Elections 2010 Matatizo yaliyopo katika majina ya wapiga kura vituoni

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Kumekuwa na malalamiko kwa wanachi sehemu mbalimbali juu ya kutoyaona majina yao toka katika vituo walivyojiandikishia ambayo yamebandikwa katika vituo vya kupigia kura.

Kwa mtazamo wangu kuna masuala yafuatayo yaliyo au yanayochangia matatizo kama hayo kutokea.

Tatizo la kwanza ni uzembe wa NEC ulosababisha baadhi ya majina yaliyoandikishwa kituo X jimbo hili yakaondolewa na kuwekwa kituo Y mkoa au jimbo lingine kabisa, kama ilivyotokea huko Tunduma. Tatizo la Pili ni la nia njema kabisa, na hili limefanywa na NEC kwa lengo la kupunguza msongamano usio wa lazima. Walichofanya hapa ni kupunguza majina toka kituo kimoja na kuyapeleka katika kituo kilichokaribu kwa au kwa kuweka kituo kipyaa kabisa kwa lengo la kufanya kituo kimoja kisizidiwe saana na idadi ya watu wakati kingine hakina watu wengi. Tatizo la Tatu ni la uzembe wa watendaji ambao wameyabandika makaratasi ya majina hayo kwa kutumia gundi feki zinazobanduka haraka na kusababisha karatasi kudondoka chini na kupeperushwa na upepo, katika hili pia kuna uzembe wa kutokuwepo na mtu wa kuzilinda hizi karatasi ili kusifanyike anykind of Vandalism. Kuyabandika tu na kuondoka, hakumzuii mzembe mmoja mwenye lengo baya kwenda kuzibandua na kuondoka nazo na kusababisha wengi wasiweze kuyaona majina yao.

OMBI LANGU:
Kwa wapiga kura, kama unaweza tembelea kwanza website ya NEC (The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage), hapo utaweza hakikisha kama jina lako lipo au halipo kwa kuandika namba ya kadi yako ya mpiga kura na detailed information zako zitaonekana ikionyesha jina lako, kituo ulichojiandikisha, jimbo, mkoa na kata. Hii itakufanya uwe na uhakika kuwa jina lako lipo

Kwa NEC, mtujulishe mapema wananchi iwapo mmefanya mabadiriko yoyote katika vituo na majina yetu kama ambavyo imeshatokea. Na kwa NEC pia ningewaomba kutoa uamuzi haraka saana, kwa mtu/watu ambao wanakadi, ila majina hayapo vituoni japo kwenye mtandao wenu yanaonekana yapo.
 
Piga namba ya simu ifuatayo ili kuuliza maswali mbali mbali yahusuyo uchaguzi 0222199780
 
Back
Top Bottom