Kaduguda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2008
- 724
- 641
Heshima mbele wadau wote!
Nimekuwa nikitatizwa sana haswa ninapoona huu utitiri wa matawi ya vyama vya Siasa haswa vya Tanzania kufungua matawi nje ya nchi na haswa nchi za magharibi na India. Kwani sijasikia Labour, Republicans wala Democrats kufungua matawi nje ya nchi zao.
Hivi nini haswa sifa ya mtu kuwa mwanachama huko ughaibuni? Je ni kwa mtu aliye mtanzania tu au hata aliyeukana uraia wake anaruhusiwa? Kama mtu ameukana uraia wa TZ na kujibandika wa USA au UK nadhani si mtanzania tena huyo na hivyo moja kwa moja anapoteza stahili yake.
Hofu yangu ni kuwa na wanachama wa vya vyama vyetu vya siasa ambao si wa-Tanzania na hivyo kupoteza ile maana halisi ya vyama vyetu. Hii ni kusema kwamba yeyote yule pasipo kujali uraia wake anaweza kujiunga na chama chetu au kuanzisha tawi popote pale duniani apendapo. Kitu hiki hakiniingii akilini kabisa.
Mods kama hii imeshajadiliwa sehemu waweza ihamishie huko!
Nawakilisha

Last edited: