Matayarisho ya Nyerere day na Hamza Kassongo on Sunday

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,906
30,245
MATAYARISHO YA NYERERE DAY NA HAMZA KASSONGO ON SUNDAY

Hamza Kassongo amenihoji historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na jinsi alivyoishi na marafiki zake aliojuananao siku za mwanzo alipofika Dar es Salaaam mwaka wa 1952.

Nilimweleza Hamza Kassongo historia ya Mwalimu Nyerere na wazalendo waliompokea yeye na mkewe Mama Maria watu ambao historia imewasahau kabisa kama Shariff Abdallah Omar Attas na mkewe Bi. Chiku bint Said Kisusa.

Bi. Chiku, Bi. Titi na Bi. Tatu bint Mzee walimsindikiza Nyerere8 Uwanja wa Ndege safari ya kwanza UNO 1955.

Huu ndiyo ulikuwa ukaribu wao na Mwalimu Nyerere.

Ingekuwa kama si ushahidi wa picha za akina mama hawa wako na Nyerere nani leo angeamini historia hii?

Picha hizi zimehifadhiwa Jim Bailey Drum Magazine Photo Collection, Johannesburg.

Nilimfahamisha Hamza Kassongo historia ya Ali Msham aliyefungua ofisi ya TANU nyumbani kwake Magomeni Mapipa na pembeni ya tawi hili la TANU Ali Msham alimfungulia Mama Maria duka dogo la kuuza mafuta ya taa.

Nilimchukua katika mazungumzo yetu Hamza Kassongo hadi Lindi kumkutanisha na wazalendo wengine marafiki wa Mwalimu kama Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Suleiman Masudi Mnonji kwa kuwataja wachache.

Hawa ndiyo walioieneza TANU Southern Province ambako maadui wa TANU walikuwa wanaeneza propaganda kuwa TANU imedhamiria kuleta Vita ya Maji Maji dhidi ya Waingereza.

Uongo huu uliwafanya baadhi ya wananchi kuiogopa TANU.

Tulifika hadi kwa Msham Awadh kijana muuza uzuri katika kikapu akitembeza biashara yake nyumba hadi nyumba.

Awadh Msham alifungua tawi la kwanza la TANU Mikindani na nikamweleza nyumba ya gorofa ya Ahmad Adam ambayo Nyerere alifikia mjini hapo.

Yapo mengi.

Kipindi In Shaa Allah kitarushwa kesho Jumapili saa tatu usiku TVÈ.

Screenshot_20211016-165528_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom