Matatizo ya Traffic Barabarani wanapanga njama na madereva bodaboda na raia wengine kukamatisha watu

Guantanamoh

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
1,983
4,170
Hivi matraffic mnaokaa barabarani kuvizia makosa huwa mnawaza nini kupanga watu wa kuwasaidia kuwakamatisha madereva, yaani scenario ziko hivi: unaweza ukawa unatembea kwenye kimteremko barabarani, alafu mbele unaona kuna dereva bodaboda kama anasua sua kwenda ili mradi tu umkwepe alafu mbele unakuta wazee wamekaa wanakungoja kukupiga fine ya ku overtake sehemu ambayo sio salama.

Sasa kwenye mteremko kama mtu wa mbele yangu ana sua sua kwanini nisimkwepe? Nikimgonga je? Na sehemu nyingine ni kwenye zebra.

Unakuta mtu anapewa kazi ya kuvuka upande mmoja kwenda mwengine hata zaidi ya mara 10 anavizia ule

Muda gari ilisimama yeye havuki alafu gari ikitaka kutoka yeye ndo anajifanya anataka kuvuka na traffic ndo anajifanya ameona tukio hilo.

Matraffic kuweni makini. Haya maswala mnayafanyia biashara sana. Yaani zebra na sehemu za ku overtake mmefanya kama biashara yenu. Muwe mna angalia na mazingira. Madereva wengine sio rough lakini mtu anaona aepushe ajali kumbe nyie mmemuwekea
Mtego.

🙌🏽2. Na balaa lingine kubwa kuliko naomba serikali iliangalie swala na madaladala kusimama popote na kushusha au kupakia abiria wakati vituo viko wazi. Hao ndo wanasababisha foleni kuliko kawaida. Unakuta gari zimeongozana zimesimama high way zinapakia abiria lakini traffic haoni anasubiri

U overtake akudake. Angalieni sana nyendo mnazofanya. Serikali imeondoa machinga lakini swala la madaladala kuzagaa hadi highway kusubiri abiria ni kero zaidi ya hizo zingine maana mnasababisha foleni.
 
Back
Top Bottom