Matatizo yanayoikuta computer, pamoja na suluhisho lake.

bigimoney

Member
Sep 6, 2017
14
15
6. KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA (MOTHER BOARD)
Ubao Mama(Motherboard), hii ni Saketi ambayo ina muunganiko wa “chip” Zaidi ya moja. Inaitwa Saketi kwa sababu inatumia umeme wa moja kwa moja (Direct Current).
Kwanini uitwe Ubao mama(Motherboard)? Kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuweza ku-programu(programing). Ina uwezo mkubwa wa kutoa kitu toka kwenye “electronic” kwenda kwenye “electronic software”.
Kwa kawaida Ubao mama unapatikana kwenye Kompyuta hapa nikiwa na maana kwenye Simu, radio, Tv, Laptop, Desktop, Mackbook n.k., maana hivi vyote viko kwenye mfumo mzima wa Kompyuta.
Lakini sisi kwa leo tutajikita kwenye Ubao mama (motherboard) kwenye Laptop pamoja na Desktop.
DALILI za kuharibika kwa ubao mama, hii ni hali ambayo hutokea ambapo Kompyuta ilikuwa inawaka lakini ghafla Kompyuta huzima na kuacha kuwaka kabisa.

SABABU(VISABABISHI) ZA KUHARIBIKA UBAO MAMA.
1. Kuchemka/ kupata joto jingi kwa Kompyuta, jambo ambalo husababishwa na Kushindwa kufanya kazi kwa feni(fan).
2. Kumwagiwa kimiminika(liquid), kwenye Kompyuta, pale Kompyuta inapomwagiwa vitu kama chai, soda, maji, uji, n.k huweza kusababisha kuharibika kwa motherboard.
3. Kuwepo kwa uchafu, moshi, kwenye Ubao mama(motherboard), kama Kompyuta haifanyiwi usafi pia inaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa ubao mama.
4. Kuanguka kwa Kompyuta, kuvunjika.
5. Umeme kuzidi kwenye Kompyuta.
6. Kutumika kwa Muda mrefu(kuzeeka).

JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI LA KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA(MOTHERBOARD).
1. Utatuzi wa Shida(troubleshooting),
(i) Angalia kama kuna “signal” zinazoonesha kama umeme unaingia kwenye Motherboard, hapa angalia kwenye “Power jeck” kama umeme unaingia kwenye motherboard.
(ii) Pima “component” mbalimbali zinazounda mfumo mzima wa ubao mama, moja baada ya nyingine kwa kutumia kifaa kinachoitwa “Multimeter, ukigundua “component” ambayo ni mbovu waweza kuibadilisha.
Kabla ya kuibadilisha hiyo “Component” yafaa ukaangalia vitu vifuatavyo;
- Uthamani/ufanano wa “component” unazotaka kubadilisha.
- Utendaji wa kazi wa “component” hiyo.
(iii) Kuibadilisha “component” hiyo. Hapa utaamua kuibadilisha component hiyo kwa kuweka “component” nyingine ambayo ni nzima kama ilivyokuwa mwanzoni.
(iv) Fanya usafi kwenye Ubao mama(Motherboard) pamoja na Kompyuta nzima kwa ujumla.
(v) Washa Kompyuta yako.
2. Kubadilisha Ubao Mama (Ubao Mama), wakati mwingine Unaweza ukabadilisha “Component” lakini bado tatizo likabaki palepale au ukakosa “component” za kubadilisha kwenye ubao mama na zile zilizoharibika, hivyo lazima ubadilishe ubao mama huo kuendana na “MODEL” ya hiyo Kompyuta yako.
TAHADHARI: Usithubutu kufungua kama wewe sio “technician”/fundi maana unaweza kusababisha matatizo mengine pia.

Karibuni sana kwa maoni na Ushauri, pia uwapo na tatizo lolote la Kompyuta usisite kututafuta. ASANTENI SANA.
Cataux Computers
P.o. Box 12598, Mwenge, Dar es Salaam, Tanzani
Contacts:0714003752
0682566622
0764074688
Tembelea Ukurasa wetu, kujifunza zaidi. (Facebook Page):Connectez-vous ou inscrivez-vous pour voir le contenu
 
Mi laptop yangu sometime nikiiwasha inashindwa kustart window inaandika non system harddisk problem
Shida inaweza kuwa nini
 
Mkuu HDD imeanza mafekeche ilo ni tatz jipange uende kwa technician unaemuani akaichek la sivyo io system itacorrupt anytime
 
Mi nina laptop ya sony vaio E series haiingizi charge kwa battery. Plugged in charging kwa 6% ila haiendelei kujaza zaidi?
 
Hapo kwanza jaribu kucharge kwa adapter nyingine, ukiona tatizo linaendelea hapo jua Battery imeharibika, badilisha Battery
 
Dah inabidi niangalie hilo la battery adaptor ninazo mbili OG, haina shida,soon nakupa feedback!
 
Mkuu mm tatizo ni upande wa cm sometimes inaambia processor stopped
Shida nn hapo ???
 
Hapo kwanza jaribu kucharge kwa adapter nyingine, ukiona tatizo linaendelea hapo jua Battery imeharibika, badilisha Battery

MNA uzoefu wa ku rekebisha power system kwenye laptop!!
I mean, adapter nzima. Battery nzima.
Tatizo laptop haipitishi umeme, whether ukiweka battery ama ukitoa.
Ikitokea inapitisha basi inapitisha chaap, then inakata, tena chaap then inakata tena. Inaenda hivohivo.
Mnaweza kusovle???
Nilipeleka kwa fundi akasema RAM inapiga short, tukabadili lakin wapi.
 
6. KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA (MOTHER BOARD)
Ubao Mama(Motherboard), hii ni Saketi ambayo ina muunganiko wa “chip” Zaidi ya moja. Inaitwa Saketi kwa sababu inatumia umeme wa moja kwa moja (Direct Current).
Kwanini uitwe Ubao mama(Motherboard)? Kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuweza ku-programu(programing). Ina uwezo mkubwa wa kutoa kitu toka kwenye “electronic” kwenda kwenye “electronic software”.
Kwa kawaida Ubao mama unapatikana kwenye Kompyuta hapa nikiwa na maana kwenye Simu, radio, Tv, Laptop, Desktop, Mackbook n.k., maana hivi vyote viko kwenye mfumo mzima wa Kompyuta.
Lakini sisi kwa leo tutajikita kwenye Ubao mama (motherboard) kwenye Laptop pamoja na Desktop.
DALILI za kuharibika kwa ubao mama, hii ni hali ambayo hutokea ambapo Kompyuta ilikuwa inawaka lakini ghafla Kompyuta huzima na kuacha kuwaka kabisa.
SABABU(VISABABISHI) ZA KUHARIBIKA UBAO MAMA.
1. Kuchemka/ kupata joto jingi kwa Kompyuta, jambo ambalo husababishwa na Kushindwa kufanya kazi kwa feni(fan).
2. Kumwagiwa kimiminika(liquid), kwenye Kompyuta, pale Kompyuta inapomwagiwa vitu kama chai, soda, maji, uji, n.k huweza kusababisha kuharibika kwa motherboard.
3. Kuwepo kwa uchafu, moshi, kwenye Ubao mama(motherboard), kama Kompyuta haifanyiwi usafi pia inaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa ubao mama.
4. Kuanguka kwa Kompyuta, kuvunjika.
5. Umeme kuzidi kwenye Kompyuta.
6. Kutumika kwa Muda mrefu(kuzeeka).
JINSI YA KUTATUA TATIZO HILI LA KUHARIBIKA KWA UBAO MAMA(MOTHERBOARD).
1. Utatuzi wa Shida(troubleshooting),
(i) Angalia kama kuna “signal” zinazoonesha kama umeme unaingia kwenye Motherboard, hapa angalia kwenye “Power jeck” kama umeme unaingia kwenye motherboard.
(ii) Pima “component” mbalimbali zinazounda mfumo mzima wa ubao mama, moja baada ya nyingine kwa kutumia kifaa kinachoitwa “Multimeter, ukigundua “component” ambayo ni mbovu waweza kuibadilisha.
Kabla ya kuibadilisha hiyo “Component” yafaa ukaangalia vitu vifuatavyo;
- Uthamani/ufanano wa “component” unazotaka kubadilisha.
- Utendaji wa kazi wa “component” hiyo.
(iii) Kuibadilisha “component” hiyo. Hapa utaamua kuibadilisha component hiyo kwa kuweka “component” nyingine ambayo ni nzima kama ilivyokuwa mwanzoni.
(iv) Fanya usafi kwenye Ubao mama(Motherboard) pamoja na Kompyuta nzima kwa ujumla.
(v) Washa Kompyuta yako.
2. Kubadilisha Ubao Mama (Ubao Mama), wakati mwingine Unaweza ukabadilisha “Component” lakini bado tatizo likabaki palepale au ukakosa “component” za kubadilisha kwenye ubao mama na zile zilizoharibika, hivyo lazima ubadilishe ubao mama huo kuendana na “MODEL” ya hiyo Kompyuta yako.
TAHADHARI: Usithubutu kufungua kama wewe sio “technician”/fundi maana unaweza kusababisha matatizo mengine pia.
Karibuni sana kwa maoni na Ushauri, pia uwapo na tatizo lolote la Kompyuta usisite kututafuta. ASANTENI SANA. Cataux Computers P.o. Box 12598, Mwenge, Dar es Salaam, Tanzani Contacts:0714003752 0682566622 0764074688 Tembelea Ukurasa wetu, kujifunza zaidi. (Facebook Page):Connectez-vous ou inscrivez-vous pour voir le contenu
computer inapiga beeping alarm zanjano mfurulizo
 
Back
Top Bottom