Matauarisho ya Nyerere Day 2021

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,850
30,193
MATAYARISHO YA NYERERE DAY 2021
Tukielekea Nyerere Day 2021 wadau wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kwa hakika ndiyo historia ya Mwalimu Nyerere wamekuwa wakinihoji mengi kuhusu maisha ya Baba wa Taifa.

Mtangazaji wa TBC Television Safina Yasin leo alinitembelea nyumbani kwangu na tukafanya mahojiano kuhusu nyumba ya Mwalimu Nyerere Magomeni ambayo sasa ni Makumbusho.

Safina Yasin alitaka kujua Mwalimu ilikuwaje hadi akakaa Magomeni.

Nilimchuka mtangazaji kutoka nyumbani kwa Mwalimu Pugu hadi Mtaa wa Stanley alipoishi nyumbani kwa Abdulwahid Sykes kwa kiasi cha miezi mitatu baada ya kujiuzulu kazi ya ualimu mwaka wa 1955.

Alipotoka hapo ndipo Mwalimu akahamia Magomeni Maduka Sita na kuishia kwenye nyumba yake aliyojenga Mtaa wa Ifunda ambapo hakukaa hapo kwa muda mrefu akahamia nyumba ya serikali Sea View.

PICHA: Mwandishi akimuonyesha Safina Yasin vitabu katika Maktaba kuhusu Mwalimu Nyerere.

Picha nyingine ni nyumba ya Mwalimu Magomeni Maduka Sita picha ya juu yakiwa maduka yaliyokuwapo hapo na chini ni nyumba aliyoishi Baba wa Taifa, Mwalimu akionekana nje ya nyumba yake akiingia ndani.

Screenshot_20210928-172623_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom