Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Kama ukibahatika kufika maeneo ya yanayozungua viunga vya hospitali ya mwananyama kuna kitu fuani kitakugusa na hasa maeneo yanayozunguka ukuta wa hospitali hiyo kwenye vioski vya juisi na chai
Utakutana na idadi kubwa ya vijana wa moto na makamu wakiwa na miili dhaifu na nyuso za kukunjamana, hapo awali walikua wanajikusanya jirani kabisa na ukuta wa hospitali na sasa wanakusanyika eneo lenye gereji wakiongozwa na kinara wao Ray C ambaye yeye huacha na kurudi
Msingi wa mada yangu ni jinsi ambavyo vijana hawa wanavyokula dawa ndani ya hospitali na mara tu wanapotoka wanaendelea kujidunga na kuifanya kazi yoote kuwa ni ubatili na kujilisha upepo na kunishawishi nitafakari kwamba huenda aidha wamefanya zoezi hili kuwa ni kijiwe cha kukutania ama ni aina ya mtaji wa kufurahisha familia zao na wakipewa nauli ya kula dawa wanaishia kunywa chai na juisi na kisha kuendeleza libeneke
Nitoe wito kwa mamlaka husika kuliangalia hili pia kwa kuwa na mfumo madhubuti wa ufuatilliaji na kadhalika niwasihi vijana ama wazazi/walezi/marafiki kuendelea kutoa ushauri nasaha kwa kundi hili