Happy nation
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 679
- 591
Uongozi katika Uislam
Uongozi tunaozungumzia siyo wa kiimani ila kwenye kila msikiti kuna Imam na kuna kamati. Tatizo ni kwenye hizi Kamati, misikiti mingi miaka ya nyuma ilikuwa ikiongozwa na BAKWATA na waliijenga kwa misingi ya ufisadi na kupora mali bila ya kuwashirikisha waislamu wengi.
Na ili waweze kuendelea na huu ufisadi wamekuwa wakibadilisha katiba na kuhakikisha mali yote inasimamiwa na makao makuu na kuamuliwa na wachache bila ya kushirikisha waumini mikoani. Hii ilipelekea kuundwa kwa kamati za watu wenye dhiki na kufanya wenye uwezo wa kifedha waache kuchangia na kukaa mbali na BAKWATA.
Hivi sasa misikiti inayojengwa kwa kasi ni ya madhehebu ya Salafi(Ansar Sunna). Misikiti hii hujengwa na waumini au wafadhili kama Islamic Foundation. Tatizo liko palepale, wanaosimamia kama kamati ya hizi misikiti ni kama mfumo wa BAKWATA. Wanaosimamia au kamati sio watu wenye uwezo wa kifedha ni watu wa hali ya chini na matajiri wanawaogopa kuongoza kuhofia kudhalilishwa na hao wanaotaka uongozi.
Sasa tujiulize mbona nchi zingine waislamu ni wachache na wana mafanikio? Mfano Kenya; wana vyuo vikuu, mashule n.k. Hii ni kwa sababu Kenya wanaosimamia misikiti ni wenye uwezo na Imamu analipwa kwa kusalisha na kutoa mahubiri. Mfano mwingine mzuri ni misikiti za madhehebu mengine tofauti na waafrika hapa Tanzania.
Malalamiko ya waislam
Waislamu wanalalamikia serikali na kuacha kujiuliza hivi ni kwanini sisi hatujiamini au ni kwanini tunawatumia matajiri wetu kwenye sadaka tu? Hivi wanaosimamia hii misikiti wana uwezo wa kutoa sadaka au mawazo ya kuendeleza watoto wetu huko mbeleni au wana uwezo wa kidunia ya kusimamia hospitali, shule na vyuo vikuu?
Ushauri wangu ni muanze na kamati za misikiti na mkaribishe wenye uwezo wa kielimu na kifedha. Msitibu dalili, tibuni ugonjwa na ugonjwa uko misikitini.
Nilimsikia shehe Khalifa na takwimu zake, na ni ukweli kuhusu hizo takwimu ila nia ya Rais Mungu ndio anaijua. Malalamiko lazima ya fanyiwe kazi kabla hayajaleta madhara.
Mfumo wa elimu
Dini zote za zamani viongozi wa kidini walikuwa wanapikwa toka utotoni na hivyo kuwafanya wawe na imani ya kweli na kazi zao mfano Mapadre, Mabuda, Mashehe wa zamani. Lakini mfumo ulivyobadilika kutoka wa zamani na kufuata mfumo wa kupeana digrii imefanya kila mwenye kuipata hata kama ni kichaa kutoa fatwa na kupata wafuasi.
Mfano huwezi kufananisha Padri na Mchungaji. Mchungaji ana historia yake na dhamira yake tofauti na Padre ambae toka kijana alikuwa akitayarishwa kuwa kiongozi.