MATATIZO YASIWE SABABU YA WEWE KUACHANA NA MPENZI WAKO.

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
3,327
2,000
Habarini

Nimekuwa nikitafakari sana Kupitia Nyuzi mbali mbali zinazo wekwa Na wadau Mbalimbali humu! Watu wamekuwa wakilalamika sana Juu ya Matatizo/Tabia mbaya Za Wapenzi wao na kuona kuachana Kama Ndio suluhu ya matatizo/Tabia hizo, Tabia/Matatizo ninayo yasema ni kama yale kuwa mpenzi wangu hanirishishi,mpenzi wangu ana michepuko,mpenzi wangu ana mdomo mchafu,mpenzi wangu hajui kuoga na mengine mengiii kama hayo

Ni wakumbushe tuuu kitu kimoja kuwa Wote hapa hatukuzaliwa tunajua kusoma na Kuandika,Lakini waalimu wetu walitufundisha hadi tukajua kusoma na kuandikaa na Kumbuka kuwa Shule wote hatukuwa na Uelewa sawaa wapo walio kuwa wanavichwa vyepesi akifundishwa A leo kesho ashajua kuna wengine walikuwa na uelewa wa kati na wengine walikuwa vichwa vigumu kabisa lakini kuanzia Chekechea,awali na kuendelea walimu wetu hawakukata tamaa ya kutufundisha hadi tuelewee pamoja na Utofauti wetu katika uelewa,Walimu walihakikisha/Wanahakikisha Kila mmoja Kwa wakati wake anajua kusoma na kuandika,Hawakufanya hivi kwasababu ni kazi yao hapana Walifanya hivi ili pia na sisi tujifunze na tuweze kuongea lugha moja! Kama Wangeamua kutuachaaa na Kusema Kuwa Ulimwengu utatufunza Pengine hadi leo kungekuwa na watu hawajui kusoma na kuandikaa licha ya kupitia shule!

Same Applies kwenye Kuongea! Hakuna alie zaliwa anajua kuongea, Lakini kwasasa kila mmoja wetu humu ukimuuliza nani alikufundisha kuongea na kutamka baadhi ya maneno hata sema waulimwengu bali atajisifia na kuwasifia wazazi wake/walezi wake kuwa Hawa ndio walionifundisha mimi kuongea,Baba angu na Mama angu ndio walio nifundisha Kuongea hivyo!

Nirudi kwenye point sasa baada ya mifano hiyo, Iwe mwanaume au mwanamke upo katika ndoa au mahusiano ya kimapenzi usichukulie Matatizo ya Mpenzi wako kama Njia au sababu ya Kumuacha Wala Usichukulie Tabia mbaya zake au vitu vya ajabu anavyo vifanya kama sababu ya kumuacha! Unachoweza kufanya ni Kumvumilia na Kumbadirisha hadi kuwa kama vile ambavyo wewe unataka! Usije Kusema Kuwa Huyu mtu mimi nimemshindwa wengine watanisaidia hapana Huyo mtu Hajakushindwa ila wewe umeshindwa kujua ni njia gani utumie kumbadirisha,Vuta picha mwalimu/mzazi wako angekuacha Akasema Huyu mtoto nimeshindwa kufundisha Kuongea Ungejisikiaje?

Hakuna Kitu kizuri kama Kupita katika Nyakati ngumu na Mpenzi wako na mkatengeneza Historia,Kumuacha Mtu katika Mahusiano Sio Tiba Ya matatizo aliyo nayo mpenzi wako,Kaa naye chini Mfundishe,muelekeze,muelimishe na kumuelewesha kumbuka katika kumbadirish hadi kuja kuwa kama vile unavyotaka awe kuna watu wa aina tofauti tafauti kuna slow learner,kuna wale wanaelewa haraka na wale wenye uelewa wa katikati mvumilie hadi awe vile unavyotaka awee

Kinacho tushinda binadamu wengi ni Uvumilivu lakini ukiona Uvumilivu unakushinda basi jikumbushe hio mifano miwili ya Mwalimu na Mzazi Wako! Usije Sema Atafundishwa na waulimwengu kumbuka waulimwengu wanao Zungumziwa Ni pamoja Na Wewe! Kama unaona Mmeo/mkeo hakufikishi kileleni Basi Take a Time Kumfundisha Hadi akufikishe kileleni kumbuka kila kitu kinawezekana, Kama Hutaki awe na Michepuko basi Kaa chini ongea nae hadi abarike na kuacha Tabia ya Kuchepuka Kumbuka Hiyo tabia Hakuzaliwa nayooo! Achana Na Misemo ya Watu walioshindwa ya kusema huyuu hii Tabia Yake ipo kwenye Damu kumbuka Kuna Magonjwa yapo kwenye Damu lakini watu wanayatibu na Maisha yanaendelea

Jiulize Kama Nitamuacha Huyu mpenzi wangu kisa Nimemkamata na Sms za Ajabu kwenye Simu yake! Je ukipata Wachumba 12 wenye tabia kama hizo utakuwa Wapi wewe utakuwa ni wa kuacha Tuu??? Hapana Unahitaji kutenga Mda wako kumuelimisha na kumbadirisha hadi kuwa vile ambavyo wewe unataka!

Kamwe Usije Kuanzisha Mahusiano na Mtu ambae hujampenda kabisa hata Alie na Kusagana Meno usilazimishe moyo kuanza naye mahusiano utajaza tuu list ya watu uliokuwa nao kwenye uhusiano na hii ndio itakuwa sababu ya wewe kutoweza kumvumilia na kumbadirisha

Unamkuta mtu anasema Aah huyu Nimemuonea huruma kwenye mahusiano hakuna Neno Huruma ila Moyo ndio unao Fanya kazi! Wakija Watu 20 wanao lia kwa uwezo sawa wote utatembea nao Kisa Huruma imekuingia?

Tubadirike Wanadamu na Tuache kutumia Matatizo ya mtu kama sababu ya Kumuacha! Kaeni kwa pamoja mvuke kwenye matatizo kwa pamoja

Danya
 

mbalizi1

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
14,619
2,000
Hakuna jambo tamu kama kuvuka vikwazo, mitifuano na matatizo ya ndoa hadi mkafika uzeeni raha saaana
 

Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
4,328
2,000
Mwanaume anaejielewa ana uwezo wa kumbadilisha mwanamke mbka akawa boraa,, kuwa STRONG tu dem hakusumbui


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom