Matatizo ya Waislam sio ya serikali

Happy nation

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
679
591
Uongozi katika Uislam

Uongozi tunaozungumzia siyo wa kiimani ila kwenye kila msikiti kuna Imam na kuna kamati. Tatizo ni kwenye hizi Kamati, misikiti mingi miaka ya nyuma ilikuwa ikiongozwa na BAKWATA na waliijenga kwa misingi ya ufisadi na kupora mali bila ya kuwashirikisha waislamu wengi.

Na ili waweze kuendelea na huu ufisadi wamekuwa wakibadilisha katiba na kuhakikisha mali yote inasimamiwa na makao makuu na kuamuliwa na wachache bila ya kushirikisha waumini mikoani. Hii ilipelekea kuundwa kwa kamati za watu wenye dhiki na kufanya wenye uwezo wa kifedha waache kuchangia na kukaa mbali na BAKWATA.

Hivi sasa misikiti inayojengwa kwa kasi ni ya madhehebu ya Salafi(Ansar Sunna). Misikiti hii hujengwa na waumini au wafadhili kama Islamic Foundation. Tatizo liko palepale, wanaosimamia kama kamati ya hizi misikiti ni kama mfumo wa BAKWATA. Wanaosimamia au kamati sio watu wenye uwezo wa kifedha ni watu wa hali ya chini na matajiri wanawaogopa kuongoza kuhofia kudhalilishwa na hao wanaotaka uongozi.

Sasa tujiulize mbona nchi zingine waislamu ni wachache na wana mafanikio? Mfano Kenya; wana vyuo vikuu, mashule n.k. Hii ni kwa sababu Kenya wanaosimamia misikiti ni wenye uwezo na Imamu analipwa kwa kusalisha na kutoa mahubiri. Mfano mwingine mzuri ni misikiti za madhehebu mengine tofauti na waafrika hapa Tanzania.

Malalamiko ya waislam

Waislamu wanalalamikia serikali na kuacha kujiuliza hivi ni kwanini sisi hatujiamini au ni kwanini tunawatumia matajiri wetu kwenye sadaka tu? Hivi wanaosimamia hii misikiti wana uwezo wa kutoa sadaka au mawazo ya kuendeleza watoto wetu huko mbeleni au wana uwezo wa kidunia ya kusimamia hospitali, shule na vyuo vikuu?

Ushauri wangu ni muanze na kamati za misikiti na mkaribishe wenye uwezo wa kielimu na kifedha. Msitibu dalili, tibuni ugonjwa na ugonjwa uko misikitini.

Nilimsikia shehe Khalifa na takwimu zake, na ni ukweli kuhusu hizo takwimu ila nia ya Rais Mungu ndio anaijua. Malalamiko lazima ya fanyiwe kazi kabla hayajaleta madhara.

Mfumo wa elimu

Dini zote za zamani viongozi wa kidini walikuwa wanapikwa toka utotoni na hivyo kuwafanya wawe na imani ya kweli na kazi zao mfano Mapadre, Mabuda, Mashehe wa zamani. Lakini mfumo ulivyobadilika kutoka wa zamani na kufuata mfumo wa kupeana digrii imefanya kila mwenye kuipata hata kama ni kichaa kutoa fatwa na kupata wafuasi.

Mfano huwezi kufananisha Padri na Mchungaji. Mchungaji ana historia yake na dhamira yake tofauti na Padre ambae toka kijana alikuwa akitayarishwa kuwa kiongozi.
 
hujui kiini cha malalamiko ya waislamu. Funga Domo lako

Uislam ndiyo kujibu kwa hasira na matusi?

Eleza basi kiini unachokijua wewe. Mambo ya imani hatutaki yahusishe serikali. Dini inayoshindwa kujisimamia katika katiba huru, ife. Maana yake imeshindwa kuonyesha umuhimu wake. Na inapokata roho, ife kwa amani ama kwa fujo bila kuathiri watu wengine. Kila mtu afanye dini aitakayo bila kuvuruga watu wengine.
 
Uongozi Katika uislam.

-Uongozi tunaozungumzia siyo wa kiimani ila kwenye kila msikiti kuna Imam na kuna kamati,Tatizo ni kwenye hizi Kamati,Misikiti nyinge miaka ya nyuma ilikuwa ikiongozwa na Bakwata na waliijenga kwa misingi ya ufisadi na kupora mali bila ya kuwashirikisha waislamu wengi,na ili waweze kuendelea na huu ufisadi wamekuwa wakibadilisha katiba na kuhakikisha mali yote inasimamiwa na makao makuu na kuamuliwa na wachache bila ya kushirikisha waumini mikoani,hii ilipelekea kuundwa kwa kamati za watu wenye dhiki na kufanya wenye uwezo wa kifedha waache kuchangi na kukaa mbali na bakwata.

-Hivi sasa miskiti inayojengwa kwa kasi ni ya madhehebu ya Salafi(ansar suna),misikiti hizi hujengwa na waumini au wafadhili kama Islamic Foundation,Tatito liko pale pale wanao simamia kama kamati ya hizi miskiti ni kama mfumo wa Bakwata,wanao simamia au kamati siyo watu wenye uwezo wa kifedha ni watu wa hali ya chini na matajiri wanawaogopa kuongoza kuhofia kudhalilishwa na hao wanaotaka uongozi,

-Sasa tujiulize mbona nchi zingine waislamu ni wachache na wana mafanikio, mfano Kenya wana vyio vikuu ,mashule nk,Hii ni kwa sababu Kenya wanaosimamia miskiti ni wenye uwezo na Imamu analipwa kwa kusalisha na kutoa mahubiri,au miskiti za madhehebu mengine tofauti na waafrika hapa Tanzania.

Malalamiko ya waislamu.

Waislamu wanalalamiki serikali na kuacha kujiuliza hivi ni kwanini sisi hatujiamini au ni kwa nini,Tunawatumia Matajiri wetu Kwenye sadaka tu,hivi wanasimamia hizi miskiti wanauwezo wa kutoa sadaka au mawazo ya kuendeleza watoto wetu huko mbeleni au wana uwezo wa kidunia ya kusimamia Hospitali,shule,vyio vikuu?ushauri wangu muanze na kamati za miskiti mkaribishe wenye uwezo wa kielimu na kifedha,Msitibu Dalili tibuni ugonjwa na ugonjwa iko miskitini.

Ni limsikia shehe Khalifa na takwimu zake,ila ni ukweli kuhusu hizo takwimu ila nia ya Rais mungu ndiyo anajuwa,ila malalamiko lazima ya fanyiwe kazi kabla hayajaleta madhara,

Mfumo wa elimu

Dini zote za zamani viongozi wa kidini walikuwa wana pikwa toka utotoni na hivyo kuwafanya wawe na imani ya kweli na kazi zao mfano,padre,mabuda, mashehe wa zamani,lakini mfumo ulivyo badilika kutoka wa zamani na kufuata mfumo wa kupeana digri imefanya kila mwenye kuipata hata kama ni kichaa kutoa fatwa na kupata wafuasi,mfano huwezi kufananisha PADRI na Mchungaji ,mchungaji ana historia yake na dhamira yake tofauti na padre ambae toka kijana alikuwa akitayarishwa kuwa kiongozi.

Wewe unapokuwa muumini wa dini yako, unapashwa kuzungumzia dini unayoifahamu. Ukisema Padri na Mchungaji, sijui unapima nini kwa sababu kila mtu anaimani tofauti na mwingine. Mapadri wanaimani yao wanayofundishwa na Wachungaji nao wana imani yao ambayo ni tofauti na mapadre.

Ninatamani ungeishia kusema serikali haihusiki na matatizo ya dini kwa sababu imeruhusu uhuru wa kuabudu bila kuingiliwa na bila kuvunja sheria. Dini zitumie uhuru wa kikatiba uliopo kufanya imani zao lakini zisilazimishe kuiburuta serikali katika failures zake.

Masuala ulioyaelezea nimeyapenda pale ulipojikita kwenye uongozi, miundo na mifumo ya dini. Kuanzia hapo dini zijue kujitegemea bila kuhujumu wala kuburuta mifumo mingine ifuate vile dini hizo zinataka kwa sababu imani ni hiyari ya mtu. Anayeona imani yake inakufa, ajue ameshindwa yeye kwa kuwa hakuna sheria ya nchi inalazimisha ustawi ama ufu wa imani yoyote.
 
Uongozi katika Uislam

Uongozi tunaozungumzia siyo wa kiimani ila kwenye kila msikiti kuna Imam na kuna kamati. Tatizo ni kwenye hizi Kamati, misikiti mingi miaka ya nyuma ilikuwa ikiongozwa na BAKWATA na waliijenga kwa misingi ya ufisadi na kupora mali bila ya kuwashirikisha waislamu wengi.

Na ili waweze kuendelea na huu ufisadi wamekuwa wakibadilisha katiba na kuhakikisha mali yote inasimamiwa na makao makuu na kuamuliwa na wachache bila ya kushirikisha waumini mikoani. Hii ilipelekea kuundwa kwa kamati za watu wenye dhiki na kufanya wenye uwezo wa kifedha waache kuchangia na kukaa mbali na BAKWATA.

Hivi sasa misikiti inayojengwa kwa kasi ni ya madhehebu ya Salafi(Ansar Sunna). Misikiti hii hujengwa na waumini au wafadhili kama Islamic Foundation. Tatizo liko palepale, wanaosimamia kama kamati ya hizi misikiti ni kama mfumo wa BAKWATA. Wanaosimamia au kamati sio watu wenye uwezo wa kifedha ni watu wa hali ya chini na matajiri wanawaogopa kuongoza kuhofia kudhalilishwa na hao wanaotaka uongozi.

Sasa tujiulize mbona nchi zingine waislamu ni wachache na wana mafanikio? Mfano Kenya; wana vyuo vikuu, mashule n.k. Hii ni kwa sababu Kenya wanaosimamia misikiti ni wenye uwezo na Imamu analipwa kwa kusalisha na kutoa mahubiri. Mfano mwingine mzuri ni misikiti za madhehebu mengine tofauti na waafrika hapa Tanzania.

Malalamiko ya waislam

Waislamu wanalalamikia serikali na kuacha kujiuliza hivi ni kwanini sisi hatujiamini au ni kwanini tunawatumia matajiri wetu kwenye sadaka tu? Hivi wanaosimamia hii misikiti wana uwezo wa kutoa sadaka au mawazo ya kuendeleza watoto wetu huko mbeleni au wana uwezo wa kidunia ya kusimamia hospitali, shule na vyuo vikuu?

Ushauri wangu ni muanze na kamati za misikiti na mkaribishe wenye uwezo wa kielimu na kifedha. Msitibu dalili, tibuni ugonjwa na ugonjwa uko misikitini.

Nilimsikia shehe Khalifa na takwimu zake, na ni ukweli kuhusu hizo takwimu ila nia ya Rais Mungu ndio anaijua. Malalamiko lazima ya fanyiwe kazi kabla hayajaleta madhara.

Mfumo wa elimu

Dini zote za zamani viongozi wa kidini walikuwa wanapikwa toka utotoni na hivyo kuwafanya wawe na imani ya kweli na kazi zao mfano Mapadre, Mabuda, Mashehe wa zamani. Lakini mfumo ulivyobadilika kutoka wa zamani na kufuata mfumo wa kupeana digrii imefanya kila mwenye kuipata hata kama ni kichaa kutoa fatwa na kupata wafuasi.

Mfano huwezi kufananisha Padri na Mchungaji. Mchungaji ana historia yake na dhamira yake tofauti na Padre ambae toka kijana alikuwa akitayarishwa kuwa kiongozi.
jinga kweli wewe
 
Matatizo yenu waislamu wenye akili na mali mnawafukuza kwenye uongozi,halafu mnabaki na viongozi wajinga halafu mnategemea kushindana,jiulize kwanini mhindi au mwaarabu akiongoza mnasogea,njie waswahili ni kula tu na kulalamika.
 
Dini ya kiislam ni miongini mwa dini zenye karne nyingi katika ardhi ya Tanzania lakini imekuwa na maendeleo duni kwenye mambo ya huduma za kijamii.

Hili litaendelea kuwatafuna endapo hawatabadili mfumo wa kufikiri.

Miaka ya 1980 mwishoni wazungu walianza kukata misaada kwa makanisa ya Africa hususani Katoliki.Wakatoliki walipogundua hilo walianza kutunga nyimbo za kuhamasisha waumini kuchangia wao wwnyewe kwa ajili ya mawndeleo ya kanisa na kusahau misaada ya ulaya.Hii namna moja wapo ya kujitathimini na kubadili mfumo wa kufikiri.Huo ulikuwa mfano tu.

Ndugu zetu waislam hamuwezi kujikwamua kwa kuilalamikia serikali kila uchao .Tafakari nini kinawakwamisha na mkitatue.Serikali haiwezi kuwa mtatuzi wa matatizo yenu.

Jiulizeni tangu serikali ya awamu ya tatu ilipowapa Chuo kikuu pale Morogoro mmeongeza vyuo vikuu vingapi ?

Badilikeni wakuu .Walau serikali zinazoongizwa na wakristu huwa zinawajali.Mfano ,Mkapa na chuo cha Morogoro, Magufuli na kuwaombea msikiti kwa mfalme wa Morocco na Makonda kuwaombea jengo la Bakwata.

Kama ndugu zetu hamtajitafakari upya mtapitwa na madhehebu ya kikristo yaliyoanzishwa miaka hii ya karibuni kama akina Gwajima, Mwingila na wengineo.

Kila la heri ndugu zetu.
 
Ungejua nani alianzisha BAKWATA nadhani usinge hangaika.

Na angejua nani anaongoza BAKWATA ndio angeshangaa kabisa.

Kwa taarifa yako BAKWATA inaendeshwa na kuongozwa na BARAZA LA WAKRISTO TANZANIA ndio maana mambo hayaendi kabisa.Siku BAKWATA ikiongozwa na waislam wenyewe hakika mashule,misikiti,mahospital makubwa kuliko Bugando na KCMC yatajengwa mavyuo makubwa kuliko Tumaini University na Dodoma University yatajengwa bila wasiwasi wowote.
 
Mfano mmoja mzuri sana, miaka ya nyuma mjini singida alotokea kijana mmoja tajiri na kujitolea kujenga msikiti mkuu pale mjini, alisema mimi nitasimamia na kuumaliza huu msikiti, wazee wa mjini wakakataa, wakamwambia kama unataka kusaidia basi ni lazima pesa tukabidhiwe sisi halafu tuujenge huu msikiti, jamaa akagoma akihofia hela kuliwa, wazee walivyo ona jamaa amekomalia kujenga yeye wakamwambia kuwa hawako radhi msikiti ujengwe. Sasa hapo ndio utajua tatizo liko wapi. Mtu amejitolea kujenga halafu wazee wenye njaa wanagoma kisa hawata pata maslahi yeyote.
 
Tatizo liko kwe nye baadhi ya matabaka ya kiislamu. Sunni wengi ni wapigaji. Mbona hatusikii matatizo kwenye misikiti ya ibadhi. Misaada inatoka Oman lakini wanahakikisha wanaweka mtu wao kusimamia ujenzi, shehe wa msikiti anapewa mshahara, mapato yote ya msikiti yanasimamiwa na wafanya biashara wakubwa. Waganga njaa wote pembeni. Tazama msikiti wa ibadhi Mwanza na Dar, yote miwili haina tatizo hata moja.
 
Ni kama mtoa mada yako sahihi, tatizo lingine labda ni ule ukosefu wa nadhani inaitwa 'hierarchy' misikiti haina organization moja na makanisa yaliyo chini ya mfumo wa kipentekoste vilevile .tofauti na wakatoliki ambao wanajua nani mwamuzi wa mwisho na rufaa zinawezekana kimkoa,kitaifa,na kimataifa,, Kwa mantiki hiyo kuna lengo kuu na malengo madogomadogo ya pamoja,
Upentekosteni na msikitini tukivuragana hapa nahamia pale na hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji kupokelewa kwangu.
 
Siku BAKWATA ikiongozwa na waislam wenyewe hakika mashule,misikiti,mahospital makubwa kuliko Bugando na KCMC yatajengwa mavyuo makubwa kuliko Tumaini University na Dodoma University yatajengwa bila wasiwasi wowote
Tunaisubiri hiyo siku mkuu .........>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
 
Tunaisubiri hiyo siku mkuu .........>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Ukweli bakwata walianzisha matatitizo,lakini hivi sasa miskiti mengine tayari ni mengi kuliko bakwata,sasa shida ni kamati za walala hoi kusimamia miskiti,hata saud arabia leo miskiti yote inasimaiwa na matajiri,kenya pia leo kenya kuna zaidi ya vyuo vikuu 4 na zinasimamiwa na matajiri,hapa kwetu tajiri atoe hela waliokwenye kahawa ndio waipangie kazi.
 
Back
Top Bottom