapungukiwa nini kama ukitoa Daftari kama zawadi kwa wanfunzi walio 10 kumi bora katika shule uliyosoma au iliyoko jirani?Utapungukiwa nini ukiwanunulia watoto wa maskini sare za shule?Utawatia moyo na utajisikia vyema kwa kutenda mema

Safari yangu ya makaburini ilinifikirisha sana,Nilijifunza mengi na nilitafakari Mengi.Najipanga nami nitende wema mdogo mdogo.SOTE TUTAKUFA.TUIFANYE DUNIA IWE SEHEMU BORA

Kama andiko hili limekuamsha basi GONGA VOTE ila cha muhimu zaidi ni kuifanya dunia kuwa sehemu BORA.Hujachelewa ANZA LEO.SHIRIKI
 
Tuifanye Dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi, ni wazo zuri na ndio maana ya maisha. Makaburi yote uliyoona kama kuna waliokufa kwa kudra za Mungu ni wachache. Vifo vingine ni michezo michafu ya dunia, ni katika kutekeleza usemi "maisha ni mchezo" . Basi tuifanye Dunia mahali pazuri kwa njia halali, nasema hivyo kwani mimi (58 years) nimeona mengi, inaweza ikawa heri waliokufa kuliko wanaoishi (kwa wengi sio wote)
 
Zamani wamisionari walileta nguo makanisani ikiwa ni misaada kwa waumini. Walipokwenda kwao likizo walieleza maisha halisi ya huku kwetu na kila muumini alitoa alichonacho.
 
Asante Mkuu kwa kuunga mkono,Unajua mpaka mtu akupe kura ni lazima umshawishi.Kwa jinsi ninavoona labada andiko halijashawishi.
Tatizo wale wa mobile app tunapata kazi sana kupiga kura
 
Unajua mimi naona hata ukiwa mzuri vipi wanadamu wana makwazo sana, sometimes wanakufanya uwe guilty kwa vitu usivyopenda kufanya
 
Hii dunia unaweza ukawa mtu mzuri sana kimatendo, huruma na mtoa msaada pia, ukawa na notion kuwa wote duniani hapa tunapita ni vizuri kuwa wakarimu na mwema kwa wenzetu wanaotuzunguka lakini ukweli ni kwamba watu WABAYA huleta makwazo kwa watu wenye nyoyo safi yani unakuta tu mtu ni msafi kiroho lakini anatiwa sumu na watu wabaya moyo unafura jaziba na hasira na kupelekea makwazo na mwisho wake kumkosea Mungu ,


Ni vizuri kuwa mtu mwema mtu mwenye kutoa msaada katika jamii kwa wenye uhitaji na matendo mazuri maana thawabu za Mungu zitamiminika juu yako
 
Unajua mimi naona hata ukiwa mzuri vipi wanadamu wana makwazo sana, sometimes wanakufanya uwe guilty kwa vitu usivyopenda kufanya
Lakini ni ukweli usiofichika kwamba kila mwanadamu hufikiri hivo hivo na matokeo yake wengin tunajikuta tunakuwa wabaya na wale tunaowatendea mabaya nao wanafikiri hivo hivo na kutenda mabaya pia.SO bado naamini nafasi ya kutenda wema inapopatikana basi na tutenda wema.
 
Back
Top Bottom