Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,315
- 33,111
Matatizo na magonjwa ya kawaida
Katika sehemu hii, utajifunza kuhusu magonjwa na matatizo ya kawaida ya meno. Baadhi iya matatizo haya huenda yatakuathiri hata kama unatunza meno yako vizuri. Ingawa unaweza ukayazuia baadhi kwa kusugua meno na kuondoa chakula iliyokwama kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli mara mbili kwa siku; kumwona daktari wa meno mara kwa mara, kutovuta sigara na kula vizuri
Alama ya uchafu/madoadoa kwenye meno
Tumbaku, baadhi ya vyakula na vinyaji vyaweza kufanya meno yetu kuwa na alama ya uchafu na madoadoa kadri tunavyozidi kuzeeka. Alama hizi za uchafu au madoadoa hayasabibishi tatizo lolote la afya. Lakini watu wengi wanatamani kuwa na meno meupe.
Ni nini husababisha alama za uchafu au madoadoa kwenye meno
Baadhi ya vitu vinavyosababisha hali hii ni pamoja na:
Unatibu vipi?
Ikiwa meno yako yana madoadoa au uchaafu, jaribu dawa ya meno itakayofanya yawe meupe. Unaweza kwenda kwa daktari wa meno akaya pausha ingawa ni bei ghali sana. Dawa ya meno husaidia sana ingawa hufanya kazi polepole.
Mashimo
Mashimo ni nini?
Mashimo ni uwazi ulio kwenye meno yako na hutokana na meno kuoza. Ingawa ni rahisi sana kuzuia mashimo, ni watu wengi huwa na mashimo. Daktari wako wa meno anaweza akakutibu mapengo ila ni vyema sana kuyatibu kabla hayajazidi au kuwa makubwa au kusabisha maumivu ya meno, ufizi kufura au uchungu wowote ule.
Njia zitakazokuwezesha kuzuia mashimo:
Picha za baadhi ya maradhi ya meno
Tooth Enamel
Bruxism: Effects of Teeth Grinding
Bulimia: Impact on Oral Health
Teeth Damaged by Bulimia
Katika sehemu hii, utajifunza kuhusu magonjwa na matatizo ya kawaida ya meno. Baadhi iya matatizo haya huenda yatakuathiri hata kama unatunza meno yako vizuri. Ingawa unaweza ukayazuia baadhi kwa kusugua meno na kuondoa chakula iliyokwama kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli mara mbili kwa siku; kumwona daktari wa meno mara kwa mara, kutovuta sigara na kula vizuri
Alama ya uchafu/madoadoa kwenye meno
Tumbaku, baadhi ya vyakula na vinyaji vyaweza kufanya meno yetu kuwa na alama ya uchafu na madoadoa kadri tunavyozidi kuzeeka. Alama hizi za uchafu au madoadoa hayasabibishi tatizo lolote la afya. Lakini watu wengi wanatamani kuwa na meno meupe.
Ni nini husababisha alama za uchafu au madoadoa kwenye meno
Baadhi ya vitu vinavyosababisha hali hii ni pamoja na:
- Uvutaji wa sigara au biri na kutafuna tumbaku. Matumizi ya aina yoyote ya tumbaku yanaweza kuleta ugonjwa wa kansa, ikiwemo kansa ya kinywa. Uchungu ukizidi kwa muda wa siku mbili na zaidi, muone daktari wa meno, labda una jino lililovunjika
- Vinyaji kama vile chai, kahawa, mkola na mvinyo wenye rangi nyekundu husababisha kuwepo na madoadoa kwenye meno. Chai na mvinyo nyekundu ni nzuri au bora kwa afya yako, lakini hakikisha kuwa umesugua meno baada ya kuvinywa.
- Matunda kama vile beriberi ni nzuri pia, lakini huchafua meno. Sugua meno yako baada ya kuyala.
Unatibu vipi?
Ikiwa meno yako yana madoadoa au uchaafu, jaribu dawa ya meno itakayofanya yawe meupe. Unaweza kwenda kwa daktari wa meno akaya pausha ingawa ni bei ghali sana. Dawa ya meno husaidia sana ingawa hufanya kazi polepole.
Mashimo
Mashimo ni nini?
Mashimo ni uwazi ulio kwenye meno yako na hutokana na meno kuoza. Ingawa ni rahisi sana kuzuia mashimo, ni watu wengi huwa na mashimo. Daktari wako wa meno anaweza akakutibu mapengo ila ni vyema sana kuyatibu kabla hayajazidi au kuwa makubwa au kusabisha maumivu ya meno, ufizi kufura au uchungu wowote ule.
Njia zitakazokuwezesha kuzuia mashimo:
- Sugua meno yako, kisha uondoe chakula iliyo kwenye meno kwa kutumia uzi spesheli na umuone daktari wa meno mara kwa mara
- Usile peremende kwa wingi na vyakula vitamu au vinywaji vingi vilivyo baridi na vinywaji vitamu. Jizoeshe kunywa kinywaji kimoja baridi kwa siku au peremende kidogo.
- Kula matunda na mboga (itakayosafisha meno yako) ama jibini na mtindi (ambazo ni nzuri kwa meno na ufizi wako) kama kumbwe
- Ili kutengeneza mate, tafuna sandarusi isiyo na sukari baada ya vyakula. Mate huwa na kemikali inayozuia meno kuoza.
- Hakikisha kuwa unatumia dawa ya meno iliyo na floraidi. Floraidi hufanya meno yako kuwa na nguvu.
- Dalili au ishara huwa zipi
- Ukiona doa nyeusi au hudhurungi (kahawia) kwenye meno au wasikia maumivu ya meno ambayo haishi muone daktari wa meno haraka iwezekanavyo. Usipoende kupata matibabu ya meno, uozo uliopo kwenye meno huenda ikasababisha matatizo mengine kama vile kufura kwa ufizi, maumivu kwenye taya na kichwa kuuma.
- Unatibu vipi?
- Safisha/sugua meno yako vizuri, kula vyakula bora na upate uchunguzi wa meno mara kwa mara ili kuzuia matatizo haya.
Picha za baadhi ya maradhi ya meno