Matatizo ya kupiga simu muda mrefu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya kupiga simu muda mrefu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Grader, Jul 18, 2009.

 1. Grader

  Grader JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 446
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ajeruhiwa na Mumewe kwa Wivu wa Kimapenzi
  MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Mariam Hassan[23]mkazi wa Sinza jijini Dar es SAlaam, amejeruhiwa na mumewe kutokana na sababu za wivu wa kimapenzi kwa kuwa aliongea na simu kwa muda mrefu na rafiki yake kitendo ambacho mumewe kilimuudhi
  Mwanamke huyo alijeruhiwa usoni kwa kupigwa magumi na muwewe huyo kwa kile kilichosemekana mumewe alipatwa na jazba kwa kuwa aliongea na simu kwa muda mrefu na mtu ambaye hakumfahamu.

  Dada huyo akiongea na Nifahamishe alisema kuwa juzi alipigiwa simu na rafiki yake ambaye kwa muda mrefu walikuwa wamepotezana.

  Alisema kuwa mtu aliyempigia simu alikuwa ni kijana aliyemtaja kwa jina moja la Hamisi ambaye walisoma wote shule ya msingi Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar.

  Alisema kuwa aliongea na kijana huyo zaidi ya masaa matatu na baada ya kumaliza kuongea na simu hiyo aliulizwa na muwewe alikuwa anaongea na nani na kumjibu ni rafiki yangu anaitwa Hamisi nilisoma nae ndio amenipigia.

  Kumbe mumewe huyo wakati anajibiwa hivyo na mkewe huyo hakuridhika majibu hayo na kumwambia kuwa alikuwa akiongea na mpenzi wake na kuanza kumpa kichapo ambacho hakukitegemea kwa wakati huo.

  Alisema alijitahidi kujitetea kadri alivyoweza lakini muwewe huyo hakuridhika na kumshambua na kumwambia anadiriki kuongea na mabwana zake mbele yake.

  Dada huyo alijeruhiwa sehemu zake za usoni na kupelekea hadi kupata uvimbe na kuvilia damu kwa ngumi ambazo alitandikwa na muwewe huyo.
   
 2. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 3. Robweme

  Robweme Senior Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli, nampongeza ngoja amchape.Hana heshima kabisa huyo dada, inaonekana jamaa naye aliokota huyo demu.Huyo dada baada ya kujua ni mwanaume alitakiwa kumwambia basi nitakupigia niko busy.Sasa kama aliongea nae masaa 3 huoni wakikutana watakumbushana yale ya zamani.Alitakiwa kumweleza bwana habari ya siku nyingi, alafu kwakumheshimu mumewe amwambie okay nitakupigia.
  Huyo dada sio mke, jamaa anatakiwa kumwona kuwa hamna heshima hapo.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni mshenzi sana huyu mwanamke.
  How come unaongea na saa masaa3 wakati bwanako yupo ndani?
  Mbali ya wivu, lakini pia huyo mwanamke inaonyesha hakufanya majukumu yake ya ndani kwa muda wote huo, what a nonsense?
  Alitakiwa arudishwe kwao fasta maana ana dharau kubwa mno!
  Ni mambo gani utaongea na kijana wa kiume kwa masaa3 kama si kubaniana pua?
  Shiiit!
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha ushenzi jamani alipitiwa tu loh..... ingawa ni kweli alikosea ila je ninyi kina sham huwa mnalizingatia hilo eti mpenzio yuko ndani ukatishe mazungumzo yako na marafiki zako?

  Huwa mnatugandishaga sana hasa mkiwa mwenye viti virefu!
   
 6. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha ha nimecheka sana wamekuwa wakali kama pilipili. .... kwenye comment za jamaa hapo juu....jamani hakuna kitu inauzi kama hiyo bana.....yaani hizi extreme za call....zinaweza fanya ukapiga mtu...the same mtu mnaongea nae yeye yuko busy ku reply sms kwa marafiki na jamaa...

  Unakuwa not conftable kabisa...hii nilikuwa nayo zamani..lkini kulingana na wakati nimegundua ninavyo udhika mie na wengine huudhika vile vile..kwa kutopata antension.
   
 7. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nilishasema kwenye post moja kuwa wivu kwenye mapenzi ni
  -hasara
  -majuto
  -kifo
  -kilio
  -kiama
  -huzuni
  -presha
  -n.k, n.k

  ingawa huyu bibie alikosea sana, three hours analonga-longa na kidume wakati mumewe anasubiri kutengewa maji au kupepewa na ili joto la bongo, nway ni part and parcel ya dicsipline
   
 8. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Pole sana bibie. Next time ujue simu ni kama dawa za waingereza "shake well before use"
   
 9. afkombo

  afkombo Member

  #9
  Jul 19, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Bint kwa kweli amekosea sana!!Ataongeaje na mvulana masaa matatu hata kama ni rafiki au ni nani,maana hata kama angekuwa anaongea na msichana pia inaboa kimtindo!!
   
 10. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kweli dada huyo alikosea kabisa kuongea masaa matatu kwenye simu. Hata kama huyo jamaa walisoma naye na walipotezana muda mrefu, kwa kweli kuongea masaa matatu kwenye simu inaonyesha wazi kuwa enzi hizo walikuwa na mambo fulani.
  Hata mimi kuna jamaa zangu ambao tumesoma wote primary school na hatujawahi kuonana toka tumalize elimu ya msingi. Hata tukionana ghafla au kupata mawasiliano kama hayo ya simu kwa kweli hata dakika 5 ni nyingi.

  Alichotakiwa kufanya huyo dada ni kutafuta muda mzuri waonane kisha waongee mambo yao kama ni mazuri.

  Pia kuongea na simu muda mrefu kunaweza kuwa na madhara kiafya.

  Ngoja niishie hapo kwanza.
   
Loading...