Matawi ya CCM ndani ya vyama vya Upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matawi ya CCM ndani ya vyama vya Upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kidatu, Feb 3, 2009.

 1. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Upinzani wa kweli hakuna Tanzania. Vyama vingi vya upinzani ni matawi ya CCM ama kuna watu wa CCM wamepandwa ndani yake. Ukombozi wa Mtanzania uko mbali sana. Angalieni upuuzi wa msomi na mwanasheria aliyebobea.

  2009-01-19


  DK MVUNGI AYEYUSHA RAI YA KUMSHITAKI MKAPA

  Written by James Magai

  MHADHIRI maarufu wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, amesema hakuna sheria inayoweza kutumika kumshitaki Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kwa mambo anayotuhumiwa.  Kauli hiyo ya Dk Mvungi, inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wanasiana na wanaharakati, kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili ashitakiwe kwa tuhuma za kufanya biashara akiwa Ikulu.  Wanasiasa hao ni pamoja na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa. Dk Slaa pia ni Mbunge wa Karatu  Hivi karibuni, Mohamed ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, alielezea azma yake ya kutaka kuwasilisha hoja binafsi bungeni, kumtaka Mkapa aondoelewe kinga na hatimaye ashitakiwe.  Kwa upande wake, Dk.Slaa amekuwa akidai kuwa Mkapa anaweza kushitakiwa hata bila kuondolewa Kinga.  Lakini akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu kuhusu uwezekano wa kumfungulia mashatka Mkapa kwa uthuma hizo, Dk. Mvungi ambaye ni mtaalamu wa Sheria na Katiba, alisisitiza kuwa hakuna sheria yoyote inayoweza kumtia hatia Mkapa.  Dk. Mvungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, aliliambia Mwananchi kuwa watu wanaomjadili Mkapa wanajadili kwa hoja nyepesi tu ambazo hazina nguvu za kisheria.

  "Hakuna sheria inayoweza kushitaki Mkapa kwa tuhuma za kufanya biashara akiwa Ikulu.Wale wote wanaojadili hoja hiyo wanajadili kwa hoja nyepesi tu na wanasukumwa na emotions (maono) zao tu na si kwa misingi ya kisheria," alisema Dk. Mvungi.  Alisema ingawa Mkapa wakati wa utawala wake aliwaminya na kuwakandamiza wapinzani, lakini kwa hili yeye kama mtaalamu wa sheria hawezi kutumia kigezo hicho cha uhasama wa kisiasa,wala taaluma yake kama silaha kushinikiza kumwangamiza na kwamba anazungumza kisheria.  Ingawa alikiri kuwa kitendo cha Mkapa kufanya biashara akiwa rais wa nchi hakifai, lakini alisema kisheria rais kufanya biashara si kosa na kwamba hakuna sheria inayomzuia kufanya biashara.  "Hata kwenda kukopa pesa benki, siyo kosa, ila tu inaweza kuonekana kuwa umepewa kipaumbele kwa sababu ya nafasi yako, lakini bado hakuna sheria inayomzuia kiongozi yeyote wa seriakali wala hata awe rais kuomba mkopo benki," alisema Dk. Mvungi.  Alisema yeye akiwa mwalimu wa sheria, anazungumza kitaalamu na kwa ushahidi wa kisheria,na kwamba kwa tuhuma hizo dhidi ya Mkapa haoni kosa la kisheria.  "Kama wanasema ni kosa basi wanieleze hapa kosa ni lipi na wanioneshe ni sheria gani inayomshitaki,"alisisitiza Dk.Mvungi.  Alisema wanaojadili suala la Mkapa kabla ya kwenda mahakamani kumfungulia mashitaka kwa kufanya biashara Ikulu inabidi kwanza waangalie Katiba ya nchi, Sheria ya Mambo ya Urais (Presidential Affairs Act) na Sheria ya Huduma za Jamii (Public Service Act).  "Kama kuna kifungu cha sheria kinachozuia rais kufanya biashara wakilete tukijadilina kama hakuna basi tuache kupiga kelele, vinginevyo turudi na tuangalie sheria zetu,kwa kuwa zina mapungufu".  Akitetea hoja zake Dk. Mvungi alisema yako mambo mengi tu ambayo hayafai kufanywa na na kiongozi au raia yeyote kimaadili, lakini si kinyume cha sheria na hivyo mtu hawezi kushitakiwa kwa kuwa hakuna sheria inayovunjwa.
  "Mkapa anaweza kuitwa kwenye Tume ya Maadili ya viongozi na kuhojiwa kama kweli alifanya biashara ndani ya Ikulu,na hata kama akikiri bado hatuwezi kumfungulia mashitaka" ,alisema Dk Mvungi.  Aliongeza kuwa ikiwa Mkapa atakiri mbele ya tume hiyo, itakuwa nafasi ya kurekebisha sheria za nchi kwa ajili ya kukabiliana na rais ajaye na si kurudi nyuma hata kwa yule aliyefanya mambo kama hayo kabla ya marekebisho ya sheria hiyo.  Dk. Mvungi anakuwa ni mwanasiasa wa kwanza kumtetea Mkapa kwa hoja za kitaalam, tangu tuhuma dhidi yake zilipoibuliwa na wanasiasa kuanza kujadiliwa kwa mtizamo wa kutaka kumshitaki.  Watu wengi ambao wamekuwa wakimtetea Mkapa dhidi ya tuhuma hizo,wakiwemo wabunge,wanaharakati viongozi wa kidini na wananchi wa kawaida wamekuwa wakimtetea Mkapa kwa hoja za kiutendaji wake tu kuwa amelileta taifa heshima na si kwa misingi ya kisheria.  Mkapa anatuhumiwa akiwa madarakani alianzisha kampuni ya Kiwira Coal Mine ambayo ilinunua mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira akishirikiana na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini Daniel Yona.

  Comments Add New Search  Write comment
  Name:
  Email: do not notifynotify
  Title:  Powered by !JoomlaComment 3.23
  3.23 Copyright (C) 2007 Alain Georgette / Copyright (C) 2006 Frantisek Hliva. All rights reserved."
  Next >
  [ Back ]
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kidatu,
  Mkuu huyu msomi ana matatizo kweli kweli... wala sishangai majjibu kama haya yanapotoka kwa wanasheria wetu..
  Ukisoma sheria ya Mambo ya Urais (Presidential Affairs Act),au hizo sheria ya Huduma za Jamii (Public Service Act), pamoja na Azimio la Zanzibar - Hakuna kifungu hata kimoja KINACHOMRUHUSU rais kuzitumia Ofisi za Ikulu kwa biashara zake..

  Hakuna sheria yoyote duniani iliyotangulia maovu....isipokuwa sheria hutungwa baada ya kutokea maovu hata ikiwa sio nchjini mwetu kwa hiyo ni muhimu afahamu kwamba It out of question rais kuzitumia ofisi za Ikulu kwa biashara binafsi..
  Kutokuwepo kwa sheria inayozuia haina maana inaruhusiwa kufanya hivyo na ndio maana nimetoa mifano hata ktk imani zetu za dini kuwa hakuna kitabu hata kimoja kinachozungumzia specifically kwamba Kulawiti (molest) watoto wadogo ni dhambi kubwa....Na hata ku rape wanawake utaona ktk Biblia imekatazwa tu kwa wanawake ambao tayari wamekwisha chumbiwa..wakati rape ni kitendo kiovu kwa wanawake wote! Hivyo haina maana ni RUKSA ktk dini zetu kufanya vitendo ambavyo havikukatazwa na misahafu..
  Nje ya dini, hakuna sheria yoyote Kitaifa au kimataifa inayomkataza mtu kuoa mama, au dada yake hivyo huwezi kunambia rais wetu kesho akiamua kumwoa mama yake basi watu tupige makofi na tuache emotions ati kwa sababu katiba haizungumzii miiko ya viongozi ktk ndoa..

  Ni Ujuha na Upumbavu mkubwa kuwaambia wananchi kwamba wanazungumza kwa emotions wakati kiongozi wa nchi ametumia madaraka yake kufanya mambo machafu..Elimu za mapishi hizi zina taabu kweli kweli yaani mtu unashindwa kufikiri nje ya kabati ulofungiwa!
   
 3. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Mkuu Kidatu,
  Kama kweli wewe ni muungwana basi tafadhali muombe radhi Bw. Mvungi kwa shutuma zako ulizozielekeza kwake kwamba yeye amepandikizwa na CCM katika upinzani.
  Pili, uwaombe radhi CCM kwa kubandika shutuma dhidi yao ambazo huna ushahidi wowote wa kuthibitisha maneno yako.
  Tatu, ukumbuke kuwa Bw. Mvungi ametoa maoni yake kitaalam zaidi na wala siyo kwa msukumo wa kisiasa. Katika kutoa maoni yake ameonya kuwa kinachofanyika sasa hivi ni mashinikizo yanayotokana emotions za watu na wala siyo kwa mujibu wa sheria.
  Kwa mtazamo wangu ni kwamba kinachofanyika kwa wanaoshikilia hoja hiyo bila ya kuwa na mikakati inayoweza kufanya kazi, ni kupiga kelele zisizokuwa tija at the end of the day zaidi ya kutaka kutafuta mitaji ya kisiasa. Ni muhimu kwa wanajiita viongozi hasa hawa wabunge wakafanya kazi zao kwa kuangalia na kuzingatia sheria ambazo wao ndiyo watungaji. Na kama basi wanaona hazifai hao wabunge wana nafasi ya kuomba marekebisho, vinginevyo kelele hizi hazisaidii nchi na hazina manufaa yeyote.

  Mwisho kwa contents za maoni ya Dk. Mvungi, hakuna mahali popote ambao pana kupelekea wewe kutoa stress zako kwa kutumia jina la CCM.

  Hapa jukwaani hatuko kwa ajili ya kumpendeza mtu au kikundi cha watu, kama huna ushahidi na madai yako yaliyobeba kichwa cha habari basi huna haki ya kuendelea kupotosha umma kwa manufaa yako binafsi au kikundi chako.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundamilia07,
  Mkuu waneno haya ya huyu mwanasheria ni aibu tupu.. huwezi kusema wala kutumia neno emotions ktk sheria kama sababu hata kidogo kwani bila emotions sheria zisingetungwa..Kama wewe hufahamu kwamba kuua ni kosa wala huoni ubaya wake kwa nini utunge sheria!..

  Maamuzi ya kisheria (hukumu) yanayotokana na emotions ndiyo hukataliwa kisheria lakini kusimamisha kosa au shitaka ni lazima emotions ziwepo laa sivyo watu wasingeshtaki baada ya kuibiwa, ndugu zao kuawa na kadhalika...
  Ebu nambie hivi wewe unafikiria ni kitu gani kinatufanya tukumbuke genocide na pandikizi zote za sheria zinazohusiana na genocide!..Hakuna sheria iliyokuwa ikimzuia Hitler kufanya alofanya..Kwa hiyo unataka watu wasahau kwa sababu tu kisheria hakuna mahala inakatazwa!..
  Mkuu acheni siasa ktk kuzitumia elimu zenu..Mvungi maelezo yake yote ni siasa tupu na kaitumia sheria kuficha maovu lakini huwezi kunambia wale ati Mapadre na Masheikh wanao molest watoto wadogo wasifunguliwe mashtaka ktk dini zao ati kwa sababu hakuna sheria inayowakataza wao (viongozi wa dini), na kwamba ati kelele za wananchi zinatokana na emotions!..
   
 5. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkandara,

  Mimi si mwanasheria, lakini nitakuwa **** endapo nitajaribu kupingana na Dk. Mvungi kwa kutoa hoja ambazo si za kitaalam. Nina hakika kabisa kwa Dk. Mvungi katika kuongelea hili haihitaji kufanya research kama vile mimi ambaye si mwanasheria ambapo ingenibidi nifanye utafiti na kujua sheria inasemaje. Lakini vilevile itanichukua muda mrefu kuelewa kila kitu au kila sheria na inavyofanya kazi. Kwa mantiki hiyo basi ili kupingana na Dk. Mvungi one needs to be sure na anachokiongea rather than kutoa emotions zetu ambazo at the end hakuna tunachofaidika.
  Sisi kama maamuma katika sheria hatuna budi kusilikiza mhadhara toka kwa Dk. Mvungi na kuuliza pale ambapo tunadhani hatupaelewi ili tujifunze zaidi. Hapa Mkapa anatuhumiwa kwa kufanya wrong decision na sisi tunaongozwa tunashabikia appeals ambazo ziko wrong decided...au ndiyo kusema kuwa sisi wananchi ndiyo reflection ya viongozi wetu?
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundamilia07,
  Mkuu wangu elimu ni zaidi ya hisia zetu ktk kila swala na ndipo watu kama Mvungi wanapoingia..Huwezi kunambia ni lazima usome kufahamu kwamba binadamu anatakiwa kula, au usome ndipo ufahamu kwamba unahitaji usafiri, electronics na kadhalika ktk matumizi yetu ya kila siku..na kama yatatumiwa vibaya basi ni lazima msomi ndiye mwenye kuelewa makosa yako wapi!
  Sheria inatokana na maisha yetu ya kila siku, maisha ambayo hayana msomi wala kabuntas, tajiri kwa maskini isipokuwa tunapofikia kutafuta solutions za mambo haya ndipo wasomi hungia kazini kutuongoza na sio wao kuwa immune.
  Kitu anachozungumzia Dr. Mvungi ni sheria ambayo haikuandikwa kwa njia yoyote ile. hakuna kifungu ktk sheria yoyote kinachoruhusu wala kukataza kutumia ofisi za Ikulu kwa biashara binafsi za kiongozi kwa sababu haijawahi kufanyika..
  Of course tutakuwa reflection ya viongozi wetu kama tutashindwa kuona makosa ya Mkapa kwa sababu ndani ya majumba yetu huyageuza kuwa madangulo tukashindwa kuona ubaya wa kufanya Umalaya ndani ya nyumba yako tukatazama swala ni kulisha familia..tunashindwa kutazama kosa badala yake tunatazama faida inayotokana na kosa hilo kuunda sheria za utetezi...
  Dr. Mvungi anatazama sheria ambayo haipo pande zote lakini ameamua kuchukua upande mmoja na kuuliza swali...Sasa mimi namuuliza yeye ni wapi ktk sheria hizo hizo imemruhusu rais kufanya biashara kwa kutumia ofisi za Ikulu?..
   
 7. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi sio mwanasheria na natoka nje ya mada lakini pia tuna-judge discussions zenu kutokana na mnachoandika. Je, hayo unayotuambia hapo ni kweli? Kwa sababu kama sio kweli, inawezekana na huko kwenye presidential affairs pia ume-interprete vingine. Nnachojua hata TZ mtu kumuoa mamayo ni kosa [soma hii, 158(i) ya penal code]
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Feb 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Outliner,
  Mkuu that's exactly nachojaribu kusema hapa kuwa sio lazima sheria izungumze kitu chenyewe ili sheria itumike na hakuna kitu kibaya zaidi kama kutumia sheria kupindisha ukweli..
  Ukisoma sheria nyingi ktk hiyo sexual Offences Provisions utaona zinazungumzia sana vitendo vya sexsual intercourse na kukataza mengi lakini sheria hizo hazikukataza kuhusiana na ndoa..Sasa kama mtu akioa mama yake kisha apatikane mwanasheria aseme ati wamwonyeshe mahala sheria inaposema Kuoa mama yako ni kosa, akijua wazi kuwa sheria inazungumzia ngono tu ndipo naposema huu ni Upuuzi mtupu...Ni kujaribu kuondoa fikra za watu ktk ngono na ubaya wake kwa kutumia neno ndoa!
  Wewe na mimi pamoja na watu wote haturuhusiwi kabisa kufanya biashara Ikulu kwanza haiwezekani lakini Mkapa anapofanya hayo yeye anapewa special exemption pamoja na kwamba ni makosa.. Halafu basi kibaya zaidi tunajenga hoja kuhalalisha alichokifanya bila aibu!
   
 9. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  '...nitakuwa **** endapo nitajaribu kupingana na Dk. Mvungi kwa kutoa hoja ambazo si za kitaalam.'

  Mkuu Mkandara,
  Mimi nimemaliza, nilichofaidika katika thread hii ni maelezo ya Dk. Mvungi ambayo mimi ninakwenda kufanya research ili niweze kumwelewa zaidi. Na endapo nitakuwa sijamuelewa mahali fulani, basi nitarudi kumuuliza.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,574
  Likes Received: 1,942
  Trophy Points: 280
  Mkandara akubaliana na wewe moja kwa moja...Kwa kweli huyu dokta amekuwa dokta mvunguni maana ndiko alitakiwa aseme hayo. Atathubutu vipi kuonra maneno kama hayo halafu ajiitre msomi? Ndio hapo either pandikizi ama keshapewa chake kutokana labda na influrmcr aliyonayo.
  Kusema rais anaruhusiwa kufanya biashara haina maana kuwa rais huyo anaruhusiwa kuiba mali za wananchi.
  Mvungu anasema hakuna sheria iliyomzuia rais kufanya biashara ikulu...Sasa naomba anieleze kama wizi nao unaruhusiwa ikulu. Yani hata mwalimu aliposema ikulu imekuwa pango la wanyan'ganyi basi kama si heshima ya mwalimu inawezekana angesema hakuna sheria inayomzuia rais kuiba ama kujiuzia mali za Taifa ama hata ikulu kuwa pango la wanyang'anyi....Ni onething kuiba na ni another kufanya biashara. Sasa hiyo Kiwira ukiwa kama mradi wa wananchi ndio biashara aliyojikabidhi kihalali then nina mashaka na huyo Mvungi
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana,
  Mkapa anashutumiwa kwa wizi wa mali ya umma. Anashutumiwa kwa kuhujumu uchumi, anashutumiwa kwa kukiuka taratibu za ofisi ya rais wa Tanzania na anashutumiwa kwa kutumia ofisi aliyoapa kuilinda kikatiba kujijazia mapesa mifukoni na kufanya biashara. Makosa haya katika nchi ya Ghana enzi za Rawlings hukumu yake ilikuwa ni firing squad. Vivyo hivyo na kwa wenzetu China. Siyo kufanya wrong decision. Mwizi wa kuku naye hufanya wrong decision lakini tunajua kinachomjiri anapokamatwa.
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dkt.Mvungi anajikanganya katika matamshi yake na yalimgarimu kule Tarime kwa kupigwa mawe.Dkt.Mvungi hana tofauti na Mwenyekiti wake J.Mbatia naona wanataka kuanzisha CCMb.Hivi kama hakuna sheria mfano inayomzuia Rais kufanya ngono/ufuska ofisini wakati ameapa kuilinda katiba ya nchi unawe kusema kweli ni sawa kufanya ufuska ofisini?Matamshi ya Dkt huyu ni sawa na miktaba ya kinyonyaji ya madini iliyosainiwa na wanasheria wetu,wote hawa ni wasomi lakini hukiuka maadili kwa maslahi fulani.
   
 13. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Pindamilia,
  Asante sana kwa mchango wa mawazo yako katika hili suala.
  Benjamini William Mkapa alikula kiapo cha kuilinda Tanzania, watanzania na mali zao kwa moyo wake wote, nguvu zake zote na akili zake zote. Hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba mali na utajiri wa nchi unakuwa chini ya wananchi, na wala si chini ya wageni ama watu wachache na ni kitu ambacho hata yeye mwenyewe Mkapa kwa sasa anakubali kwamba alifanya kosa na anajutia.
  Kama Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania alipaswa kuelewa kwamba yuko pale ikulu kwa ajili ya Watanzania na si vinginevyo. Tumejionea wazi kwamba Mkapa amevunja ama amekiuka kiapo alichokula. Alipageuza ikulu kuwa ofisi za ANABEN LTD kitu ambacho hakupaswa kufanya na wala hakijawahi kutokea katika Historia yetu ya Tanzania kampuni binafsi kuandikishwa na kutumia anuani ya Ikulu. Unakumbuka Bill Clinton alipofanya tendo la ngo'no white house na Monica Lewinski nini kilimkuta?
  Mkapa kwa kutumia madaraka aliyokuwa nayo alijiuzia kiwira cool mine (kwa faida yake na kundi lake) na si kwa faida ya watanzania, kitu ambacho hakupaswa kabisa kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba Mkapa ana kesi kubwa sana ya kujibu kwa Watanzania na hakuna sababu ya kumtetea.

  Matokeo ya Mkapa kuwa Ikulu ni pamoja na Watanzania kuwa wageni katika nchi yao na kundi kubwa la Wananchi ni masikini wa kupindukia, wachache ni matajiri wa kutisha mpaka wanauwezo wa kujiwekea dhamana mahakamani ya Shs bil 6 bila shaka wala hofu.
  Wakati huohuo tunasafiri kwenda nchi za nje kuomba msaada wa kuchimbiwa kisima cha maji kinachogharimu shs mil 138 tu kitu ambacho tungeweza kufanya wenyewe kama utawala wa Mkapa ungekuwa makini na kuwajibika kwa wananchi ipasavyo.
  Mkapa ametuacha pabaya na kamwe Watanzania hatuwezi kumsamehe kwa uchafu alioufanya.
   
 14. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu Pundamilia, nimefuatilia hoja zako na mkulu Mkandala. Samahani kama ntakukwaza lakini ukweli unanidhamu ya woga juu ya kiwango cha taalamu ya mtu. Pundamilia kuwa Dr. sio kwamba unajua kila kitu na haimaanishi unachokisema watu wasikichalleng. Kauli yako yakwamba kumpinga Dr. Mvungi bila hoja za kitaalamu ni ujua, ni feki na inadidimiza uwezo wa kujiamini hasa kwa watu ambao hawajafikia academic maturity.

  Nashukuru mkulu Mkandala amaendelea kukuelimisha japo inaonekana unagoma kuelewa. Anacho kisema Mkandala ndio uhalisi wenyewe sipendi nami nirudie kitu hicho hicho. Naamini Dr. mvungi ametoa tamko hili akiwa na dhamira tofauti kabisa na miiko ya taaluma yake. Ni aibu kauli za msomi kama huyu kusikika ulimwenguni zikiwa na udhaifu wa wazi kiasi hicho.
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kwa kuwa umeamua kuwa mouthpiece wa Bw. Mvungi na kwa kuwa yeye mwenyewe hajakanusha yaliyoandikwa na Kidatu, naomba umfikishie ujumbe kama ni muungwana aombe radhi kwa matamshi yake ambayo yametukera sana wengine na hayakufaa kutolewa na yeyote mwenye nia njema na taifa letu.

  Kwa kuwa wewe ni msemaji wa CCM, nakuomba uwaambie CCM kuwa kama wanahusika kwa namna yoyote basi wanapaswa kuomba radhi kwa matamshi ya Bw. Mvungi.

  Na wewe ukumbuke kuwa kuna wanasheria wengine wengi tu ambao hawakubaliani na Bw. Mvungi na hawasukumwi na hicho kilichomsukuma Bw. Mvungi kusema aliyoyasema.

  Sheria yetu mama inasema kuwa "no one is above the Law" na wezi hawatabaguliwa kulingana na nafasi au hadhi zao. Ni mahakama tu itakayo toa hukumu lakini kabla ya hapo shutuma zetu zinabaki pale pale.

  Kama wewe huwezi kuona tija at the end of the day, huo ni upofu wako. Mimi najua hili litakuwa fundisho babu kubwa kwa yeyote atakayepewa madaraka ya kuongoza nchi hii. Wanaotafuta mitaji ya kisiasa ni hao wanaokubali kuwa vibaraka na wananchi wameanza kuwashtukia.

  Kwanza unaanza vibaya - ni wanaojiita viongozi ama ni viongozi ?. Hii peke yake inanifanya nisiyatiilie sana maanani mawazo yako. Kama unadai viongozi ama wabunge hawaangalii na kuzingatia sheria (hiyo ni tafsiri yako) - kwa nini hawachukuliwi hatua ? Je, ni kwa nini watuhumiwa hawaendi mahakani ila kubaki wakilialia na kutetewa na akina Bw. Mvungi ?

  Hilo mbona liko wazi - wezi watapelekwa tu mahakamani na kama marekebisho yanahitajika, yatafanywa. Sasa bila hizo unazoita kelele haya yatawezekana vipi ?

  Once is chance, twice is coincidence but third time is a call for action.

  Kwa vyovyote vile unaonekana upo jukwaani kumpendeza mtu ama kikundi cha watu. Kwa maneno yako mwenyewe kama huna ushahidi na madai yako yaliyobeba kichwa cha habari basi huna haki ya kuendelea kupotosha umma kwa manufaa yako binafsi au kikundi chako. Usiku mwema.
   
 16. F

  Fataki Senior Member

  #16
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mkandara, msimamo wako ni mzuri ila acha kuongelea kitu usichokijua. Outlier amekusaidia ujue kuwa kuoa mama au dada yako ni kosa la jinai liitwalo incest. Badala ya kukiri kosa kiume, unaendelea tu kujikanyaga na hoja isiyo na kichwa wala miguu. Tutatuma makachero waje wakuone nyumbani kwako: usije ukawa umeoa ...
   
 17. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Mvungi na Mbatia ni walewale tu, controversial, kuna lao jambo!! Hata hivyo yeye sio kamusi ya kutafsiri sheria na katiba Tanzania!! Hakuna sheria pia inayomkataza mtu kuiba BOT?
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Pundamilia, hapa tupo pamoja sana hakuna cha kuongeza, hivi huyo Dr. Mvungi ni mwanasiasa wa chama gani cha upinzani?.
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  NCCR-Mageuzi,nadhani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 aligombea urais kwa chama hikihiki
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkulu Balatanda, shukrani kwa hii info unajua picha yako inanikumbusha wakulu wengi niliowaona hivi karibuni kwenye movie ya Notorious Biggie Smalls lakini thanxs for the info.
   
Loading...