Matatizo ya wanafunzi China-Msolla ajiuzulu?

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Mapema leo asubuhi nimetumiwa e mail na wanafunzi wa kitanzania wanaosoma kule nchini china wakiwa na matatizo ya kutokupelekewa pesa na bodi ya mikopo tangu mwezi wa saba.

naiweka hapa e mail yao ili kuweza kuwatetea hawa watanzania wenzetu yasije yakawakuta yale yale ya vijana wetu walioko Ukraine.

Nina njia za kuweza kuwasiliana nao kwa ajili ya kupata details zaidi.

Msolla sasa yafaa ajiuzulu ama rais amwondoe kwani anaangamiza vijana wetu na kuwalazimisha kuwa ombaomba huko waliko.


MATATIZO Y WANAFUNZI CHINA TAREHE 12.11.2007
SISI NI BAADHI YA WANAFUNZI TULIO CHINI YA UDHAMINI WA SERIKALI YA TANZANIA,TUNASIKITIKA KWAMBA MPAKA SASA HATUJAPATA MKOPO TOKA BODI YA MIKOPO HALI INAYOFANYA TUISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU YA KULA MLO MMOJA KWA SIKU,KUSHINDWA KUINGIA DARASANI KWA KUKOSA VITABU,KUSHINDWA KUFANYA MAJARIBIO SABABU YA KUKOSA VIFAA MUHIMU.
TULIJAZA FOMU ZA MKOPO TOKA MWEZI WA SABA NA KUZITUMA UBALOZINI KAMA ULIVYO UTARATIBU TULIOELEKEZWA WA KUJAZA FOMU NA KUZITUMA UBALOZINI .
CHA AJABU FEDHA ZILIPOKUJA ZILIKUJA ZA WANAFUNZI BAADHI HUKU WENGINE WAKIAMBIWA KUSUBIRI KWAMBA FEDHA ZITAKUJA.TUMESUBIRI NA KILA TUKIPIGA UBALOZINI TUNAAMBIWA TUSUBIRI.
TUMEVUMILIA HALI HIYO MPAKA SASA WANAFUNZI AMBAO HATUJAPA FEDHA TUPO 14(KUMI NA NNE)KATIKA VYUO VIFUATAVYO,
1.shandong university WANAFUNZI 3
2.SOUTH CHINA UNIVERSITY OF TECHNOLOGY ,WANAFUNZI 5
3.WUHANI UNIVERSITY OF TECHNOLOGY 4
4.BEIJING UNIVERSITY 2
HALI HII IMETUFANYA KUSHUKA KIMASOMO KWANI TUNASOMA KWA LUGHA YA KICHINA NA SI KIINGEREZA.KAMA LUGHA ILIVYO NGUMU TUNAPOKOSA VITABU NA NJAA,HALI INAKUWA NGUMU.
WENZENTU WALIO SOUTH CHINA UNIVERSITY OF TECHNOLOGY WAKIPIGA SIMU HUAMBIWA WAFUATILIE WAO WENYEWE TANZANIA,HALI KWAMBA WAO WANAONA NI KINYUME NA UTARATIBU UTARATIBU WA KIKAZI
MPAKA SASA NI MWEZI WA 11 TOKA MWEZI WA SABA NA MAISHA TUNAYOISHI NI MUNGU NDIYE ANAYEJUA.
TUNAMUOMBA WAZIRI HUSIKA ,WAZIRI MKUU NA RAISI KUINGILIA KATI ILI KUTUNUSURU KWANI TUNAELEKEA KUFANYA MITIHANI YA KUFUNGA MUHULA ITAKAYOANZA MWEZI DESEMBA BILKI VITABU NA FEDHA ZA KULA HAMNA,TUNAOMBA SERIKAILI KUTUNUSURU NA HALI HII KWANI NI MBAYA MNO.
KATIKA HAO KUMI KUNA TAARIFA ZISIZO RASIMI KWAMBA KUNA FEDHA YA WANAFUNZI NANAE ZIMEFIKA WIKI MOJA ILIYOPITA ,CHA AJABU MBAKA SASA HAIJAWAFIKIA WAKATI HUO HUO WANAFUNZI WALIO CHUO CHA SOUTH CHINA UNIVERSITY HAUJULIKANI ZITAFIKA LINI;
KWA KWELI TUNAANGAMIA.ubalozi unatwambia tuvumilie mpaka hapo frdha itakapofika na tuwawaeleza kutusaidia wa fedha kidogo ya chakula wanadai ubalozi hauna hela.Sasa tunashindwa kuelewa tusubiri na njaa bila kuelewa fedha itafika lini
WANAFUNZI CHINA.
nb,tunaogopa kutaja majina
 
Very serious.

Sasa hizo zilifika tayari zimekwama wapi? Ubalozini? Nadhani kutakuwa na urasimu fulani somewhere.
Msolla inaelekea amekata tamaa, mzigo mzito.
 
waambie warudi nyumbani,wakapate neema huko.kwa kifupi tu sasa tunachuo kukubwa kulikovyote barani afrika cha dodoma.msolwa anasema nafasi ni za kulala hakuna shida.
 
MUUNGWANA akishavunja BARAZA LA MAWAZIRI,next itakuwa BODI LA MIKOPO.mwaka huu kazi kweli kweli.

Saharavoice..........

zimebakia siku ngapi 2007 imalizike?
 
wafanyakazi wa BODI YA MIKOPO mbali na kulipwa mishahara mikubwa (ofisa mdogo analipwa zaidi ya 1.5M kwa mwezi) lakini hakuna wanacho-deliver. Nafikiri kuna tatizo la watu wanaoajiliwa kama sio watoto wa vigogo ambao wanabebwa kama kawaida kwenye kazi zenye mshahara mkubwa serikalini basi bosi wao MSOLLA ndo ana tatizo. Hivi kwanini MSOLLA hasijiuzulu kwa heshima tu.
 
Labda ni seme kidogo hapa,tutawalaumu watu wa badi wee bila mafanikio,bodi kama bodi haina matatizo tatizo lipo hazina ambapo pesa zinatoka,kinachofanyika ni bodi kuficha siri na kukubali kubeba lawama.
Serikali yetu haina pesa huwa inategemea makusanyo ya mwezi ili kuzigawa kutokana na mahitaji ya wizara na kuangalia kipaumbele kwa taifa.wanafunzi sio muhimu hivyo wanaweza kusubiri.
Ndio maana hakuna mtu yeyote uliyewahi kusikia kahadhibiwa kwa kuchelewesha malipo kwa wanafunzi wawe wa ndani au nje ya nchi.
 
Katibu Tarafa, pesa zipo na zinatumwa ila zikienda kulipiwa wanafunzi zinakatwa, kuna racketing ya ajabu sana. Mwanafunzi anapata chuo nje, anaenda kupata pesa ya nauli (tiketi dola 1000, anakopeshwa 1500 - 500 inabakia kwa afisa). Halafu akienda kule masomoni, pesa inatumwa kupitia Ubalozi, Balozi wanatuma ofisa wao anaenda kule anawapelekea pesa kidogo kwa ahadi zilizosalia ziko njiani (wakati zilishafika)... basi zinamegwa na zinarudishwa kwa watu wao, wanasubiri mgao mpya kulipia deni la zamani na mzunguo unaendelea hivyo hivyo... this is true in Ukraine, China, Urusi, India, Cuba na in the past hata Poland
 
No wonder wakaambiwa walijipeleka wenyewe huko china.
Tuliwaambia hatuna hela wakaamua kwenda huko Kujilipia wenyewe.

Yale yale ya UKRAINE!
 
No wonder wakaambiwa walijipeleka wenyewe huko china.
Tuliwaambia hatuna hela wakaamua kwenda huko Kujilipia wenyewe.

Yale yale ya UKRAINE!


sasa wataambiwa hivyo wakishatokea hadharani hivyo bodi itawang'aka..
 
Katibu Tarafa, pesa zipo na zinatumwa ila zikienda kulipiwa wanafunzi zinakatwa, kuna racketing ya ajabu sana. Mwanafunzi anapata chuo nje, anaenda kupata pesa ya nauli (tiketi dola 1000, anakopeshwa 1500 - 500 inabakia kwa afisa). Halafu akienda kule masomoni, pesa inatumwa kupitia Ubalozi, Balozi wanatuma ofisa wao anaenda kule anawapelekea pesa kidogo kwa ahadi zilizosalia ziko njiani (wakati zilishafika)... basi zinamegwa na zinarudishwa kwa watu wao, wanasubiri mgao mpya kulipia deni la zamani na mzunguo unaendelea hivyo hivyo... this is true in Ukraine, China, Urusi, India, Cuba na in the past hata Poland

Mwanakijiji,
Huku India ni aibu.Kama mwezi uliopita waliwatumia wanafunzi hela za chakula na stationary halafu hawakutuma accomodation hadi ubalozi ulipowaandikia barua tena kuwaambia mbona hamkutuma accomodation za hawa wanafunzi? Hadi leo wanasema wanalishughulikia.

Cha ajabu kuna wanafunzi wa chuo kingine hawakuletewa hela kabisa huku bodi ikidai hawakupata form za wanafunzi hao yaani eti ziliyeyuka katika mazingira ya kutatanisha.

Aibu kubwa kuliko zote ni kwamba hata fedha za field hawakutuma huku wakijua ni for partial fullfillment of the course.Sasa hawa jama huwa wanatake advantage kwa sababu wanafunzi wako mbali na serikali yao hawawezi kutia pressure.
 
Tatizo siyo umbali asikudanganye mtu. Tatizo ni uzembe na ufisadi uliokithiri. Unafikiri wale walio Arusha, Mbeya au Dodoma na wale walio Dar wana umbali gani? Mbona wote wana matatizo hayo hayo na mara zote lawama zinawaangukia wanafunzi! Kuna wakati natamani waniombe niwatengenezee bodi ya mikopo and I promise you within six months hakuna atakayecheleweshewa mikopo au kuwa na mikopo pungufu! It makes no sense unapokuwa na Professa mzima anayeshindwa kufikiri na amebakia kung'ang'ania..
 
Ukiona vitu vitatkavyotupush kwenye siasa ni vitu kama hivi.Nimechoka na hawa Wakoloni weusi wacha na sisi tukapambane nao humo humo ila Mungu atupe nguvu tu.

Inashangaza mtu ukiwapigia hapo wizarani weanavyoongea kwa kiburi kana kwamba wao ndio wenye uwezo wa kupiga parapanda ya Mwisho.


Mkjj,
Hapo Bodi kuna uzembe wa hali ya juu.Ni watu wanaofanya kazi bila kufikiria nje ya box ndio maana hata bajeti ya Wizara hiyo inapwaya kabla mwaka wa fedha hujaisha kwani hawa watu hawawezi kupanga mambo kimkakati hata siku moja.HII BODI INATAKIWA KUVUNJWA hata MSOLLA ni mtu anaetakiwa kujiuzulu
 
Ben, hivi umesoma hotuba ya Msolla ya Bajeti uone kama alisema lolote la msingi kuhusu wanafunzi wanaosoma nje ya nchi.. utashangaa..
 
Nchi hii ndio maana hata madaktari wetu wanapasua watu vichwa badala ya miguu.

Hii inatokana na kuwa na msongo wa mawazo tangu kipindi wanasoma huko nje.

Nchi hii iangalie hawa vijana na jinsi ya kuwasaidia vijana wetu na sio kuwaacha wakiteseka kila kukicha.
 
mpaka kieleweke, wakifanya hivyo watakuwa wanaoongoza, na kuongoza ndio tatizo. Si ulisoma yule afisa wa bodi aliyesema vijana waliokuwa wanafuatilia mikopo Dar "wanaenda kutalii tu".
 
Matusi kwa watanzania ni mengi sana ,kama mtu akiwa anafuatilia tatizo halafu anaambiwa kuwa anakuja kufanya utalii ni matusi yasiyovumilika.

Ama na wale wazee wa jumuiya ya EAC ambao wanadai mafao yao nao wanakwenda kutalii pale wizarani ndio maana wanalala kwenye mahema nini?
 
mpaka kieleweke, wakifanya hivyo watakuwa wanaoongoza, na kuongoza ndio tatizo. Si ulisoma yule afisa wa bodi aliyesema vijana waliokuwa wanafuatilia mikopo Dar "wanaenda kutalii tu".

Hawa watu jamani wana matusi,cha msingi ni kuingia humo humo kupambana nao ili kwa wadogo zetu lisitokee tena.Tumeshakua wahanga na inatosha kuwa sacrifice for the next generation.Chamsingi na sisi hii dhambi ya Mauti ya ufisadi isije ikatuingia na sisi tukakubali.

Muda wa wao kuongoza una kikomo tu na unakaribia.Chamsingi vijana wote wenye mapenzi ya dhati na uzalendo na nchi yetu ambao tumepata elimu chini ya serikali hii kandamizi tuwe tayari kuitumia hii elimu kwa mapambano mapana yenye kuleta ahueni kwa Tanzania ya kesho.

Ben, hivi umesoma hotuba ya Msolla ya Bajeti uone kama alisema lolote la msingi kuhusu wanafunzi wanaosoma nje ya nchi.. utashangaa..

Mkjj,

Hakuna la maana mkuu wangu tena ni kama vile nchi haina watua ambao inawahudumia nje ya nchi kama wanafunzi.Na idadi ya wanafunzi walioko nje ya nchi chini y a bodi inajkaribia au inazidi 500.Tutapambana nao hadi tone la mwisho
 
So Msolla anapaswa kuondoka kwa kipindi hiki.

Hapaswi kuendelea kuwepo kwa mateso ya vijana wetu huko nje.
 
Hapa watu wanakuna vichwa kujaribu kutafuta solution huku huku ugenini ambayo haitaliaharibia sifa taifa letu ingawa serikali kwa hili imedhamiria kuwadhalilisha wanafunzi.

Kura hata za wazazi wetu na ndugu na jamaa 2010 watazisikilizia kwenye bomba.mAANAKE KAMA MIMI NI KUWASHAWISHI NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KADIRI NIWEZAVYO KUHAKIKISHA HAWAPATI KURA ZAO.nINAAAMINI NA WENGINE WENGI WATAFANYA HIVYO
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom