Matatizo ya wakulima hayatamalizwa na wataalam wa ugani peke yao.

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Nimesikliza matamshi ya viongozi wa serikali wengi kuhusiana na kilimo.Wengi kama sio wote wanaelekea aidha kutoelewa matatizo yanayoikumba sekta ya kilimo au kuyafumbia macho makusudi kwa maslahi yao binafsi au maslahi ya NWO(New World Order).Niseme wazi kwamba kudhani matatizo ya sekta ya kilimo yatamalizwa kwa maafisa ugani kupeleka mbinu bora za kilimo kwa wakulima hata kama wangekuwa na uwezo huo na mbinu hizo zingekuwepo ni kichekesho.Sina haja sana ya kuongelea kwa kirefu matatizo yanayoikumba wizara ya kilimo.Itoshe kuyataja tu kama ifuatavyo na kusema kwamba kama serikali haitachukua hatua za makusudi kabisa za kuyatatua isitegemee kabisa kilimo kuboreka hata kama ingeajiri maafisa ugani milioni kumi!

*Sera kubadilika mara kwa mara inasababisha kukosa "continuity" katika
utendaji mzima wa Wizara ya Kilimo.

*Serikali yenyewe kutothamini kilimo huwafanya watendaji wa sekta
hiyo kukosa "morale" ya kujituma.

*Miundombinu hasa barabara za vijijini ambazo ndizo zinazotumika
kusafirishia mazao kupeleka kwenye masoko bado, ni kitendawili.Kujenga
masoko tu kama mazao hayawezi kufika huko sio suluhu."This is a very
cosmetic gesture."

*Bei za mazao kwa wakulima bado ni ndogo sana ikilinganishwa na kile
wafanyibiashara wanachopata.Kuna wizi wa kutisha anaofanyiwa
mkulima,wizi ambao unamfanya mkulima aendelee kuwa maskini.Katika
hali hii mkulima anashindwa kabisa ku-reinvest back to the land.Serikali
isimamie vizuri eneo hili ili wakulima wapate stahili yao.

*Maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya kilimo na wafanyakazi wote kwa
ujumla ni duni mno.Mpaka hapo serikali itakapo kuwa 'serious' na
kuliangalia swala hili kwa undani zaidi,isitegemee mchango wa wataalam wa
kilimo kuwa mkubwa.

*Mazingira ya kufanyia kazi ni mabovu mno na vitendea kazi hakuna
kabisa.Serikali isitegemee afisa ugani aliyetoka kwenye nyumba ya
manyasi awe na "output" ya maana,wala isitegemee afisa ugani mwenye
baiskeli atembelee wakulima kwa moyo hasa ukizingatia ubovu wa
barabara zetu na umbali unaohusika. Kama serikali inataka maendeleo
ya kilimo kweli ni lazima iboreshe mazingira ya kufanyia kazi na maslahi
ya wafanyakazi wake.Vinginevyo kitakachoendelea ni ngonjera tu.

*Serikali imesahau kabisa kitengo cha utafiti wa kilimo.Tumesahau kabisa
kwamba utafiti ndio moyo wa taifa lolote.Taifa lisilofanya utafiti wake
lenyewe limekufa.Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia maamuzi
ya kushangaza kabisa ya serikali yetu.Kwamba sasa serikali
itegemee wafadhili katika utafiti wa kilimo.Napenda niweke wazi kwamba
yeyote anayekupa pesa yake ni lazima apate maslahi fulani,na katika hili
naomba kusiwe na ubishi.Maslahi haya yamekuwa kilio kwetu.Miaka
nenda miaka rudi mikakati ipo lakini kilimo kinazidi kudidimia.Naiomba
serikali isitegemee wafanzili katika suala la utafiti wa kilimo."Let us fund
our own agricultural research." Uwezo tunao!Watu hawa wana ajenda za
siri.

*Utendaji wa watendaji wakuu katika sehemu mbali mbali za kazi
umekuwa mbovu mno.Wengi wamekuwa wafujaji wa mali za uma,
kwa hiyo kazi zilizokusudiwa hazifanyiki,kwa vile fedha hutumika katika
malengo ambayo hayakupangwa.Matokeo ni kwamba
wale wafanyakazi wanaokubaliana nao katika uovu wao ndio
wanaosogezwa karibu, na wasiokubaliana nao husogezwa mbali na
kuchukiwa kabisa. Niseme wazi kwamba wale wafanyakazi wanaopenda
'favours" ndio wabovu na wasiokuwa na uwezo kikazi kabisa.Sasa hali hii
hukatisha tamaa wafanyakazi wazuri,na hivyo utendaji kwa ujumla
kuzorota.Kama serikali halitadhibiti utendaji mbovu wa wawatendaji
wake wakuu katika sehemu mbalimbali za kazi,isitegemee miujiza kabisa.


*Pembejeo za kilimo na vitendea kazi kama matrekta vimekuwa ni ghali
mno.Hivi tunategemea mkulima gani wa kawaida aweze kununua mfuko
mmoja wa mbolea ya DAP.( Sh.100,000,Lushoto), Urea(Sh.50,000,
Morogoro) au mbegu ya mahindi Sh.1,200?Naishauri serikali katika hili
itoe ruzuku ya kutosha katika mbolea, mbegu na hata matrekta,ili
kumuwezesha mkulima kumudu gharama za uzalishaji.

*Mvua nazo katika siku hizi za karibuni zimekuwa haziaminiki kabisa.
Serikali haionekani kama iko makini katika suala la uanzishwaji wa miradi
ya umwagiliaji.Ni vema serikali ikalipa suala hili uzito unaostahili ili
kuongeza uzalishaji na hivyo kupunguza umaskini wa wanachi wake
uliokithiri.

NAWAKILISHA.
 
Back
Top Bottom