Matatizo ya watanzania ni zaidi ya uchaguzi mkuu wa 2015,tujikite kwenye kujenga uchumi


sammosses

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,342
Points
1,500
sammosses

sammosses

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,342 1,500
Matatizo ya Watanzania si Ikulu kwa sasa wala uchaguzi wa 2015 kama makundi mengi yanavyo jaribu kujenga basement hivi sasa kwa uchaguzi ambao bado miaka zaidi ya miwili ili kuufikia.Viongozi wa serikali nao wamejikita zaidi kwenye presidential rally kuliko kutatua matatizo yanayo ikabili nchi.

Kila anayesimama yupo nyuma ya mwamvuli wa uchaguzi wa 2015.Cha ajabu na kweli hata CCM ambao wapo madarakani nao pia wana waza uchaguzi ujao na kuweka mikakati ya kushinda ilihali hawajatekeleza ahadi za uchaguzi uliopita.

Mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema hadharani kuwa Ikulu si mahali pa mchezo kila mmoja anawaza kupakimbilia.Kuna biashara gani ikulu inayowafanya watu kuwa maadui ilhali nyumba yao ni moja.Kila waziri anayetekeleza wajibu wake naye pia yupo kwenye kundi fulani lenye ndoto za kuingia Ikulu,kwa hali hii nchi kweli itasonga mbele!

Watanzania hawakuzoea kukaa kimkakati na kutekeleza majukumu yao kwa kuwaza nafasi za juu kabisa ndani ya taifa hili ilihai madaraka waliyo nayo yana wapwaya.

Tukiacha mawazo ya uchaguzi wa 2015 taifa letu litasonga mbele na wananchi ndiyo watakao kuwa waamuzi kwa yale ambayo serikali imeyafanya.Si busara serikali kuzinadi barabara ilihali kuna mambo jungu nzima ambayo ni changamoto ambazo serikali ilitolea ahadi kuzitatua kwenye uchaguzi uliopita lakini zimebaki kwenye makabrasha.

Kwa serikali inayo kusanya kodi zaidi ya bilioni 800 kwa mwezi tulitegemea mengi zaidi ya barabara.Waalimu wanataabika kutokulipwa stahiki zao,mishahara haitoki kwa wakati,shule hazina miundo mbinu ya kufundishia,mahospitali hayana dawa lakini rais na timu yake hawaoni zaidi ya barabara.

Sisi ndiyo waamuzi tunaona kama kweli kuna haki ya kuirudisha serikali ya CCM baada ya uongozi wake wa miaka zaidi ya 50 au la.Watanzania wana akili timamu za kujitambua zaidi kuliko kunadi vitu ambavyo kwao havina tija wala mashiko.

Tunataka kuona barabara zinazo nadiwa zina leta tija katika kufufua uchumi wetu na kuwa kishawishi cha serikali kuweza kuwapatia wakulima soko bora la mazao yao.Soko la mazao likiwa zuri barabara zitakuwa na tija.Elimu ikiwa ni bora barabara zitakuwa na tija,lakini kuzinadi barabara kama njia kuu ya kukuza uchumi wakati wananchi hawana kitu mfukoni mwao ni sawa na kuwatukana Watanzania.Barabara nzuri ziendane na uchumi bora kwa kila Mtanzania,hapo ndipo haki itaonekana ikitendeka.

Tanzania yetu itajengwa kweli na watu wenye moyo safi na wenye dhamira ya kweli kwa Watanzania wenzao na kugawa mali zetu kwa wageni,hizo ni sawa na akili za shetani.
 

Forum statistics

Threads 1,294,754
Members 498,027
Posts 31,187,127
Top