Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Nchi yetu imejaa mauza mauza kila mahali, kila unapogusa ni uchafu tu , Raisi wetu Magufuli pmj na Uongozi wake kwa ujumla wameamua kupambana na hili na kuirudisha nchi kwetu ktk kwa Mafisadi lkn kuna watu wanakwenda Bungeni bila ya aibu na kupoteza muda wetu kushinikza Raisi wetu asafiri kwenda kuuza sura Ulaya, kuna wengine humu wanashinda kwenye mitandao na ktk mambo yoote wanataka Raisi Magufuli aende safari za nje, kweli kuna watu na viatu, na adui yetu sisi Waafrika na Watu weusi ni sisi weusi wenyewe na sasa naanza kuamini kabisa siyo kweli kwamba tuliuzwa Utumwa kwa nguvu na Wazungu na Waarabu bila ya idhini yetu bali ni sisi wenyewe tuliuza watu wetu kwa maana hakuna jinsi naweza kuelezea watu wabinafsi kama hawa wanaotaka Raisi wa nchi aende Ulaya wakati nchi inanuka kila kona, Raisi anajitolea kusafisha anakejeliwa anatukanywa mara hajui Kiingereza, mara hajasoma wakati Raisi Magufuli anachokipigania ni kwa manufaa ya sisi wote, wewe kama ni chadema leo, mwanao hatakuja kuwa chadema kesho bali atakuwa Mtz, sasa kwanini una-sabotage juhudi za kumtengenezea mwanao mwenyewe maisha mazuri kama siyo laana nini? !
Kwani Raisi Magufuli anashindwa kuanza kusafiri na kuhudhuria kila mkutano Dunia na kupeleka familia yake Ulaya shopping kama Raisi wa nchi?
Anashindwa nini kuhamisha watoto wake wakasome Yale ada milioni 200 kwa gharama ya nchi?
Anashindwa nini kuhamisha Familia yake yote Chato na kujenga kijiji kipya kwa gharama ya nchi?
Lkn hafanyi na yote hii ni kwa sababu ya hii nchi na vizazi vijavyo lkn bado tunamkejeli na kumtukana, sisi waafrika ni watu wa ajabu sana kwa kweli!