Matatizo ya tumbo na miguu kuwaka moto

kinywanyuku

JF-Expert Member
Jul 13, 2015
3,557
2,626
Wadau mama yangu anasumbiliwa na matatizo haya toka mwaka 1982 anahisi vidonda vya tumbo hajawahi kupima,hii ni sms yake aliyonitumia kashindwa kwenda kazini anaumwa Nina tatizo nikila mboga zenye nyanya tumbo linauma naharisha kinyesi cha njano vidonda kooni haviponi koo linawasha sana kama fangus, pua, masikio, macho na upande wa kulia unauma kwa ndani kama kuna kidonda linakua lamoto sana, miguu inawaka moto kama nimeungua pia inavimba sana kwenye kiungio cha kukakanyaga
 
Atakuwa na Vidonda vya tumbo na maradhi mengine yanayo msumbuwa mwilini. Anaweza kutibiwa na dawa zetu za asili na akapona maradhi yake.

Kitu Muhimu kwanza aende kupima Hospitali kisha uje hapa utuambie ameambiwaje huko kwenye Vipimo vya kizungu aka Hospitali? kisha tunaweza kumtibia na atapona kabisa maradhi yake auguwe pole.
 
Atakuwa na Vidonda vya tumbo na maradhi mengine yanayo msumbuwa mwilini. Anaweza kutibiwa na dawa zetu za asili na akapona maradhi yake. Kitu Muhimu kwanza aende kupima Hospitali kisha uje hapa utuambie ameambiwaje huko kwenye Vipimo vya kizungu aka Hospitali? kisha tunaweza kumtibia na atapona kabisa maradhi yake auguwe pole.
Nashukuru mkuu unapatikanaje
 
Kupandisha kinga unafanyaje
Kupandisha kinga ,kunategemea na nin kimesababisha kinga kushuka.

Inaweza kua kisukari? maambukizi ya kisasa ? Umri ? Matumiz ya muda mrefu ya baadhi ya madawa? Madawa ya kansa ? N.k

So ukijua kisababishi, ni rahis kujua namna ya kuipandisha kinga.
 
Miguu kuwaka moto atafune vitunguu swaumu usiku na asubuhi...wiki moja tu tatizo limeisha....hivo vidonda vya tumbo kiboko yake ni baking soda au baking powder (ile ya kupikia maandazi) alambe kwa wiki moja tu vitaisha...Huyo ana acid nyingi sana....aache kula nyanya ,NANASI, machungwa etc...
 
Embu mkuu, Fanya kitu kimoja, mchukue Mama umpeleke Hosp na Huko atatoa maelezo kamili ambayo yatatoa Picha halisi ya Aina ya Vipimo ambavyo Mama anatakiwa kufanyiwa.
 
Wadau mama yangu anasumbiliwa na matatizo haya toka mwaka 1982 anahisi vidonda vya tumbo hajawahi kupima,hii ni sms yake aliyonitumia kashindwa kwenda kazini anaumwa Nina tatizo nikila mboga zenye nyanya tumbo linauma naharisha kinyesi cha njano vidonda kooni haviponi koo linawasha sana kama fangus, pua, masikio, macho na upande wa kulia unauma kwa ndani kama kuna kidonda linakua lamoto sana, miguu inawaka moto kama nimeungua pia inavimba sana kwenye kiungio cha kukakanyaga
Mkuu Bimkubwa alikwisha pata tiba ya matatizo yake?
 
Atakuwa na Vidonda vya tumbo na maradhi mengine yanayo msumbuwa mwilini. Anaweza kutibiwa na dawa zetu za asili na akapona maradhi yake.

Kitu Muhimu kwanza aende kupima Hospitali kisha uje hapa utuambie ameambiwaje huko kwenye Vipimo vya kizungu aka Hospitali? kisha tunaweza kumtibia na atapona kabisa maradhi yake auguwe pole.
Oi MziziMkavu nimekuwa nikisumbuliwa sana na gesi kujaa tumboni na tumbo kuunguruma mda mwingi sana! Nimekwishapima vidonda vya tumbo kama mara nne hivi lakin mara zote naambiwa sina vidonda! Kuna namna ya kulimaliza hili tatizo kabisa?
 
Back
Top Bottom