Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
CHANGAMOTO ya UGONJWA wa FIGO..jpg

Ugonjwa wa figo
Figo ni ogani inayoshirikiana na moyo. Kuathirika kwake kuna athari kubwa kwa mfumo wa damu na mapigo ya moyo.
Magonjwa sugu ya figo hutokea pale ogani hiyo inapopoteza uwezo wa kutenda kazi zake kikamilifu.

Tatizo huanza taratibu na kudumu kwa muda mrefu hadi kuonyesha dalili za wazi .

Huu ni kati ya magonjwa yasiyoambukiza kwani unatokana na mienendo na mitindo ya kimaisha .

Figo huwa na kazi ya kuchuja takamwili zilizo ndani mwilini na kuzitoa nje kwa njia ya mkojo na kupunguza kiasi cha maji kilichozidi mwilini.

Figo hutoa homoni inayochochea ogani zingine mwilini ikiwamo kuhamasisha utengenezwaji wa chembe nyekundu za damu,utendaji wa madini ya kalsiamu na homoni zinazoongeza mwendo kasi wa misuli ya moyo.

Vilevile ,figo hufanya kazi ya kufyonza na kuvirudisha vitu muhimu ambavyo vingehitajika kutoka kwa njia ya mkojo.

Hudhibiti madini kama potasiumu,magnesiumu,na tindikali ili kuweka sawa mazingira sawia katika damu.

Figo inapopoteza uwezo wake wa kutenda kazi husababisha kukosekana kwa ufanisi wa shughuli za mwili. Hali hii husababisha kuwapo kwa kusanyiko na limbikizo la maji, uchafu na sumu hutokea mwilini mwa mgonjwa.

Pia husababisha kutokea kwa maradhi mengine kama vile, upungufu wa damu mwilini, shinikizo la damu na ongezeko la tindikali kwenye damu. Vilevile husababisha ongezeko la lehemu na mafuta kwenye damu na magonjwa ya mifupa.

Inaelezwa kuwa karibu watu nusu milioni wapo katika uchujaji damu na mashine mbadala wa figo ( dialysis ) na huku wakiwa wameshawahi kubadilishiwa figo.

Mambo kadhaa yanahusishwa na tatizo la ugonjwa sugu wa figo ikiwamo ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu,unene uliopitiliza na uzee.

Vilevile mabadiliko katika tabia na namna watu wanavyohishi.
Ili kujiepusha na hatari ya kupata ugonjwa wa figo fanya yafuatayo.

1. usichelewe kwenda haja
Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya.kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.

Pia mkojo unaporudi nyuma ya njia husababisha maambukizi katika figo pia njia ya mkojo "nephritis", pamoja na "uremia".
Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya haraka iwezekanavyo nenda kakojoe .

2. kula chumvi kupita kiasi nalo ni tatizo
Inatupasa kula chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku .

3. kula nyama kupita kiasi.
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.

4.unywaji mwingi wa "caffeines"
Caffeine hutokana na vinywaji vya soda na vinywaji vingine laini kama kahawa, red bull n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza kupata mateso .
Unapaswa kupunguza kiwango cha coke, pepsi, red bull, nk. Ambavyo hunywa kila siku.

5.pia kutokunywa maji
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri .endapo hatunywi maji ya kutosha , sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu ,kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo . Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.

Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha nayo ni kuangalia rangi ya mkojo wako,wepesi wa rangi ndiyo vizuri.

6.pia kuchelewa matibabu

Pia epuka vidonge hivi ni hatari sana:-
D- baridi.
Vicks action- 500
Actified
Coldarin
Cosome
Nice
Nimulid
Cetrizet- d
Hivi vidonge vina phenyl propanol- amide ppa ambayo husababisha stroke na zimepigwa marufuku huko marekani.

Namalizia kwa kukupatia maonyo muhimu ya afya.

1. Jibu (pokea) simu wito na sikio la kushoto.
2. Usinywe dawa kwa maji baridi.
3. Usile milo mizito baada ya saa kumi na moja jioni .
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku . Usinywe maji baridi kamwe .
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo wa usiku, kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji kwani wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
 
SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO. JIHADHARI NA ONYEKA!.

Raia wa Ghana wanazidi kufa kwa matokeo ya ugonjwa wa Figo.

JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:

1.Usichelewe kwenda haja

Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya.
Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu.
Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo,
pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.

2. Kula Chumvi kupita kiasi. Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.

3. Kula nyama kupita kiasi
.
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako.
Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.

4. Unywaji mwingi wa "Caffeins".
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k.
Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso.
Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.

5. Kutokunywa maji.
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri
Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu,
kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo.
* Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku. Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha
Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.

6. Kuchelewa matibabu.
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara
Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe... Shirikisha wengine, kama unajali.

----------------
Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:
D- baridi
Vicks Action- 500
Actified
Coldarin
Cosome
Nice
Nimulid
Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.
MWISHO... Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
Inaweza kumsaidia mtu!
Wasambazie wengi kwa kadiri uwezavyo.
Shirikisha ujumbe huu kwa mpendwa wako.

Maonyo muhimu ya Afya
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio la kushoto.
2. Usinywe dawa zako kwa maji baridi....
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni.
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako....!!.

NB:Hotoweza tena maishani mwako " kula tunda la mti wa kati" ambalo infact ni tamu kuliko asali hasa pale unapokaribia kilele cha kilimanjaro
 
"Kula Chumvi kupita kiasi. Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku"

Gram 5.8 kwa vijiko vya chai ni kama vingapi?au kiasi gani katika kijiko?
 
"Kula Chumvi kupita kiasi. Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku"

Gram 5.8 kwa vijiko vya chai ni kama vingapi?au kiasi gani katika kijiko?
Jumvi siyo tishio kivile wataalamu wanadai Unaweza kuidilute kwa kunywa Maji mengi sanaaaa. Sukari ndio noma huwezi kuidilute
 
Jumvi siyo tishio kivile wataalamu wanadai Unaweza kuidilute kwa kunywa Maji mengi sanaaaa. Sukari ndio noma huwezi kuidilute
Napenda Soda sana naweka na ice, lakini vyakula vyenye sukari nyingi sipendi kama Cake, Biscuit, Candy, hata juice ikiwa na Sukari nyingi siiwezi.
 
Mkuu soda ndio hatari hasa zero sugar zote ni hatari. Vitu Salama ni bangi na Maji baas Zina boost body immune system nakukufanya uishi maisha marefu yenye furaha
ndio maana watoto wa KISIMIRI SEKONDARI wanaongoza kitaifa, asante
 
ndio maana watoto wa KISIMIRI SEKONDARI wanaongoza kitaifa, asante
Watu hawajui tu. Ukivuta bangi kiustaarabu na mpangilio huwezi kupata Magonjwa ya kujitakia kama Figo kufeli. Elon musk anapiga hii cha Arusha ona from nowhere anafanya Vitu vya ajabu hadi Sasa hivi Tajiri namna nne duniani.

Kwenye Figo renal artery, Renal vein na Ureter zikipata mushkel umekwisha. Sasa hapo Marijuana inasaidia
 
Jumvi siyo tishio kivile wataalamu wanadai Unaweza kuidilute kwa kunywa Maji mengi sanaaaa. Sukari ndio noma huwezi kuidilute
Aisee kumbe, kwanza mpaka nile kijiko kizima na ushee cha chumvi kwa siku nitakuwa nakula kitu gani labda kulamba
 
Kuna vitu hujavieleza.

mfano wanywaji wa pombe kali,

uhusiano wa kisukali ugonjwa wa figo na presha.

unywaji mkubwa wa asali na madhara yake.
 
5.8 grams equals to 1.16 teaspoons or there are 1.16 teaspoons in 5.8 grams
....Kwa maana kwamba jumla ya Chumvi yote unayokula kupitia vyakula mbali mbali kwa Siku Moja Isizidi kijiko kimoja na robo cha Chai?? Ngumu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom