Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,785
- 10,183
Samahani wana JF, nimekuwa nikipata sana shida kupiga simu katika mtandao wa Vodacom nyumbani (niko nje ya nchi), sijajua shida iko wapi! Kuna wakati huwa nikipiga simu inaita kama kawaida ila huwa haipokewi na nikituma ujumbe mtu niliyekuwa nikimpigia anasema simu haijaita wala nini, sasa hii huwa inanipa wakati mgumu sana! Mara nyingine huwa nikipiga, simu inakuwa inatafuta line muda wote tu bila majibu, sasa huwa nakereka sana! Nikituma Ujumbe unaenda kama kawaida! Nilidhani ni mtu mmoja tu mwenye shida hii, lakini nikaja kugundua kuwa ni line zote za vodacom zina shida ya namna hii nikipiga toka huku nje niliko. Kama kuna maelezo yoyote ya kutatua kadhia hii kutoka kwa wahusika (Vodacom) nitafurahi sana. Nilishakutana na mtu akilalamikia shida ya namna hii katika blogu fulani maarufu! Naomba kusaidiwa shida hii!