Salaamu kwenu!
Tanzania ilibahatika kuwa na kiongozi mmoja tu awamu ya kwanza mwalimu Nyerere, alikuwa na mapungufu yake lakini kama binadamu alikuwa na nia njema kwa kuhakikisha Tanzania inashinda vita dhidi ya umaskini.
Alipigania kuwepo na maadili katika viongozi, dira ya taifa ambayo ndiyo msingi wa taifa lolote lile la watu wenye akili timamu, huduma bora za afya, elimu bora kwa wote nk, alikataa na kuchukia rushwa, udhalimu nk.
Bahati mbaya sana yule mwalimu hakujenga mfumo imara utakaorithi na kuendeleza fikra zake katika uongozi, ni bahati mbaya hii jamani.
Sasa awamu zilizofuata Tanzania imepata watawala, tena mbaya zaidi ni watawala madhalimu hawa, natumia neno hili 'dhalimu' sababu ni kuwa hawa watu wanachojua ni kimoja tu kusababisha dhiki, shida na mateso kwa raia wasio na hatia.
Nani anabisha hapa? nani huyo? Umaskini tu kila kona unashamiri, huduma za afya mbaya, elimu duni, rushwa nk vimekithiri sana sasa kama siyo kusababisha mateso kwa raia ni nini hiki?
Mbaya zaidi hakuna hata dira ya taifa leo utaskia hiki, kesho oh mara kile hivi mara vile ni balaa tupu.
Lakini kwa mkwamo huu kwa nchi ya Tanzania wa kubeba lawama ni mtanzania mwenyewe namaanisha raia wa kawaida.
Kwa sababu kama hawa watu waliapa kuwatumikia raia na kuwa viongozi waadilifu wanapokengeuka na kuwa madhalimu wakuwadhibiti ni raia wa kawaida.
Ndiyo ni raia tu mwenye uwezo wa kuwadhibiti watawala hawa madhalimu siyo EU, siyo USA, China wala Urusi.
Raia kuendelea tu kulialia na kusubiri eti sanduku la kura huku ni kukosea sana, njia nzuri ni kuchukua hatua palepale mtawala anapoenenda kinyume na alivyoapa kama kupinga kwa maandamano ya amani na kuwashinikiza waachie hizo ngazi.
Maandamano ingawa yamekatazwa kwa sasa lakini katazo hili ni batili sababu limevunja katiba ya nchi.
Usinambie kuandamana ni vurugu au vyombo vya ulinzi na usalama kama polisi, JWTZ wataua waandamanaji wasio na hatia, kama kuua ni dili kwao acha watuue iko siku maneno na matendo ya WATESI WETU HAWA nao vitapimwa katika midhani ya haki.
Karibuni tujadili.